Ijumaa, 19 Septemba 2014

REAL INSURANCE YATOA MSAADA WA VIFAA VYA ELIMU ST. AUGUSTINE UNIVERSITY



 Kutoka kushoto ni Meneja wa kampuni ya Real Insurance, kanda ya nyanda za juu kusini, Smart Mwaheleja, Meneja wa Masoko na Biashara kutoka REAL Insurance, Amani Boma akimkabidhi kiti na meza, Mkurugenzi wa Maendeleo ya ST. Augustine tawi la Mbeya, Padri Innocent Sanga, leo chuoni hapo Jijini Mbeya.


 Meneja wa Masoko na Biashara kutoka REAL Insurance, Amani Boma (kushoto) akimkabidhi kiti na meza, Mkurugenzi wa Maendeleo ya ST. Augustine tawi la Mbeya, Padri Innocent Sanga, leo chuoni hapo Jijini Mbeya.

 Baadhi ya wasomi wa chuo kikuu cha St. Augustine tawi la Mbeya, wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa kampuni ya Real insurance na Mkurugenzi wa Maendeleo wa chuo hicho, wakati wa hafla fupi ya kampuni hiyo kukabidhi viti na meza za kusomea wanafunzi. Hafla hiyo imefanyika leo chuoni hapo Jijini Mbeya.

Kutoka kushoto ni Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Rayson Mwangwala na afisa mahusiano wa chuo hicho, Emmanuel Mwalupindi, waliishukuru kampuni hiyo na kwamba msaada huo wameupokea kwa muda muafaka kutokana na mahitaji ya chuo na hivi karibuni chuo kinafungua kikiwa na wanafunzi wengi.


Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Rayson Mwangwala na afisa mahusiano wa chuo hicho, Emmanuel Mwalupindi, wakibadilishana mawazo na uongozi wa Real Insurance, baada ya kukabidhiwa viti na meza za kusomea wanafunzi.

. Meneja wa Masoko na Biashara kutoka REAL Insurance, Amani Boma,(kushoto), akipewa mkono wa shukrani na Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha St. Augustine, tawi la Mbeya, Rayson Mwangwala, baada ya kampuni ya Real Insurance, kutoa msaada wa viti na meza za kusomea wanafunzi wa chuo hicho.
 Moja ya kiti na meza, ambavyo kampuni ya Real Insurance, imetoka katika chuo cha St. Augustine, tawi la Mbeya leo.

 Picha ya pamoja kati ya viongozi wa chuo kikuu cha St. Augustine tawi la Mbeya, viongozi wa wanafunzi na viongozi wa kampuni ya Real Insurance.



Kampuni ya Bima ya REAL Insurance imeendelea kuunga mkono juhudi za wadau wa Elimu katika kukuza sekta ya elimu nchini kwa kutoa msaada wa viti na meza za wanafunzi kwa Chuo Kikuu cha St.Augustine tawi la Mbeya.

Kampuni hiyo imetoa meza 6 na viti 12 maalum kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vyenye thamani isiyopungua shilingi za kitanzania 2.5Mil. Meneja wa Masoko na Biashara kutoka REAL Insurance, Amani Boma, alibainisha kwamba kwa kutambua mchango wa sekta ya elimu ya juu nchini na umuhimu wa wanafunzi kujisomea katika mazingira mazuri na salama, kampuni yake inahamasika kuchangia maendeleo ya elimu nchini ili kuunga mkono juhudi za serikali na wadau wa elimu kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora wakati wote.

“REAL Insurance inatambua kuwa hakuna elimu iliyo bora bila nyenzo imara na nzuri, hivyo kwa kutoa motisha ya vifaa kwa ajili ya wanafunzi tunaamini kwamba tutaongeza ari na moyo wa kujituma kwa wanafunzi hawa ili kupata matokeo mazuri ya chuo hiki,” alisema Amani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya chuo hicho, Padri Innocent Sanga aliyepokea msaada huo kwa niaba ya  Mkuu wa Chuo, alisema anaishukuru REAL Insurance kwa kutoa mchango huo kwenye chuo chake huku akisema REAL Insurance ni kati ya makampuni machache yanayo unga mkono sekta ya elimu nchini.

“Msaada huu utatumika na wanafunzi wengi sana sababu ya ubora wa viti na meza hizi, tuna hakika viti na meza hizi zitaendelea kutumika kwa miaka mingi ijayo na wanafunzi mbalimbali watafaidika navyo wakitumia katika kujisomea.” Alisema Padri Innocent.

Meneja wa kampuni hiyo kanda ya nyanda za juu kusini, Smart Mwaheleja, alisema kampuni hiyo zamani ilijulikana kwa jina la Royal Insurance , ilianzishwa mwaka 1998 chini ya Sheria ya Bima ya mwaka 1996.

Alisema lengo kuu la kampuni hiyo ni kuwa kampuni bora ya bima barani Afrika, kwa kutoa huduma bunifu  ili kuendeleza  mchango wa Bima katika pato la taifa.

“Makao makuu ya kampuni ya REAL Insurance yapo Dar Es Salaam kwenye Jengo la PPF Tower. Kampuni hii ina matawi maeneo ya Mlimani City na Motor Inspection Center iliyoko Moroco na Ursino Road Dar Es Slaam. Pia ina matawi mengine katika mikoa ya Arusha mkabala na benki ya NBC, Mwanza kwenye jengo la PPF Tower,Dodoma jengo la Lawate Mji Mpya na Mbeya  jengo la Centruy Plaza- Mwanjelwa. Ofisi za Dodoma zilizinduliwa mwezi wa Aprili mwaka huu.Pia huduma za REAL Insurance zinapatikana kwa mawaala wao wanopatikana Tanzania nzima zikiwamo ofisi za Posta Tanzania’’alisema Mwaheleja.

Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Rayson Mwangwala na afisa mahusiano wa chuo hicho, Emmanuel Mwalupindi, waliishukuru kampuni hiyo na kwamba msaada huo wameupokea kwa muda muafaka kutokana na mahitaji ya chuo na hivi karibuni chuo kinafungua kikiwa na wanafunzi wengi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...