Ijumaa, 4 Aprili 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 04.04.2014.




KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MPANDA BAISKELI MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MAIKO PETER (45) MKAZI WA KAFUNDO AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.361 CRS AINA YA SANLG ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA WAKILI MWASUNGUTI.

AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 02.04.2014 MAJIRA YA SAA 19:15 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAFUNDO, KATA YA IPINDA, TARAFA YA NTEBELA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA KUITELEKEZA PIKIPIKI MARA BAADA YA AJALI. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJAI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

KATIKA TUKIO LA PILI:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMOS CHARLES (32) MFUGAJI, MKAZI WA MAMBA F KWA TUHUMA ZA WIZI WA NG’OMBE WAPATAO 24 MALI YA MFUGAJI AITWAYE BUNDALA MSOMA (64) MKAZI WA KIJIJI CHA MAMBA F.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.03.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. THAMANI HALISI YA NG’OMBE HAO NI TSHS. 7,200,000/=. CHANZO NI KULIPIZA KISASI BAADA YA MTUHUMIWA KUMDHAMINI MAHAKAMANI MTOTO WA MLALAMIKAJI LEA MASASI ALIYEKUWA ANAKABILIWA NA KESI YA KUFANYA FUJO KISHA KUTOROKA. 

MTUHUMIWA KABLA YA KUTEKELEZA UHALIFU HUO ALIVUNJA ZIZI LA NG’OMBE NA KISHA KUIBA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA AKIWA NA NG’OMBE 23 NYUMBANI KWAKE. MARA UCHUNGUZI UTAKAPO KAMILI ATAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHANA NA TAMAA YA MALI NA BADALA YAKE WATUMIE NJIA HALALI KUJIPATIA KIPATO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTUMIA NJIA ZA AMANI KWA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUFIKIA MUAFAKA WA MIGOGORO YAO.





KATIKA TUKIO LA TATU:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WATATU WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI. WAHAMIAJI HAO HARAMU NI 1. ABRI KABAI (26) 2. KISHETI KIBANO (21) NA 3. CHIKAMLA GEORGE (24) WOTE WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA.

WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.04.2014 MAJIRA YA SAA 05:30 ALFAJIRI KATIKA ENEO LA STENDI KUU, KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAFANYIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA PALE WANAPOWAONA WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI WAFANYIWE UCHUNGUZI/UPELELEZI. AIDHA ANATOA WITO KWA WAGENI/WAHAMIAJI KUFUATA TARATIBU/SHERIA ZA UHAMIAJI IKIWA NI PAMOJA NA KUWA NA KIBALI KINACHOWARUHUSU KUINGIA NCHINI ILI KUEPUKA USUMBUFU.


KATIKA MISAKO ILIYOFANYIKA:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE 1. ALOYCE ALFRED (22) 2. ABEL MTAWA (19) 3. AWAMI HARUNA (23) NA 4. KENETH KIZITO (30) WOTE WAKAZI WA MBALIZI WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TATU [03].

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.04.2014 MAJIRA YA SAA 11:30 ASUBUHI KATIKA ENEO LA MBALIZI, KATA YA UTENGULE –USONGWE, TARAFA YA BONDE LA SONGWE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA FRANK MWAKIKAO (26) MKAZI WA ILOLO AKIWA NA BHANGI KETE 10 SAWA NA UZITO WA GRAM 50.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.04.2014 MAJIRA YA SAA 11:55 ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA MAKUNGULU, KATA YA MANGA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] NA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...