Jumatatu, 11 Agosti 2014

NHC MBEYA YAMKABIDHI KANDORO MASHINE 40 ZA KUFYATULIA TOFALI KWA HALMASHAURI 10



Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amepokea msaada wa mashine 40 za kufyatulia tofali za kisasa, zenye thamani  ya Tsh.18,000,000,000/= kwa ajili ya vikundi vya vijana kutoka halmashauri 10 za mkoa huo.
 
‘’Shirika lenu linafanya vizuri sana, mnastahili pongezi,’’alisema.
 
Alisema msaada huo umeongeza chachu ya mahitaji ya nyumba bora kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira kwa vijana.
 

Meneja (NHC)mkoa wa Mbeya Antony Komba alisema mashine hizo ni kati ya mashine nyingi zilizotolewa na Shirika hilo kwa ajili ya kuwasaidia vijana kutokana na kuwepo kwa makazi duni ya walio wengi nchini.

Awali, Shirika hilo, liliziomba halmashauri kuunda vikundi kwa kila halmashauri iwe na vikundi  vinne  vyenye jumla ya watu kumi ambavyo vitachagua viongozi na kufungua akaunti ya kikundi na baadaye watapatiwa mafunzo.
 
Shirika linatarajia kutoa Tsh. 500, 000/= kwa kila kikundi ikiwa ni mtaji wa kuanzia shughuli hizo.
 
Halmashauri ni Chunya,Mbeya, Kyela, Rungwe, Ileje, Mbarali,Mbozi,Mbeya mjini,Momba na Busokelo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...