Naibu waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Juma Nkamia amesema ‘serikali kuu hutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji na gharama halisi ya wakati husika ambapo mwaka 2012 jumla ya shilingi milioni mia sita hamsini (650) zilitengwa kwa ajili ya kuadhimisha uzinduzi na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru na kati ya hizo milioni 450 zilitumiwa na Wizara na milioni 200 zilitumiwa na mkoa uliokua mwenyeji wa sherehe za kilele’
‘Kuhusu kiasi cha fedha kinachotumiwa na wilaya, ni kwamba zinatofautiana kulingana na michango ya Wananchi katika wilaya husika kwani michango hiyo ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambayo huzinduliwa wakati ya mbio za mwenge, kwa ujumla mwaka 2012 Wananchi walichangia zaidi ya BILIONI 11 na milioni 500′
‘Mbio za mwenge wa uhuru hutumika kuhimiza miradi mbalimbali kwa njia ya kuweka mawe ya msingi au kuzindua miradi iliyowekewa jiwe la msingi mwaka uliopita na pia kuhamasisha moyo wa Wazalendo na kujitolea kwa vijana hasa kuonyesha umuhimu na nafasi yao katika kudumisha nchi yao, kulinda uhuru na kuleta maendeleo ya nchi yao’
Baada ya kusoma haya yaliyosemwa na Naibu waziri wa habari Juma Nkamia leo May 27 2014 bungeni,
Credit; millardayo.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni