Mbunge
 wa Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na viongozi wa 
Mahakama ya Qadhi wakati alipotembelea Mahakama hiyo kuona namna 
inavyohudumia waumini wa Dini ya Kiislamu katika kutatua migogoro ya 
ndoa.
Sheikh
 wa Mahakama ya Qadhi, Ramadhani Kaoja akimweleza Mheshimiwa Mbunge 
shughuli za Mahakama hiyo pamoja na changamoto mbalimbali 
zinazowakabili, Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Singida Mjini , Hamis 
Nguli, wa pili kulia ni Katibu wa Mahakama ya Qadhi, Alhajj B. Mlau.
Mbunge
 wa jimbo la Singida Mjini MO akisalimiana na waumini wa Msikiti wa Kata
 ya Mtipa wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Msikiti huo, 
ambapo mara baada ya kuona hatua zilizofikia za ujenzi huo aliahidi 
kutoa  Mabati 50 pamoja na mifuko 50 ya Saraji kwa ajili ya kukamilisha 
ujenzi huo.
MO akitoka kukagua ujenzi wa Msikiti wa kijiji cha Mangwanjuki kata ya Mtipa.
Waumini wa Msikiti wa kijiji ch Mangwanjuki wakimsikiliza Mbunge wao Mheshimiwa MO.
Baadhi ya wapiga kura wa kijiji cha Mangwanjuki wakipeana mikono ya Kheri na Mbunge wao.
Baadhi
 ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Mwankonko darajani 
wakimsikiliza Mbunge wao (hayupo pichani) wakati alipoendelea na zoezi 
la kutembelea nyumba za kuabudu zilizopo jimboni kwake.
Jengo
 la wa Mwankonko darajani likiwa kwenye hatua Lenta, ambapo baada ya 
Mbunge kuona hatua hiyo ya nguvu za wananchi aliahidi Bati 50 na Mifuko 
ya Saruji 50.
Mheshimiwa Mohammed  Dewji na baaadhi ya viongozi wa Msikiti wa kijiji cha Kisasida.
Mbunge
 MO akizungumza na waumini wa Msikiti wa Kisasida, ambapo ameahidi kutoa
 msaada wa Mabati 100 na Mbao 100 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa 
Msikiti huo.
MNEC
 wa Manispaa ya Singida, Hassan Mazala akitoa hamasa kwa wakazi wa 
Kisasida kushiriki Mkutano wa hadhara  ambao umeitishwa kwa ajili ya 
Katibu Mkuu CCM Taifa, Abdulrahman Kinana wa kuongea na wakazi wa jimbo 
la Singida Mjini utakaofanyika viwanja vya People’s Club.
Mheshimiwa Mohammed Dewji akielekea kukagua ujenzi wa Msikiti wa Minga mjini Singida.
Watoto
 wa Madrasa ya Msikiti wa Mwankoko Darajani wakimpokea Mbunge wao kwa 
mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati alipotembelea ujenzi wa Msikiti 
huo.
Mheshimiwa Mohammed Dewji akifurahia jumbe zilizoandikwa  na watoto wa Madrasa ya Mskiti wa Mwankoko Darajani.
Baadhi ya watoto wa Mwankoko Darajani pamoja na wazazi wao wakifurahia ujio wa Mbunge wao.
MO akizungumza na wananchi wa Mwankoko muda mfupi baada ya kukagua ujenzi wa Msikiti.
Mchungaji
 wa Kanisa la FPCT kijiji cha Mtamaa akimpokea Mbunge wa jimbo la 
Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji mara baada ya kuwasili kwenye uwanja 
wa Kanisa hilo.
Waumini wa Kanisa la FPCT Mtamaa wakitumbuiza wakati wa ziara Mbunge MO.
Mbunge MO akijumuika na waumini wa Kanisa la FPCT kutoa burudani wakati wa ziara ya MO.
Mheshimiwa MO akipokea zawadi ya Beberu la Mbuzi kutoka kwa waumini wa Kanisa la FPCT Mtamaa.
MO akipokea zawadi ya Jogoo lililotolewa na waumini wa Kanisa la FPCT liwe linamuamsha asubuhi kwa ajili ya kwenda kazini.
Mmoja wa wazee maarufu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akifuatilia kwa makini hotuba ya Mbunge wake MO.
Bango lililowekwa kwenye Msikiti wa Mtamaa.
Baadhi
 ya wakazi wa kijiji cha Mtamaa wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa 
na MO baada ya kukagua ujenzi wa Msikiti wa Mtamaa.
Mheshimiwa MO akizungumza na waumini wa Msikiti wa kijiji cha Mtamaa.
Mheshimiwa MO akifurahia watoto wa kijiji cha Ng’aida kata ya Unyamiku wakati wa ziara yake.
Mbunge MO akishiriki dua kwenye kijiji cha Msikiti wa Ng’aida.
Mheshimiwa MO akiwa na watoto wa kijiji cha Ng’aida.
Mheshimiwa MO akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka kwa waumini wa Msikiti wa kijiji cha Ng’aida.
Baadhi
 ya waandishi wa habari waliombatana na Mheshimiwa Mbunge kwenye ziara 
hiyo. Kushoto ni Nathaniel Limu na Kulia ni Hillary Shoo.
 http://dewjiblog.com
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni