Dr. Mary Mwanjelwa, akimkabidhi Imamu Mkuu wa msikiti huo, Iliyasa Mchalikwao, mifuko 60 yenye saruji ndani ya gari.
Sasa kumekucha......sasa kumekucha...
*****************************************************************************************************8
WAISLAM wa
msikiti wa Almasjid Tawfiq, Soweto
Jijini Mbeya, wamepongezwa kwa ubunifu wa maendeleo na kuwa na nia ya dhati ya
kuleta amani na mshikamano nchini.
Pogezi hizo zimetolewa Juzi na Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa(CCM), alipokuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchagia ujenzi wa msikiti wa kisasa unaotarajiwa kujengwa eneo hilo la Soweto.
Dr.
Mwanjelwa alisema, Misikiti na makanisa ni maeneo ya kiimani pia ni maeneo ya
kutengeneza maadili na kuiweka jamii kuwa salama.
‘’Kiongozi
mzuri ni yule mwenye maadili, asiyejali itikadi za kiimani, bali kuhudumia
jamii, mimi ni kiongozi wa wote sibagui kabila, dini wala tabaka lolote, moyo
wangu ni wa kusaidia jamii’’ alisema Dr. Mwanjelwa.
Alisema kuna
baadhi ya wananchi na makundi yenye nia nzuri ya kimaendeleo, wanawachukia
baadhi ya viongozi hata bila kuwashirikisha, jambo ambalo alisema jamii
inapaswa kuondokana nalo na aliomba yeye ashirikishwe kwa kila jambo la kimaendeleo
kwasababu yeye ni mwanamaendeleo na si ‘’longolongo’’.
Katika
harambee hiyo, Mbunge huyo alitoa mifuko 60 ya saruji yenye thamani ya Shilingi
Milioni moja na Laki Nne, ambayo aliikabidhi papo hapo ikiwa kwenye gari aina
ya Canter T 441 BRL, na kuahidi
kuwatafutia viongozi wengine wa kuchangia ujenzi wa msikiti huo wa kisasa.
Imamu mkuu
wa msikiti huo, Ilyasa Mchalikwao, alimshukuru Mbunge huyo kwa ajili ya moyo
wake wa kukubali kuchangia msikiti huo bila kujali itikadi ya kidini na kwamba
huo ndiyo uongozi.
Awali
akisoma risala ya Msikiti, Katibu wa
Maendeleo ya Msikiti huo wa Almasjid Tawfiq, Juma Ramadhani, alisema
wanatarajia kujenga msikiti wa kisasa wenye ghorofa tatu ambao utajengwa kwa
awamu nne na kugharimu zaidi ya Shilingi Milioni 700.
Alisema
lengo la ujenzi wa msikiti huo wa kisasa ni maendeleo na kwamba msikiti huo
ukikamilika, utakuwa ni wa mfano katika mkoa wa Mbeya na Dr. Mwanjelwa tayari
ameingizwa kwenye historia ya msikiti huo kwa kuwa ni kiongozi wa kwanza
kuchangia.
‘’Tayari
tumekusanya Shilingi Milioni 34, na tumeshauriwa kuacha kusambaza majengo
ardhini, tuna imani nawe kwasababu unaweza na ni makini sana tena sana na
tunakutegemea kututafutia wafadhili kwasababu unao marafiki ndani na nje ya
nchi’’ alisema Juma Ramadhani.
Alisema
historia na maisha ya Mwanadamu vinaenda sawa, hivyo wanamtakia kheri katika
kazi zake za kisiasa na kutumikia wananchi na kwamba mbali na yeye pia Mbunge
wa Sumbawanga Mjini, Aesh Hilary(CCM), alituma Sh. 1.5 Milioni kwa ajili ya
kumwongezea nguvu ya harambee Dr, Mwanjelwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni