Meneja
wa NHIF mkoani Mbeya Dk.Mohamed Kilolile akiwasilisha moja ya mada kwa
watoa huduma wa KFW wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa
Mtenda jijini Mbeya
MRADI wa Afya ya Mama na Mtoto(KfW) unaoendeshwa na Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya(NHIF) kwa ufadhili wa benki ya maendeleo ya watu wa Ujerumani
umewezesha wanaume kushiriki shughuli za uzazi kwa kuwasindikiza wake zao
kliniki wanapokuwa wajawazito.
Hayo yamebainishwa na watoa huduma wa KFW walipohudhuria
semina ya siku mbili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo iliyofanyika jijini Mbeya.
Watoa huduma hao wanasema tofauti na awali hivi sasa kumekuwa na
mwamko mkubwa wa wanaume kuongozana na wake zao kwenda kliniki wanapokuwa wajawazito na kupata elimu kwa
pamoja juu ya njia sahihi zinazotakiwa katika kumhudumia mama mjamzito.
“Kwa sasa wanaume wanashiriki kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na
awali. Wanapenda kuongozana na wake zao ili wapate elimu kwa pamoja.
Tunaamini kupitia elimu tunayoitoa upitia KfW wamebadilika na wametambua kuwa wanawajibu pia wa kuhudhuria kliniki ili kupata tarifa sahihi za ujauzito wa wake zao” anasema mmoja wa watoa huduma hao Elizabeth Mwamlima kutoka zahanati ya kijiji cha Utulo wilayani Mbarali.
Tunaamini kupitia elimu tunayoitoa upitia KfW wamebadilika na wametambua kuwa wanawajibu pia wa kuhudhuria kliniki ili kupata tarifa sahihi za ujauzito wa wake zao” anasema mmoja wa watoa huduma hao Elizabeth Mwamlima kutoka zahanati ya kijiji cha Utulo wilayani Mbarali.
Mwamlima amesema kwa ushiriki huo wa wanaume hivi sasa familia
zimekuwa zikijipanga mapema wakati wa ujauzito ili kuhakikisha mwanamke husika
anapata huduma stahiki ikiwemo kupelekwa katika hospitali waliyoshauriwa na
wataalamu mara wakati wa kujifungua unapowadia.
Amesema hali hiyo inawaepusha wanawake wajawazito kuepuka hatari
ambazo zilikuwa zikiwakumba awali na kuhatarisha maisha yao na watoto wachanga
wakati wa kujifungua na baada.
Kwa upande wake katibu wa Afya mkoa wa Mbeya Juliana Mawala amesema
mradi wa KfW ambao kwa hapa nchini unaendeshwa katika mikoa miwili ya Mbeya na
Tanga umeleta manufaa makubwa katika utatuzi wa changamoto za Afya za
wajawazito na watoto wachanga.
Mawala amesema ni imani ya wadau wa afya kuwa ushiriki wa jamii
katika utatuzi wa changamoto zinazowakabili wajawazito na watoto utakuwa
endelevu hata baada ya ukomo wa KfW kwakuwa tayari wananchi wamepata uelewa juu
ya umuhimu wa kuchangia na kuwekeza katika masuala ya afya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni