Kulia ni Mzee wa mila katika wilaya ya Mbarali, akimsalimu na kumshukuru KAMANDA wa UVCCM wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Ibrahimu Ismail(Mwakabwanga).
Kushoto ni Chifu, Salehe Merere, akipokea mifuko kumi ya Saruji kwa ajili ya shule ya Msingi, mifuko hiyo ya saruji ilitolewa na KAMANDA wa UVCCM wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Ibrahimu Ismail(Mwakabwanga).
Gari la wagonjwa lillotolewa na kampuni ya Usangu ambayo inamilkiwa na KAMANDA wa UVCCM wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Ibrahimu Ismail(Mwakabwanga).
Jokofu
APRIL 4,
mwaka huu. Limefanyika tukio la historia katika kata ya Utengule Usangu, wilaya
ya Mbarali mkoani Mbeya.
Hapa ni eneo
ilipo Ngome ya chifu Merere.
Kwa
waliosoma miaka ya nyuma kidogo, nchi yetu ilipokuwa ikithamini kwa vitendo
masuala ya kihistoria na ushujaa wa watemi wetu, wanalikumbuka jina la chifu
huyu wa kabila la Wasangu.
Siyo nia
yangu leo kueleza historia ya Merere, bali kuelezea suala la kihistoria
lililofanyika mita mia moja kutoka eneo la Ngome hiyo.
Kaimu katibu
Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mmapinduzi(UVCCM), Taifa, Mfaume Kizigo,
alifika eneo hilo na kusimikwa pia kuwa mmoja wa watemi wa kabila la wasangu.
Baadaye,
Kizigo, alimsimika kamanda wa Vijana wa UVCCM wa wilaya hiyo, Ibrahimu
Ismail(Mwakabwanga), ambaye pia alimsimika naibu wake Leonatus Mdindile.
Kizigo
anasema kuwa, kwa wanaokumbuka historia, ni kwamba zamani watu walikuwa wakitembea
uchi, lakini hakukuwa na kesi za ubakaji.
Lakini hii leo
kuna kesi za namna hiyo kutokana na kuporomoka kwa maadili kunakochagizwa na
kuwadharau wazee wakiwemo machifu.
Jamii
imeendelea kulalamikia suala zima la uharibifu wa mazingia na ukataji miti kwa
ujumla wake na kusahau kuwa, zamani jamii ilipokuwa ikiheshimu wazee ndipo
ilikuwa salama, kwasababu machifu walikuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa kukuza
mila na desturi na utunzaji wa mazingira.
Baada ya
kuapishwa, Ibrahimu Ismail, maarufu kwa jina la kibiashara(Mwakabwanga), ambaye
pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Usangu Logistics Ltd, anashukuru vikao vya
uteuzi vya vijana kwa madai kuwa yeye siyo mzigo.
Ukimwangalia
machoni, unatambua kuwa Mwakabwanga, anajua fika, majukumu yake kama kamanda wa
Vijana kwa mujibu wa miongozo ya kanuni za UVCCM kuwa ni kuwaunganisha vijana
na shughuli zao za kiuchumi.
Siku hiyo
hiyo, alianza kuihudumia jamii kwa kukikabidhi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gari
la wagonjwa na Jokofu la kuhifadhia maiti na kwamba haombei watu kufa bali
anataka hata watakaotangulia, wawe na mwisho mwema na wa heshima.
Gari na
Jokofu anasema vina thamani ya Milioni 35 na zaidi, huku akiweka wazi kuwa
ataendelea kuzungumza na marafiki zake kuikomboa jamii ya wananyika wa Mbarali
kwa kuwapelekea mahitaji wanayoomba bila kujali itikadi za siasa.
Katibu wa
CCM wilayani humo, Mr. Luambano, baada ya kukabidhiwa, naye akakabidhi
serikalini. Anamshukuru kamanda huyo na kumsihi azidi kuwasaidia wananchi kwa
ujumla.
Mkuu wa
wilaya hiyo, Gulam Kiffu, anasema msaada wa gari la wagonjwa na Jokofu ni
msaada mkubwa kwasababu kabla ya msaada huo walikuwa wakipeleka maiti kuhifadhi
Ilembula mkoani Njombe au katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya zaidi ya kilomita
80.
Katibu wa
UVCCM wilayani humo, Sure Mwasanguti na Mwenyekiti wake Amin Kimulungu, wanampa
moyo kamanda wao na kwamba wanajua fika kuwa utendaji kazi wake wa kuhudumia
jamii unaweza kuwa tatizo kwa baadhi ya wasaka madaraka. Hivyo asikate tamaa.
Vijana wanaruhusu
magugu na ngano vikue pamoja kisha jamii itaamua wakati wa mavuno wakati CCM
Taifa, sidhani kama ina maono kama jamii inavyohitaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni