Jumatatu, 15 Septemba 2014

TUWAJIBIKE MAMA AISHI

Kutoka Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama ndani ya siku 500 kuelekea ukomo wa tarehe iliyowekwa kwa Malengo ya Milenia

Kwa niaba ya Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi  Salama Tanzania, naungana na wanawake na familia zao duniani, kufurahia mafanikio ya kampeni ya dunia ya kuzuia  vifo vya kina mama na watoto wachanga wakati wa ujauzito, kujifungua na baada ya kujifungua. Ilivyo sasa idadi ya kina mama wanaofariki kutokana na uzazi ni nusu ya wale waliokua wanafariki miaka ishirini iliyopita- haya ni mafanikio makubwa. Hii i nadhihirisha tukiweka bidii zaidi kwa pamoja tunaweza kukifikia lengo tulilojiwekea.

Hata hivyo, pamoja na mafanikio haya bado tumekua tukipoteza wakina mama wengi. Hapa nchini, wanawake 24 wanafariki kila siku waki wa katika  harakati za kuendeleza kizazi kijacho. Mara nyingi, watoto wao pia hufariki na  hivyo familia zao husononeka sana.Tunaweza kufanya mambo mengi zaidi ilikuhakikisha usalama wa wakinamama wetu.Mheshimiwa Rais JakayaKikwete amekuwa akifanya kazi bila kuchoka katika kuzuia vifo hivi vya kusikitisha-na kila mmoja wetu anaweza kuchangia  katika kulinda  kinamama wetu wakati wanapokua kati kajukumu la kuleta uhai duniani.
Muungano wa Utepe Mweupe duniani na nchini  tumekuwa tukihamasisha viongozi kuweka kipaumbele katika mipango ya maendeleo  kwa kuhakikisha vifo vya kina mama na watoto wachanga wakati wa uzazi vinatokomea kabisa. Tunaona mabadiliko makubwa. Suala la afya ya mama na mtoto limekua likijadiliwa katika mikutano ya  kidunia na katika bunge letu.Wiki iliyopita kulikuwa na mkutano wa viongozi wa bara la Afrika nchini Marekani ambapo mwenyeji wake alikua  Rais Baraka Obama.  Walijadili kuhusu mambo ambayo tunaweza kufanya ili kuokoa maisha ya  akina mama wakati wa uzazi Mh. Rais na Mama Salma Kikwete walihudhuria mkutano huu  na walijadili mambo mengi kuhusu afya ya uzazi hapa Tanzania. Kwa kuwa uongozi wakidunia na wa hapa nchini tuna utayari,  natumaini kwamba , tunaweza tukaweka rekodi na kufanya vifo vya  kina mama kutokomea na kuwa historia katika nchi yetu.
Tunajua kwamba kina mama wengi hufariki kwa sababu   wanajifungulia majumbani bila  msada wa wakunga au watumishi wa afya wenyesifa. Kwa hiyo tunatoa rai kwa viongozi wafanye kila njia ili kuhakikisha kwamba vituo vya afya vilivyo karibu na kina mama vina vifaa nawataalam wa kutosha ili viweze kutoa huduma inayohitajika na akina mama wajawazito hasa wakati wa dharura. Sisi kama Muungano  wa Utepe MweupeTanzania tumewajumuisha maelfu ya mashirika nawatu binafsi, waandishi wahabari na wanasiasa kupitia mikakati I   muhimu kwa ajili ya kuzuia vifovya akina mama na watoto wachanga. Tumeono  mafanikio ya kihistoria katika miezi ya hivi karibuni kwa serikali kuelekeza halmashauri zote kuwa na kasma maalum kwa ajili ya gharama za huduma za  dharura za mama na mtoto.
 
Viongozi wa dunia waliokusanyika kwa ajili ya Malengo ya  Milenia ya mwaka 2000 walitupa changamoto yakupunguza vifo vya kina mama kwa robo tatu (3/4) na vifo vya watoto kwa theluthimbili (2/3) kufikia mwaka 2015. Tumebaki na siku mia tano kuanzia leo kabla ya kufikia kikomo cha muda uliopangwa kwa ajili ya malengo haya. Ni lazima tuongeze kasi ya kufikia malengo  haya kwa siku hizi 500 za mwisho kwa kufanya kila linalowezekana ili kufikiaangala ukaribu na malengohaya kwa ajili ya kunusuru maisha ya mama na mtoto kabla, wakati na baada ya kujifungua.
 
 Tafadhali unganana Muungano wa Utepe Mweupe na timiza wajibu wako!
 Wajibika Mama Aishi!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...