Jumatatu, 15 Septemba 2014

HONGERA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA, KUSHIRIKI NA VIJANA KUFANYA USAFI MBALIZI


 Katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga, akizoa taka kwenye ghuba la stendi ya umalila, Mbalizi Mbeya, juzi, alipoongoza suala la kufanya usafi katika mji huo kwa ushirikiano wa wakuu wa idara za Halmashauri hiyo na kikundi cha vijana wazalendo Mbalizi(UVIWAMBA), ambao wanafanya kazi ya usafi katika mji huo kwa kujitolea.
 Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga,(kushoto), akimkabidhi Tsh.10,000/= mmoja wa watumishi wa halmashauri hiyo, baada ya juhudi zake za kufanya usafi siku ya jumamosi akishirikiana vema na kwa juhudi kubwa na vijana wa uviwamba na watumishi wenzake.


 Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga, akihojiana na waandishi wa habari, ambao walifika eneo la usafi Mbalizi juzi.
 Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga, akisukuma toroli lenye taka, akipeleka kwenye gari la taka tayari kwenda kumwagwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...