KAMANDA POLISI MBEYA, MSANGI.
KIJANA Medi
Wailes, mkazi wa Kijiji cha Chalangwa wilaya ya Chunya mkoani hapa, amejikuta
akishinda na pingu kwa zaidi ya saa nane, baada ya polisi waliomfunga pingu
hizo kuwakimbia wananchi waliokuwa wakipinga kukamatwa kijana huyo kwa kosa la
kumpinga mwekezaji wa madini.
Tukio la
kumfunga pingu kijana huyo, lilianza majira ya saa 8;35 za usiku wa kuamkia
Machi 2, mwaka huu, baada ya askari polisi kufika kijijini hapo na kuwakamata
baadhi ya wananchi wanaompinga Mwekezaji, Joseph Mwazyele.
Mwazyele
anadaiwa kutaka kufungua mgodi katika kijijiji hicho, jambo ambalo baadhi ya
wananchi wanapinga ingawa baadhi wanahitaji uwekezaji huo ufanyike.
Baada ya
hali hiyo kutokea, wananchi walipiga mbiu, ambapo baada ya askari polisi kuona
hivyo walikimbia huku wakimwacha Wailesi akiwa na pingu mkononi na ndipo
wananchi wakafunga barabara na kusababisha kutopita magari yanayofanya safari
zake za Mbeya-Chunya mpaka majira ya saa Nne asubuhi leo.
Kamati ya
ulinzi na usalama wilaya ya Chunya, iliwasili eneo la tukio kwa lengo la
kuwatuliza wananchi majira ya saa 1;50 asubuhi. Ambapo wananchi walikataa
kugungua barabara wakimhitaji Mkuu wa mkoa wa Mbeya na uongozi wa madini wilaya
na mkoa na funguo za pingu.
Wakati
mazungumzo yakiendelea, ziliingia gari nne za askari wa kutuliza ghasia(FFU), na
kuanza kufungua geti la barabra hiyo huku wananchi wakitaka mwenzao afunguliwe
pingu.
Gari hizo
ambazo zilikuwa zimejaa askari, zilikuwa na namba za usajili PT 2079, PT 1931,
PT 0943 na PT 1925 na hatimaye zikaondoka eneo hilo.
Mkuu wa
wilaya ya Chunya, Deodutus Kinawiro alianza kuzungumza na wananchi wa kijiji
hicho katika uwanja wa shule ya Msingi Chalangwa.
Kinawiro alisisema
eneo hilo linalolalamikiwa linasitishwa uwekezaji na shughuli zingine ambapo
amewataka wanaohitaji kuwekeza, waanzie ngazi ya kijiji na kuwasihi wananchi
kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Mkuu huyo
alipata wakati mgumu alipomtaka aliyefungwa pingu kujisalimisha polisi jambo
ambalo zilitokea kelele kutoka kwa baadhi ya wananchi wakipinga maamuzi hayo
huku wakiwa wamemficha kijana huyo.
Baada ya
hapo, Mkuu wa wilaya aliamuru kijana huyo kujitokeza eneo la mkutano ili
afunguliwe pingu mbele ya mkutano. Wananchi wenzake walimleta kijana huyo na
kufunguliwa pingu kisha mkutano ukafungwa na hali ya usalama ikarejea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni