HOSPITALI
ya Makandana wilayani Rungwe ni miongoni mwa majengio laliyoathiriwa na
kimbunga kikubwa kilichotokea juzi katika mji mdogo wa Tukuyu na
kusababisha hasara ya kuharibika kwa mali.
Kimbunga hicho cha upepo mkali kilichoambatana na mvua kilitokea juzi
majira ya saa sita mchana na kudumu kwa muda wa dakika kumi huku
kikiacha hasara ya kuezua na kubomoa majengo mbalimbali pamoja na
kuangusha miti.
Akizungumza na Lyamba Lya Mfipa ofisini kwake,mganga mkuu wa gospitali
ya Makandana Stanfod Mwakatage alilitaja jengo la wagonjwa wa nje
kuezuliwa paa na kusababisha maji ya mvua kulowanisha vifaa kwenye
chumba cha wagonjwa mahututi.
Dk.Mwakatage alisema katika vifaa vilivyolowa maji ni pamoja na mashine
mbalimbali zenye gharama kubwa ambazo haijafahamika iwapo zimeharibika
au la kwani ilikuwa vigumu kuziwasha kwa hofu ya kuziharibu zaidi iwapo
maji yaliingia kwa ndani.
“Ni vigumu kujua iwapo vimeharibika kwani tunaogopa kuviunganisha katika
umeme vinaweza kuharibika iwapo maji yaliingia kwa ndani.
Tunasubiri
upite muda wa kutosha ndipo tuanze kujaribu na hapo tutaweza kujua iwapo
mashine hizi zimeharibika”
“Ni mashine za mamilioni kwakweli itakuwa hasara kubwa iwapo zitakuwa
zimeharibika kwa kuingiza maji.
Lakini uhakika tutaupata tukizijaribu”
Alisemaa pia majui yaliyoingia kupitia paa lililoezuliwa pia yaliweza
kuathiri chumba cha kumbukumbu kwa kulowanisha majalada kati ya 100 na
150 yaliyokuwa ndani ya chumba hicho.
Alisema ni muhimu chumba hicho kikaezekwa haraka kutokana na umuhimu
wake hospitalini hapo na kubainisha kuwa jitihada mbalimbali zimekwisha
anza kuchukuliwa ili kukirejesha katika hali yake ya kawaida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni