Jumatatu, 1 Juni 2015

Serikali yatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya afya


SERIKALI imewaomba watafiti wa masuala ya afya hapa nchini kuhakikisha kwamba wanaibua hoja mpya zitakazosaidia kuleta mabadiliko kwenye sera za kitaifa zinazohusu sekta hiyo muhimu. Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mbando mara tu baada ya kufunga mkutano mkuu watatu wa sayansi ya afya uliondaliwa na chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili (MUHAS).




“Kwa sasa taifa linashuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaosumbuliwa na magonjwa yasiyoyakuwa ya mbukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu na kisukari. Kwa bahati mbaya sana vituo vyetu vingi vya afya havijaandaliwa vizuri kukabiliana na magonjwa haya kwasababu sera zetu wakati zinaandaliwa hazikujika zaidi kwenye magonjwa yasiyoyakuwa ya kuambukiza na ndio maana tunahitaji mabadiliko kwenye hili,’’ alisema Dr. Mbando.




Dr. Mbando alizataja sababu kubwa zinazochangia ongezeko la magonjwa hayo kuwa ni pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi, aina ya vyakula vinavyotumiwa na watanzania hususani wale wanaoishi maeneo ya mijini, kutokufanya mazoezi pamoja na uvutaji wa sigara. Aidha aliiongeza kuwa kwa sasa serikali ipo kwenye mpango wa kuandaa mkakati  wanne wa huduma za afya hapa nchini (health care financing strategy) utakao muwezesha kila mtanzania kuwa na bima ya afya.




“Kwa sasa ni asilimia 20 tu ya watanzania ndio wanamiliki bima za afya zinazotolewa na shirika la bima ya afya la taifa na mashirika binafsi na hivyo kufanya asilimia 80 ya watanzania kuishi bila kuwa na uhakika wa masuala ya tiba….hili tumelianza tayari,’’ alibainisha.




Kuhusu mlipuko wa ugonjwa wakipundupindu kwenye mikoa ya kagera na kigoma uliosababishwa na kuingia kwa wakimbizi kutoka Burundi, Dr. Mbando alisema kwa sasa serikali kwa kushirikiana na Wananchi, wadau wa maendeleo na asasi zisizo za kiraia wanapambana kuhakikisha tatizo hilo linakwisha.




Akizungumza kwenye mkutano huo Makamu mkuu wa MUHAS, Prof. Ephata Kaaya alisema kwa sasa taifa linahitaji zaidi tafiti za kiafya hususani kwenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza na ndio sababu mkutano huo ulijikita zaidi kujadili tatizo hilo.




“Kama wataalamu wa masuala ya afya tunaona kuna haja kubwa tukiwekeza katika tafiti zinazolenga kuibua changamoto na suluhisho kwenye magonjwa haya,’’ alisema. Mkutano huo wa siku mbili ulihudhuriwa na washiriki zaidi ya 300 wakiwemo madaktari, viongozi na wanafunzi wa udaktari kutoka MUHAS na vyuo vingine vya afya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...