Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Kamishna wa Maendeleo Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs(Watau kushoto) na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakikagua chanzo cha maji eneo la Swaya mjini Mbeya wakati wa uzinduzi wa mradi maji safi na mazingira.
LICHA ya kukabiliana na changamoto kadhaa za uendeshaji shughuli zake, MAMLAKA ya
maji safi na usafi wa Mazingira Jijini Mbeya (MBEYA-UWSA) imewahimiza wananchi
kuendelea kulipa ankara za maji kwa ajili ya kuiwezesha Mamlaka hiyo kuendelea
kudhibiti magonjwa ya milipuko kikiwemo Kipindupindu.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ambaye pia ni Injinia wa ufundi, Martin Kimambo,
amesema Mamlaka yake imewezesha na inajivunia kudhibiti
kipindupindu na kufikia hatua serikali kufunga kambi la ugonjwa huo eneo la
Isanga Jijini Mbeya.
Alisema
gharama kubwa zinatumika katika kununua dawa za kutibu maji na kulipia umeme.
‘’Tunatumia Tsh.
50 Mil, kwa mwezi kwa ajili ya kununua dawa ya kutibu maji na Tsh. 70 Mil, kwa
ajili ya kulipia umeme, hivyo wananchi ni wajibu wao kukumbuka kulipia gharama
za maji safi wanayoyapata ili kuiwezesha mamlaka kutimiza wajibu wetu’’ alisema
Kimambo.
Aliongeza
kuwa kwa sasa tangu mamlaka hiyo ianze kukazania suala la kutibu maji, ni miaka
13 tatizo la ugonjwa wa kipindupindu uliokuwa ukilipuka kila msimu wa mvua
Jijini hapa, kwa sasa ni historia.
‘’Wananchi wanaokatiwa huduma ya maji
wasipolipa wasilaumu, ni kwa ajili ya kutekeleza majukumu yetu kwa faida ya
wananchi wote’’ alisema Injinia Kimambo.
Afisa habari
wa Mamlaka hiyo, Neema Stanton, alisema wanajisikia fahali kuwahudumia wateja
wanaokumbuka wajibu wao wa kulipia huduma za maji kwa wakati jambo ambalo
linaisaidia mamlaka kutekeleza majukumu yake.
Amewasihi
wateja wapya wanaotaka kuunganishiwa maji kufika ndani ya ofisi za Mamlaka hiyo
kwa kile alichosema kuwa kuunganishiwa maji na mamlaka ni gharama za kawaida
bali ni ghali akikamatwa mteja aliyeunganishiwa huduma hiyo na mafundi vishoka.
Mamlaka hiyo
inaendelea na zoezi la kuwakatia huduma za maji wateja wanaodaiwa wakiwemo
wateja wa majumbani, hotel kisha taasisi za serikali ambazo zinadaiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni