Jumatano, 27 Agosti 2014

TAARIFA YA ULINZI NA USALAMA KANDA NO 2 MKOA WA MBEYA TAREHE 26.08.2014.



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.


 


       R.P.C                                                                                               Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                      Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572                                                                                          S. L. P. 260,
Fax -+255252503734                                                                                                    MBEYA.
E-mail:rpc.mbeya@tpf.com.tz
Unapojibu tafadhali taja 

MBR/C.5/900/VOL.I/251.                                                                  Tarehe: 26 Agosti, 2014.

Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P 9141,
DAR ES SALAAM.

                       YAH: TAARIFA YA ULINZI NA USALAMA KANDA NO 2 MKOA
                                                         WA MBEYA TAREHE 26.08.2014.

Tafadhali husika na kichwa cha habari tajwa hapo juu.
Pamoja na barua hii ninakutumia taarifa ya hali ya ulinzi na usalama Kanda no 2 Mkoa wa Mbeya ya  masaa 24 yaliyopita kufikia tarehe 26.08.2014.
Naomba kuwasilisha tafadhali.


                                                  [Barakael Masaki – ACP].
          Kny         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA


Nakala kwa:  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai,
                        Makao Makuu ya Upelelezi,
                        S.L.P 9093,
                        DAR ES SALAAM. - Kwa taarifa tafadhali.

                        Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai,
                        Mkoa wa Mbeya,
                        S.L.P 260,
                        MBEYA – Kwa taarifa




[i] MATUKIO YA UHALIFU/AJALI ZA USALAMA BARABARANI.
S/NO
Tarehe
Muda
Maelezo ya Kosa / Tukio.
Watuhumiwa
01.
26.08.2014
03:30hrs
MB/IR/6898/2014 – AJALI YA MOTO.
Huko Iyunga, Kata na Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Mtu mmoja aitwaye DAVID S/O IMWMAMU, miaka 39, Mkurya, DSO – Mbeya, Mkazi wa Iyunga aligundua kuungua kwa Nyumba aliyopanga inayomilikiwa na RICHARD S/O YAONDE, miaka 45, Mnyiha, Mfanyabiashara na Mkazi wa Sumbawanga yenye Vyumba Vitano [05]. Moto huo uliteketeza vitu vyote vilivyokuwa sebuleni, stoo pamoja na Master Bed Room na paa lote la Nyumba hiyo isipokuwa sehemu ndogo sana ya paa hilo. Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika. Moto huo ulizimwa kwa Jitihada za Kikosi cha Zima moto na Uokoaji, Askari Polisi pamoja na Wananchi. Thamani halisi ya mali iliyoteketea bado kufahamika. Hakuna madhara yoyote ya kibinadamu yaliyoripotiwa. Kiongozi wa Zone namba 01 Kanda A amekagua tukio, Upelelezi unaendelea.
---

[ii] MATUKIO YATOKANAYO NA MAFANIKIO YA DORIA/MISAKO.
S/NO
Tarehe
Muda
Maelezo ya Kosa / Tukio.
Watuhumiwa
01.
25.08.2014
16:30hrs
MB/IR/6880/2014 – KUPATIKANA NA BHANGI.
Huko Ilolo, Kata ya Sinde, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya, Zone namba 05, Kanda A. Askari Polisi wakiwa Doria/Msako waliwakamata 1. HANS S/O PIUS, miaka 27, Kyusa, Mkazi wa Ilolo 2. ZAWADI S/O ANDREW, miaka 22, Msafwa na Mkazi wa Sinde B 3. KINGSLEY S/O MWAMAJA, miaka 24, Kyusa, Mkulima na Mkazi wa Isanga na 4. SIKUJUA S/O ELIA, miaka 25, Kyusa, Mkulima na Mkazi wa Sangu wakiwa na Bhangi Uzito wa Gramu 03 ndani ya Mfuko wa kaki.
04
02.
25.08.2014
12:14hrs
MBO/IR/1261/2014 – KUPATIKANA NA RISASI ZA SMG NA SHORT GUN.
Huko katika Kitongoji cha Ilembo “B” Mtaa wa Ilembo, Kata na Tarafa ya Vwawa, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya, Zone namba 06 Kanda B. Askari Polisi wakiwa Doria/Msako walimkamata GABRIEL S/O MWAMPASHI, miaka 25, Mnyiha, Mkazi wa Ilembo “B” akiwa na risasi 07 za Bunduki aina ya SMG na risasi 01 ya Bunduki aina ya Short Gun nyumbani kwake wakati akiwa anapekuliwa kutokana na kuhusika na makosa ya Uvunjaji.

