Alhamisi, 10 Desemba 2015

BARAZA LA MAWAZIRI LATANGAZWA RASMI LEO NCHINI TANZANIA


RAIS wa Tanzania, Dkt. John Pombe MAGUFULI, ametangaza baadhi ya mawaziri wa serikali yake hii leo.

 

Amesema baraza lake litakuwa na mawaziri 19, ambapo baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama. 

   
Kuhusu semina elekezi kwa mawaziri hao, ameeleza kwamba, zilitengwa bilioni 2, lakini fedha hizo zitapelekwa ama kwenye madawati ama kuboresha (elimu bure).
 
 
"Wizara ni 18 lakini Mawaziri ni 19 kwa sababu wizara ya Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma naiunganisha na Utawala bora hivyo itakua na mawaziri wawili. Wizara ni kama ifuatavyo";




 
1. Ofisi ya Rais, Tamesemi utumishi na utawala bora, Mawaziri; Simbachawene na Kairuki, Naibu waziri Jaffo
 
2. Mazingira: January Makamba, naibu Makamba
 
3. Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma
 
4. Ulemavu: Waziri ni Anthonu Mavunde
 
5. Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi : Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba na Naibu wake ni William Nash
 
6. Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Ngonyani.
 
7. Fedha na mipango: Waziri bado, naibu Kijachi
 
8. Nishati na madini: Waziri ni Muhongo, Naibu bado
 
9. Katiba na sheria: Waziri Mwakyembe
 
10. Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Augustino Mahiga nimemteua mbunge na waziri, Naibu Dr Suzan
 
11. Ulinzi na kujenga taifa: Waaziri Dr. Hussein Mwinyi naibu bado
 
12. Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula
 
13. Utalii: Waziri bado
 
14. Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage
 
15. Sayansi na ufundi: Waziri bado, Naibu ni Stella Manyanya
 
16. Afya na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Kingwangala
 
17. Wizara yaHabari l,Utamaduni na Wasanii : Waziri ni Nape Nnauye,
 
18. Wizara ya maji na umwagiliaji: Waziri Makame Mbarawa, Naibu ni Kamwene

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...