Jumanne, 15 Aprili 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 15.04.2014.




KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA AITWAE MSUKUMA PENGO [48] MKAZI WA MTAA WA MWAMBENE ALIFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA JIJINI MBEYA TAREHE 14.04.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.

MAREHEMU ALISHAMBULIWA  KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO, MAWE, MATOFALI NA MARUNGU TAREHE 13.04.2014 MAJIRA YA  SAA 20:00 USIKU  HUKO KATIKA MSIKITI WA SAE, KATA YA  ILOMBA, TARAFA YA  IYUNGA. INADAIWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI WA BAISKELI MOJA AINA YA BAMBUCHA YENYE THAMANI YA TSHS 150,000/= MALI YA IDDY OMARY [37] IMAMU WA MSIKITI WA SAE, MKAZI WA IGANZO.

AWALI MAREHEMU AKIWA MSIKITINI HAPO ALITOKA NDANI YA  MSIKITI NA KUIBA BAISKELI HIYO WAKATI IMAMU AKIWA NDANI NA  WANANCHI WALIMUONA KISHA KUMKAMATA NA KUMSHAMBULIA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE. AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUJENGA TABIA YA KUJITAFUTIA KIPATO KWA NJIA HALALI BADALA YA KUTAKA UTAJIRI WA HARAKA KWA NJIA ZA MKATO ZISIZO HALALI KWANI ZINA MADHARA KATIKA JAMII.


KATIKA TUKIO LA PILI:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. ABDULSALAM MOHAMED [19] NA 2. ABRUHAMAN HAYALEMASI [28] WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.

WATU HAO WALIKAMATWA TAREHE 14.04.2014 MAJIRA YA SAA 10:50 ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA NTENGANO, KATA YA IJOMBE, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI KUFUATIA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA WASAMALIA WEMA  KWA JESHI LA POLISI AMBALO LILIFANIKIWA KUWAKAMATA.TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA  UHAMIAJI ZINAFANYIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA  MSAIDIZI MWANDAMIZI  WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA  MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI.


Signed by:
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...