MWANAMKE MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA
CHRISTINA
HAYOLA (35) MKAZI WA KIJIJI CHA
LIWALANJE, ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI, KIFUANI
NA MGUU WA KULIA
NA MUME
WAKE AITWAYE
MUSSA NSAGAJE @ MWAULAMBO.
MWILI WA
MAREHEMU ULIKUTWA MNAMO TAREHE 30.05.2014
MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MAGAMBA, KATA YA ISANZA, TARAFA YA IGAMBA, WILAYA YA MBOZI
MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI ULIOTOKANA NA WIVU
WA KIMAPENZI ULIOTOKEA WAKIWA KILABUNI USIKU.
MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO.
JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO
AJISALIMISHE MWENYEWE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ABDI SANGA
(20) MKAZI WA ISANGA ALIUAWA KWA
KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE
NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA
SILAHA ZA JADI FIMBO, MAWE NA RUNGU.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 31.05.2014
MAJIRA YA SAA 03:45 USIKU WA KUAMKIA
LEO HUKO ENEO LA FOREST YA ZAMANI KATA YA FOREST, TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA
CHANZO CHA TUKIO HILI NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU NA MWENZAKE MMOJA AMBAYE ALIFANIKIWA
KUKIMBIA KUINGIA NYUMBANI KWA KASSIM
ISSA (28) MKAZI WA FOREST NA KUIBA VITENGE VYENYE
THAMANI YA TSHS 70,000/=, MHANGA ALIPIGA
KELELE ZA KUOMBA MSAADA, HIVYO KUNDI LA WATU WALIJITOKEZA NA KUMSHAMBULIA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA INA
MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA
MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWANAFUNZI WA
DARASA LA TATU KATIKA SHULE YA MSINGI IBUMILA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FATINA FESTO @ MWANDOSYA (12) MKAZI WA KIJIJI CHA MAHONGOLE
ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA
KUDONDOKA KUTOKA KWENYE POWER
TILLER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA AIZACK
MWASHANGWA (22) MKAZI WA MAHONGOLE.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.05.2014
MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA IBUMILA-MAHONGOLE, KATA YA SONGWE-IMALILO, TARAFA YA RUJEWA,
WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAREHEMU NA
WENZAKE WALIKUWA WANATOKA KUVUNA MPUNGA WA SHULE. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA KUACHA POWER TILLER MARA BAADA YA TUKIO.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO
AJISALIMISHE MWENYEWE.
KATIKA TUKIO LA NNE:
MWANAFUNZI WA
KIDATO CHA PILI KATIKA SHULE YA SEKONDARI MAKONGOLOSI ALIYEMBALIWA KWA JINA LA ADEN PETER @NGOMBE (17) MKAZI WA MAKONGOLOSI AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA
KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.117
APK/T.150 AVM AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE ALLY MOSHI (35) MKAZI WA MBARALI.
TUKIO HILO LA
AJALI LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.05.2014
MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO
KATIKA KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA MKOA
WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MAKONGOLOSI/LUPA. CHANZO CHA AJALI DEREVA ALIKUWA
AMELEWAPOMBE. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO CHA POLISI – MAKONGOLOSI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WATUMIAPO VYOMBO VYA MOTO HASA
KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI. AIDHA
ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUFUATA NA KUZINGATIA ALAMA ZA
USALAMA BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA KUTEMBEA PEMBENI MWA BARABARA NA KUVUKA
KATIKA MAENEO YENYE VIVUKO VYA KUVUKIA ILI KUEPUKA AJALI.
TAARIFA YA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWIYULEGHE MBUGHI (60) MKAZI WA KIJIJI
CHA ITENTULA AKIWA ANAMILIKI BILA KIBALI SILAHA /BASTOLA MOJA AINA YA BABY YENYE NAMBA 946663 ILIYOTENGENEZWA NCHINI UBELGIJI IKIWA NA RISASI TATU
[03] KWENYE MAGAZINE.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014
MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU WA KUAMKIA
LEO HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITENTULA, KATA YA
BARA, TARAFA YA ITAKA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUWA
AMEKUFICHA SILAHA HIYO CHUMBANI NDANI YA
NYUMBA YAKE. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA KWA
JAMII KUACHA KUJIMILIKISHA SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAFUATE
TARATIBU ZA UMILIKAJI WA SILAHA KIHALALI.
KATIKA MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DEZDERIS JACKSON (30) MKAZI WA KIJIJI CHA SAZA AKIWA NA KETE 17 ZA BHANGI KWENYE KIBANDA CHA KUUZA SABUNI SAWA NA UZITO WA GRAM 85.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014
MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA SAZA, KATA YA
MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA MSAKO WA TATU:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EVA WILSON
(23) MKAZI WA KIJIJI CHA BWAWANI
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA ANAUZA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA
SERIKALI[VIROBA] AINA YA BOSS PAKETI 51.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014
MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO
KATIKA KITONGOJI NA KIJIJI CHA BWAWANI, KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
HASA WAFANYABIASHARA KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA
MARUKUFU NA SERIKALI KWANI ZINA MADHARA KIAFYA KWA WATUMIAJI.
KATIKA MSAKO WA NNE:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ESTER
MWALUGAJA (34) MKAZI WA KIJIJI
CHA MAMBA-F ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA MBILI [02].
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014
MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MTANDE, KIJIJI CHA MAMBA -F, KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA
KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA
WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOJIHUSISHA NA MTENGENEZAJI
NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.