Jumamosi, 31 Mei 2014

MWANAMKE MMOJA AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI NA MUME WAKE.



MWANAMKE MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA CHRISTINA HAYOLA (35) MKAZI WA KIJIJI CHA LIWALANJE, ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI, KIFUANI NA MGUU WA KULIA  NA MUME  WAKE AITWAYE MUSSA NSAGAJE @ MWAULAMBO.

MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAGAMBA, KATA YA ISANZA, TARAFA YA IGAMBA, WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI ULIOTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI ULIOTOKEA WAKIWA KILABUNI USIKU.

  MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.


KATIKA TUKIO LA PILI:

MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ABDI SANGA (20) MKAZI WA ISANGA ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE  NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO, MAWE NA RUNGU.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 31.05.2014 MAJIRA YA SAA 03:45 USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO ENEO LA FOREST YA ZAMANI KATA YA FOREST, TARAFA YA  SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA  MAREHEMU NA MWENZAKE MMOJA AMBAYE ALIFANIKIWA KUKIMBIA KUINGIA NYUMBANI KWA KASSIM ISSA (28)  MKAZI WA FOREST NA KUIBA VITENGE VYENYE THAMANI YA  TSHS 70,000/=,  MHANGA ALIPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA, HIVYO KUNDI LA WATU WALIJITOKEZA NA KUMSHAMBULIA. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA INA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.


KATIKA TUKIO LA TATU:

MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU KATIKA SHULE YA MSINGI IBUMILA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FATINA FESTO @ MWANDOSYA (12) MKAZI WA KIJIJI CHA MAHONGOLE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA  KUDONDOKA KUTOKA  KWENYE POWER TILLER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA AIZACK MWASHANGWA (22) MKAZI WA MAHONGOLE.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA IBUMILA-MAHONGOLE, KATA YA SONGWE-IMALILO, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAREHEMU NA WENZAKE WALIKUWA WANATOKA KUVUNA MPUNGA WA SHULE. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA KUACHA POWER TILLER MARA BAADA YA TUKIO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.


KATIKA TUKIO LA NNE:

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI KATIKA SHULE YA SEKONDARI MAKONGOLOSI ALIYEMBALIWA KWA JINA LA ADEN PETER @NGOMBE (17) MKAZI WA MAKONGOLOSI AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.117 APK/T.150 AVM AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE ALLY MOSHI (35) MKAZI WA MBARALI.

TUKIO HILO LA AJALI LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MAKONGOLOSI/LUPA. CHANZO CHA AJALI DEREVA ALIKUWA AMELEWAPOMBE. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO CHA POLISI – MAKONGOLOSI.

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WATUMIAPO VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUFUATA NA KUZINGATIA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA KUTEMBEA PEMBENI MWA BARABARA NA KUVUKA KATIKA MAENEO YENYE VIVUKO VYA KUVUKIA ILI KUEPUKA AJALI.

TAARIFA YA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWIYULEGHE MBUGHI (60) MKAZI WA KIJIJI CHA ITENTULA AKIWA ANAMILIKI BILA KIBALI SILAHA /BASTOLA MOJA AINA YA   BABY YENYE NAMBA 946663 ILIYOTENGENEZWA NCHINI UBELGIJI IKIWA NA RISASI TATU [03] KWENYE MAGAZINE.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITENTULA, KATA YA   BARA, TARAFA YA ITAKA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUWA AMEKUFICHA SILAHA HIYO CHUMBANI NDANI YA   NYUMBA YAKE. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA KWA JAMII KUACHA KUJIMILIKISHA SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAFUATE TARATIBU ZA UMILIKAJI WA SILAHA KIHALALI.

KATIKA MSAKO WA PILI:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DEZDERIS JACKSON (30) MKAZI WA KIJIJI CHA SAZA AKIWA NA KETE 17 ZA BHANGI KWENYE KIBANDA CHA KUUZA SABUNI SAWA NA UZITO WA GRAM 85.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SAZA, KATA YA   MKWAJUNI,   TARAFA YA   KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


KATIKA MSAKO WA TATU:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EVA WILSON (23) MKAZI WA KIJIJI CHA BWAWANI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA ANAUZA  POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI[VIROBA] AINA YA  BOSS PAKETI 51.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI NA KIJIJI CHA BWAWANI, KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA   KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA WAFANYABIASHARA KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUKUFU NA SERIKALI KWANI ZINA MADHARA KIAFYA KWA WATUMIAJI.


KATIKA MSAKO WA NNE:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ESTER MWALUGAJA (34) MKAZI WA KIJIJI CHA MAMBA-F ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA   POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA MBILI [02].

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MTANDE, KIJIJI CHA MAMBA -F, KATA YA   MAMBA, TARAFA YA   KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.


TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.

            KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOJIHUSISHA NA MTENGENEZAJI NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...