Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akiwasalimu wanawake na kuwapa pole katika Kijiji cha Nyerere wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Pokea mkono wa Baraka.....
MBALI na Mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya, Dr,
Harrison Mwakyembe, kutoa misaada kwa waathirika wa mafuriko Jimboni humo, Mbunge wa viti maalum (CCM), Mkoa wa Mbeya,
Dr. Mary Mwanjelwa, naye amejitokeza na kutoa misaada ya kiutu kwa wananchi wa
wilaya hiyo.
Akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara wa
Kijiji cha Nyerere, Dr. Mary Mwanjelwa, alisema mbali na kwamba mafuriko hayo
yameathiri kaya nyingi, lakini ana uhakika kuwa wanawake na watoto ndiyo
walioathirika zaidi.
“Maandiko yanasema lieni na wanaolia, najua wakati
mafuriko yanatokea wengine yamewakuta wakiwa wajawazito, ninyi siyo wakiwa,
tupo pamoja, nilipopata taarifa hii sikuweza kukaa na amani pale Bungeni,
nimeacha posho na kuja kuwapa pole ndugu zangu’’ alisema Dr.Mwanjelwa huku
akipiga magoti.
Diwani wa kata ya Bujonde, Paul Mwambafula, alisema Kata
yake ndiyo kata iliyoathirika zaidi katika wilaya hiyo ambapo kaya 2,400
zilikumbwa na mafuriko hayo, lakini kaya 1800, ziliathirika zaidi.
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania(UWT), Pricila
Mbwaga na Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya, Mariam Yusuph, waliwaambia wananchi wa
Kijiji cha Nyerere na Mpunguti kuwa, tatizo hilo siyo la kwao peke yao, maana
dunia imelisikia.
Mkuu wa wilaya ya Kyela, Magreth Malenga na Afisa tarafa
ya Unyakyusa, Kheri William, walimshukuru Mbunge, Dr. Mwanjelwa kuwa mstari wa
mbele kujitoa kusaidia wenye uhitaji na kwamba kamati ya maafa ya wilaya hiyo,
itamalizia kusaidia kaya zilizoathirika katika Kijiji cha Nyerere.
Dr. Mwanjelwa alitoa mashuka 150 katika Vijiji vya
Nyerere na Mpunguti na kutoa wito kwa taasisi na watu binafsi kujitokeza
kuwasaidia wananchi wa wilaya hiyo walioathirika na mafuriko hayo.
Baadhi ya mashuka yalitolewa na benki ya NMB baada ya
Mbunge huyo kuiomba taasisi hiyo ya kifedha, ambayo mbali na mashuka,
ilimkabidhi madawati 83 kwa ajili ya shule za Msingi.
“Benki ya NMB inatoa huduma zake katika jamii ya watu
mbalimbali. Wanafunzi, watoto, watu wazima, wazee, mashirika na makampuni na
wateja mbalimbali. Sis kwetu hawa wote ni wadau ambao ndio wanafanya NMB
iendelee kuwepo’’ alisema Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za juu kusini, Lucresia
Makiriye.
Akishukuru kwa niaba ya wananchi wenzake wa Kijiji cha
Mpunguti, Mzee Water Butungulu, alienda mbali na kumweleza Dr. Mwanjelwa kuwa
endapo atawania nafasi ya Ubunge mwakani, atashinda kutokana na juhudi zake za kuhudumia jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni