MKUU
wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro (DC), amewataka wananchi wa Kijiji cha
Namkukwe Kata ya Namkukwe Wilayani hapa, kuchangia Tsh,10,000/= kila mmoja, ili
kukamilisha ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Namkukwe.
Kauli
hiyo ameitoa wakati wa ukaguzi wa maabara katika kata
zote za wilaya ya Chunya ambapo alibaini kata ya
Namkukwe pekee ndiyo haijaanza ujenzi wa maabara.
Aliwapongeza wananchi wa kata ya Totowe kwa kwenda kasi na ujenzi
huo ambapo wamefikia hatua ya mtambaa panya na serikali itatoa milioni
13 kwa ajili ya kumalizia ujenzi huo na fedha hizo zitatumika kununulia
mabati na mbao kwa ajili ya kuezekea jengo hilo.
Kila
mwananchi wa Kata ya Totowe huchangia elfu sitini na tano kila mmoja na
kwa kuona umuhimu wa elimu wengi wameitikia mpango huo wa Taifa na
majengo yote nchini yanatakiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Kata
ya Namkukukwe kumekuwa na marumbano, na Mkuu wa wilaya amesema atakayekaidi atachukuliwa hatua za kisheria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni