Ijumaa, 29 Novemba 2013

ZIARA YA KINANA RUNGWE MKOANI MBEYA

 Wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Mwakaleli wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro na Mbunge wa Viti maalum wanawake mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa.
 Mzee Issa Simion akitoa salaam kwa niaba ya wazee wa Kijiji cha Katende na pia kushukuru kwa Serikali na Chama Cha mapinduzi na pia kuelezea kero zinazohusu wakazi wa kata ya Katende.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Katende ambapo alihimiza sana kuwa makini na vyama vinavyojita vya siasa  kwani sasa vimeanza kupoteza muelekeo.
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya,  Dk.Mary Mwanjelwa akiwasalimia wakazi Katende
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa kijiji ambao walimpa heshima ya kuwa Mzee wa Katende na kumvisha mgolole kama heshima ya mtu mzima.
 Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa ameketi kwenye mkeka unaojulikana kama Kalili aliopewa zawadi na wakina mama wa Katende.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Katende na kuwaahidi CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi na kusema ahadi zilizoahidiwa zitatimizwa.
 
Katibu Mkuu wa CCM aliwaambia wananchi hao kuwa lazima tuhoji serikali  pesa za maendeleo kwa nini haziji kwa wakati.


chanzo;ccm blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...