Mbunge
wa Jimbo la Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), Naibu Waziri wa
Fedha ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mh. Mwigulu Nchemba
wakiwa kwenye boda boda, wakati wa msafara wa kuelekea kwenye mkutano wa
hadhara wa CCM uliofanyika eneo la viwanja vya People’s Club mjini
Singida.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana , sambamba na Katibu wa Itikadi
na Uenezi Nape Nnauye,wakiwasili kwenye viwanja vya People’s Club
kwenye mkutano wa hadhara kwa staili ya aina yake kwa kutumia usafiri wa
Bajaji.
Katibu
mkuu wa CCM , Kinana, (kwanza kulia),akifurahia ujumbe ulioandikwa
kwenye bango la wajasiriamali waliohudhuria mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya Peoples klabu mjini Singida.
Mkuu
wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,(wa kwanza kushoto) akishiriki kutoa
burudani kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya katibu mkuu
CCM taifa,Abrahamani Kinana,kuzungumza na wakazi wa jimbo la Singida
mjini.
Naibu
waziri wa fedha Adamu Malima,(wa kwanza kushoto) akifurahia jambo na
mbunge wa jimbo la Singida mjini juzi kwenye hafla ya mbunge Dewji
kukabidhi msaada mabati na mifuko yenye thamani ya zaidi ya shilingi
125 milioni.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji akiwa na Mbunge wa Jimbo la
Manyoni Mashariki Kepteni John Chiligati wakiwapungia wananchi mikono
kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadgara kwenye viwanja vya Peoples Club
mjini Singida.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi wa
Manispaa ya Singida wakati wa mkutano wa hadhara kwenye viwanja hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk, Parseko Kone akizungumza kwenye Mkutano huo.
Baadhi
ya wakazi wa manispaa ya Singida,waliohudhuria mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya peoples klabu mjini hapa.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi Charles Tzeba akihutubia wananchi wa Singida mjini
na kuwambia tatizo la usafiri wa treni limepatiwa ufumbuzi wa kudumu
kwani Reli ya kati inaboreshwa na tayari vichwa 40 vya treni vitaanza
kazi ifikapo Januari hivyo gharama za usafiri wa treni kwa abiria na
mizigo itashuka.
Naibu
katibu mkuu CCM taifa Mwigullu Nchemba, akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya people klabu mjini Singida.
Mbunge
wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gulam Dewji,akizungumza kwenye
mkutano wa hadhara muda mfupi kabla hajakabidhi msaada wa Mabati na
Saruji mwenye thamani ya zaidi ya shilingi 125 kwa ujenzi wa misikiti na
makanisa.
Mbunge
wa jimbo la Singida mjini Mohammed Gulam Dewji ( kulia) akimkabidhi
sehemu ya msaada wa mabati na mfuko wa saruji yaliyotoa kwa ajili ya
kuchangia ujenzi wa misikiti na makanisa jimbo la Singida mjini.
Naibu
waziri wa maji,Amossi Makala,(wa kwanza kulia),mbunge wa jimbo la
Singida mjini,Mohammed Dewji,mbunge wa jimbo la Manyoni mashariki,John
Chiligati,mjumbe wa mkutano mkuu NEC taifa CCM manispaa ya
Singida.Hassan Mazala,naibu waziri wa fedha,Adamu Malima,wakifuatilia
hotuba iliyokuwa ikitolewa na katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa ,Abdulrahman Kinana (katikati), Nape Nnauye na
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini MO wakiteta jambo kabla ya kukabidhi
misaada ya saruji na Mabati kwenye taasisi za dini jimboni humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dk, Parseko Kone akifurahia jambo na Naibu Waziri wa
Fedha, Mh. Adamu Malima, sambamba na Mbunge wa Jimbo la Manyoni
Mashariki, Kapten John Chiligati.
Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Matha Mlata, akiangalia picha
mbalimbali kutoka kwa mmoja wa wapiga picha walikuwemo kwenye mkutano
huo,sambamba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na
Uratibu), Stephen Wasira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni