Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akizungumza na viongozi wa umoja wa vijana (UVCCM) Mkoani Mbeya.
Vijana wa halaiki, wakifanya mazoezi yao katika uwanja wa shule ya sekondari Chimala, wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Vijana wa halaiki, wakichora maumbo mbalimbali kwa kutumia miili yao.....ubunifu....
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa(kushoto), akizungumza na mwalimu wa halaiki hiyo uwanjani hapo, katikati ni katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Mr. Yassin.
Sarakasi....
CCM HOYEEEE.....Akapusipusi, akanyaunyau....
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akizungumza na vijana wa halaiki uwanja wa Chima;la Sekondari.
Vijana wa halaiki wakiwa wamembeba juu Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna.
Wakimbeba mmoja wa matron wao....
MBUNGE wa
viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, amewatembelea vijana walioko
kambini katika shule ya Sekondari ya Chimala wilayani Mbarali mkoani Mbeya na
kuwapa moyo na kuwachangia Mchele nusu gunia, viazi viroba viwili na mahitaji
muhimu kwa kutoa Tsh. 200,000.
Dr.
Mwanjelwa amewaambia vijana hao kuwa mbalina halaiki hiyo, wao ni chachu kubwa
kwa chama na chama kitawathamini kwa kuzingatia msemo wa mchumia juani,
kivulini.
Sherehe za
miaka hiyo 37 za Chama Cha Mapinduzi(CCM), zinatarajia kufanyika Jijini Mbeya
na mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni