Ijumaa, 27 Desemba 2013

VIJANA WAZALENDO MBALIZI, WAENDELEA KUJITOLEA KUFANYA USAFI KATIKA MJI WA MBALIZI MBEYA

 Vijana wazalendo Mbalizi chini ya umoja wao wa (UVIWAMBA), wakiwa wanafanya kazi za usafi katika mji wa Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya. Vijana hao wanajitolea kufanya kazi za usafi ili kuondoa dhana ya vijana kutaka kulipwa kwa kila jambo au kufanyiwa na serikali.
 Hapa ni Ghuba la eneo la Mashine ya Bariki, lililopo katika barabara ya vumbi kutoka kituo cha polisi Mbalizi kwenda Tarafani kwenye stendi ya wilaya ya Mbeya. Vijana hao waliamua kutoa takataka zilizokuwa zimelizidi dampo hilo na kuziba nusu barabara, hivyo waliingiza ndani ya ghuba takataka hizo baada ya magari ya Halmashauri hiyo kuonekana kuwa hayakuwa mazima nyakati hizi za sikikuu ya X-mass 2013.
 Vijana wakiwajibika na kutimiza wajibu wao kwa taifa, kila aliyeguswa na uzalendo huo alihusika katika kufanya kazi hiyo ya usafi ambapo kila siku ya Jumamosi ya kila Juma, vijana hao wanafanya kazi hiyo ya usafi katika eneo hilo la Mbalizi na wilayani humo.
 Vijana wa kike na kiume, wote wanawajibika, wakiwemo watu wazima...
Ghuba hilo baada ya kusafishwa hivi ndivyo linavyoonekana ingawa kuna baadhi ya wananchi siyo wastaarabu, wanaendelea kutupa taka nje ya ghuba.
 
Chanzo; kalulunga media blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...