01
03.
25.08.2014
15:30hrs
MKI/IR/961/2014 – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Huko katika Kitongoji cha Mamba, Kata ya Mamba, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Zone namba 23. Askari Polisi wakiwa Doria/Msako waliimkamata DAUDI S/O GABRIEL@ BUKUKU, miaka 32, Kyusa, Mkulima na Mkazi wa Mamba “A” akiwa na Pombe Haramu ya Moshi [Gongo] ujazo wa lita 07 Nyumbani kwake. Mtuhumiwa ni Muuzaji wa Pombe hiyo.
01

[iii] MATUKIO YATOKANAYO NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA.
S/NO
Tarehe
Muda
Maelezo ya Kosa / Tukio.
Watuhumiwa
   --
--
      --
--
--

A: Migogoro /Maafa- Hakuna.
Ø  Kisiasa – Umefanyika Mkutano wa Chama cha Siasa cha Chadema Huko katika Kata ya Itiji, Tarafa ya Sisimba, Mkoa wa Mbeya. Katika Mkutano huo Mgeni Rasmi alikuwa ni Mbunge wa Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi ambaye alikuwa amefuatana na Viongozi Waandamizi wa Chadema ngazi ya Mkoa na Wilaya. Agenda zilikuwa ni kufanya tathmini juu ya ahadi zake kwa Wananchi zilizotolewa na Mbunge huyo. Katika Mkutano huo Hapakuwa na Lugha za Matusi na Mkutano ulimalizika majira ya saa 18:20 jioni na wananchi kutawanyika kwa amani na utulivu.
Ø  Wakulima na Wafugaji – hakuna.
Ø  Wakulima/Wananchi na Wawekezaji – Hakuna
Ø  Dini – Hakuna.
B: Idadi ya watendaji.
Ø  Jumla ya askari 1,458 waliingia kazini, doria na malindo mbalimbali.
Ø  Jumla ya watumishi raia waliopo ni 17.
Ø  Jumla ya  vikundi vya ulinzi jirani vilivyopo  Mkoa wa  Mbeya  262,  jumla ya  vikundi vilivyoshiriki  ni  101  na walinzi   394  walishiriki katika doria/malindo mbalimbali.
Ø  Jumla ya askari Mgambo waliopo Mkoa wa Mbeya ni 2,253.
Ø  Jumla ya Polisi wasaidizi waliopo ni 420.





C: Mafanikio yaliyopatikana.
§  Mafanikio yaliyopatikana kupitia doria,misako na operesheni ni kama ifuatavyo:-
v  Bhangi –
v  Dawa za kulevya {drugs} – Hakuna.
v  Pombe ya Moshi – Hakuna.
v  Silaha – Hakuna
v  Nyara za Serikali – Hakuna.

D: Ukamataji wa makosa ya Usalama Barabarani.

§  Jumla ya  makosa yaliyokamatwa –  262
§  Jumla ya  makosa yaliyolipa - 237
§  Jumla ya magari yaliyokaguliwa kwa siku – Hakuna.
§  Tozo lililopatikana kutokana na ukaguzi wa magari – Hakuna.
§  Kesi zilizopelekwa Mahakamani – Hakuna.
§  Jumla ya Tozo [Notification] Tshs 7,110,000/=.

E: Watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa mbalimbali.
  • Jumla ya watuhumiwa waliokamatwa ni 43.
  • Jumla ya wahalifu wazoefu{harbitual} Mkoa wa Mbeya   139.
  • Wahalifu wazoefu {Harbitual} – waliokamatwa – 05.
  • Jumla ya wahalifu waangaliwa {Supervisee} Mkoa wa Mbeya 86.
  • Wahalifu waangaliwa {Supervisee} – waliokamatwa – 03.
  • Jumla ya kesi zilizofikishwa Mahakamani – 65.
  • Kusomewa Mashitaka {fresh Cases} – 07.
  • Jumla ya kesi zilizosikilizwa {Hg}– 50.
  • Jumla ya kesi zilizotajwa {M}– 65.
  • Kusomewa maelezo ya awali {Phg} – 26.
  • Watuhumiwa waliofungwa {Convicted} – 04.
  • Watuhumiwa waliachiliwa huru {Acquited} - Nil.

F: HITIMISHO:
Kwa leo tarehe 26.08.2014 kumekuwa na idadi ya matukio “Hakuna” kama ifuatavyo:-
  • Mauaji – Hakuna.
  • Unyang’anyi wa Kutumia Silaha – Hakuna.
  • Ajali ya Gari Kusababisha Vifo – Hakuna.       

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...