|
ASKARI
wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba
WP 5367 wa Ilala Jijini Dar es Salaam amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa
mtoto |
|
Baba Mzazi wa mtoto aliyeibiwa Salehe Issah Mwangosi(31) ndiye alieshirikiana na polisi huyo kumwiba mtoto |
|
Mboka Mwakikagile(20) mama mzazi wa mtoto aliyeibwa
|
ASKARI wa Jeshi la Polisi aliyefahamika
kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 wa Ilala Jijini Dar es Salaam
amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mtoto jinsi ya kiume aliyefahamika kwa jina la
Goodluck Salehe(siku 7) aliyeibwa April 6 mwaka huu huko Kasumulu Kata ya Itope
Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.
Mtoto alizaliwa Machi 30 na alipoibiwa
alikuwa na umri wa siku sita ambapo mtuhumiwa alishirikiana na Baba Mzazi
aliyefahamika kwa jina la Salehe Issah Mwangosi(31) mkazi wa Matankini Kyela
aliyemtambulisha kwa mama mzazi aliyefahamika kwa jina la Mboka Mwakikagile(20)
kuwa Prisca ni shangazi yake Salehe hivyo anakuja kumwona mtoto aliyezaliwa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed
Msangi amethibitisha kukamatwa kwa Askari huyo ambapo amesema kuwa ikithibitika
kutenda kosa hilo atafikishwa mahakama ya kijeshi na baada ya taratibu hizo
kukamilika atafikishwa Mahakamani ili kujibu tuhuma zinazo mkabili.
Mtuhumiwa amekamatwa April 17 mwaka huu
huko eneo la Meta Jijini Mbeya majira ya saa nne asubuhi akiwa na mtoto huyo
mkononi ambapo alitiwa nguvuni na kufikishwa makao makuu ya Polisi Mkoa Forest
ya Zamani kwa mahojiano zaidi.
Msangi amesema kuwa Salehe na Prisca
hawana mahusiano ya Damu ila wana mahusiano ya kibiashara ambapo wanaendelea
kufanya uchunguzi wa tukio hilo na upelelezi ukikamilika watafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabili.
MTOTO ALIYEIBWA AKABIDHIWA KWA WAZAZI
|
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi akimkabidhi kwa mama yake mzazi mtoto Goodluck mara baada ya kupatikana |
|
Akipokea
Mtoto wake Mama mzazi Mboka Mwakikagile(20) amelishukuru Jeshi la
polisi na wananchi wema kwa kufanikisha kupatikana kwa mtoto wake
Goodluck Salehe aliyeibwa na Askari wa Jeshi la Polisi WP 5367 Prisca
Kilwai April 6, mwaka huu huko Kasumulu wilayani Kyela.
|
|
Mtoto Goodluck Salehe |
|
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi,akizungumza baada ya kukabidhi
mtoto huyo aliwasihi wazazi kuwa makini na utunzaji wa watoto ili
kuepuka vitendo kama hivyo kujirudia. |
|
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi akizungumza na shangazi wa mtoto
aliyeibiwa pembeni ni baadhi ya waandishi wa habari walioshuhudia
makabidhiano hayo
BAADA ya Jeshi la Polisi mkoani Mbeya
kumtia nguvuni Askari wake anayetuhumiwa kuiba mtoto wilayani Kyela,Mtoto
huyo akabidhiwa kwa wazazi wake huku wakiendelea na uchunguzi zaidi.
Makabidhiano hayo yamefanyika
katika Hospitali ya Wazazi Meta alikokuwa akipatiwa matibabu mtoto
huyo katika chumba cha Joto na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi.
Akipokea Mtoto wake Mama mzazi Mboka
Mwakikagile(20) amelishukuru Jeshi la polisi na wananchi wema kwa kufanikisha kupatikana
kwa mtoto wake Goodluck Salehe aliyeibwa na Askari wa Jeshi la Polisi WP
5367 Prisca Kilwai April 6, mwaka huu huko Kasumulu wilayani Kyela.
Aidha mwanamke huyo amemshukuru zaidi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi pamoja na Askari wengine
waliofanikisha mtoto wake kupatikana akiwa hai.
Baadhi ya ndugu waliofurika katika
Hospitali ya Meta kushuhudia makabidhiano hayo wamesema hawaamini kile
kilichotokea baada ya kuwa katika hofu takribani siku kumi na moja baada ya
kuibwa katika zahanati ya Njisi iliyopo Kasumulu Kyela.
Aidha ndugu hao wamelipongeza Jeshi la
Polisi kwa kufanikisha kupatikana mtoto na wasamaria wote walioshirikiana nao
katika maombi hata kufanikisha upatikanaji wa mtoto huyo akiwa salama salimini.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mbeya, Ahmed Msangi,akizungumza baada ya kukabidhi mtoto huyo aliwasihi
wazazi kuwa makini na utunzaji wa watoto ili kuepuka vitendo kama hivyo
kujirudia.
Ameongeza kuwa Jeshi la polisi bado
linafanya upelelezi na kukusanya ushahidi zaidi ili waweze kuwafikisha
mahakamani watumiwa kujibu mashtaka wanayokabiliana nayo.
Amesema Mtoto huyo alipatikana Aprili
17, mwaka huu akiwa na Askari huyo majira ya saa nne asubuhi na kuongeza
kuwa mpaka sasa sababu za kuiba mtoto huyo hazijafahamika na atafikishwa
mahakamani wakati wowote baada ya kuhukumiwa kijeshi.
Na Mbeya yetu
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni