Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa (N i kama anamuonya kitu) Mbunge wa Jmbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(SUGU).
..........................................................................................................
MBUNGE wa Jimbo
la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi(sugu), amesema kuwa chama chake cha Demokrasia
na Maendeleo(Chadema), kinapata taarifa za serikali kutoka kwa baadhi ya maafisa
usalama wa taifa.
Hayo
aliyasema Januari 25, mwaka huu, katika mkutano wa hadhara wa chama hicho,
uliofanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya.
Alilazimika kutoa
siri hiyo alipokuwa akizungumza kuwa amepata taarifa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),
kupeleka vijana 300 kambini katika shule ya sekondari Chimala wilayani Mbarali
mkoani hapa, kwa ajili ya mafunzo ya kuvuruga mikutano ya Chadema.
‘’Chama cha
magamba kimepasuka na ndiyo maana tunapata siri zote, na popote palipo na
maafisa usalama zaidi ya watatu mmoja wao ni wa Chadema na walipo maafisa
watatu au wanne wa Polisi, wawili ni wetu’’ alisema Mbilinyi huku akishangiliwa
na wafuasi wake.
Kwa upande
wake, Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dr,Wilbroad Slaa, alisema kutokana na
taarifa hiyo anaagiza kukutana na vijana wake wa kikosi cha Red Briged kwa
ajili ya kukabiliana na vijana hao wa CCM.
Mbali na
hilo, alisema wamepata taarifa kuwa serikali inataka kutumia jopo la waganga wa
kienyeji kuwashughulikia wapinzani lakini yeye hawatamuweza kwasababu yeye pia
ni Mganga wa jadi na kwao Karatu wanamfahamu alipokuwa Fratee katika kanisa Katoliki.
Aidha,
aliweka wazi kuwa pamoja na mambo mengine, hakupendezwa na suala la kuona
jeneza ambalo lilitengenezwa na chama hicho wilaya ya Mbeya Mjini na kuandika
buriani Zitto Kabwe, kwasababu ishara hiyo siyo nzuri kwa mtu aliye hai.
Kutokana na
tamko la viongozi hao, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM), Mkoa wa
Mbeya, ulilazimika kuitisha waandishi wa habari na kukanusha jambo hilo.
Akizungumza
na wanahabari ofisini kwake, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna,
alisema kuwa chama hicho kimepeleka vijana wasiozidi 280 katika kambi lenye
lengo la mafunzo ya haraiki kwa ajili ya sherehe za miaka 37 ya CCM zitakazofanyika
Jijini Mbeya kitaifa.
Hata hivyo,
baadhi ya waandishi wa habari mkoani Mbeya, walitembelea kambi hilo baada ya
mkutano wa Chadema uliofanyika karibu na shule ya Chimala kuisha na kukuta
vijana hao wakifanya mazoezi ya kuumba maumbo yanayoashiria sherehe hizo
sambamba na kuimba nyimbo za chama chao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni