WILAYA YA KYELA – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 12.01.2014 MAJIRA YA SAA 05:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LEMA NA KATA YA NGANA, TARAFA YA NTEMBELA, WILAYA YA KYELA,
MKOA WA MBEYA. BICCO S/O
MWAKIBIBI, MIAKA 28, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA LEMA ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA
MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA
SILAHA ZA JADI MAWE NA FIMBO. CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU
NA MWENZAKE KUVUNJA KIBANDA CHA BIASHARA NA KUIBA, MWENZAKE ALIKIMBIA BAADA YA
TUKIO HILO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA
UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKATA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
WILAYA YA MOMBA –
MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 12.01.2014 MAJIRA YA SAA 09:30HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA
SERIKALI WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. ADAMU
S/O SILUMBE, MIAKA 27, MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KAPELE
ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU
ALICHOMWA KISU MGONGONI TAREHE
10.01.2014 MAJIRA YA SAA 21:00HRS NA MDOGO WAKE AITWAE BONNY
S/O SILUMBE KATIKA KIJIJI CHA KAPELE,
KATA YA KAPELE, TARAFA YA NDALAMBO. CHANZO NI KULIPIZA KISASI
BAADA YA MAREHEMU KUMTANGAZA MTUHUMIWA HAPO KIJIJINI KUWA ALIMTOROSHA MKE WA
MTU. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA
UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUSHUTUMIANA
NA BADALA YAKE WATATUE MIGOGORO YAO KWA NJIA YA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO
ILI KUFIKIA MUAFAKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE MARA MOJA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni