Jumatano, 11 Juni 2014

WAKULIMA WADOGO WAASWA KEPUKA MATUMIZI YA KEMIKALI ZENYE ATHARI KWA MAZINGIRA NA AFYA.

Picha na 1Mshindi wa tuzo mbalimbali na mwanaharakati wa mazingira duniani Dkt.Vandana Shiva kutoka nchini India akisisitiza jambo kuhusu umuhimu wa wakulima wadogo ambao wanazalisha 70% ya chakula kinachotumiwa duniani kote walivyo na wajibu wa kuiepusha jamii na matumizi ya vyakula vinavyozalishwa na kuhifadhiwa na kemikali za viwandani zenye madhara kwa afya.Picha no 2Mkurugenzi wa Taasisi ya Kilimo Hai Tanzania Bw. Jordan Augustino (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa Tanzania katika mkutano wa kimataifa wa mwaka wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kilimo utakaofanyika June 12 katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es salaam ambapo washiriki wa mkutano huo watabadilishana uzoefu kuhusu mchango wa wakulima wadogo katika sekta ya kilimo.Picha no 3Mratibu wa Muungano huru wa watetezi wa Kilimo Hai na Chakula Salama Barani Afrika (AFSA) kutoka Ethiopia Dkt. Million Belay akiongea na waandishi wa habari kuhusu  umuhimu wa kilimo kinachoendana na mazingira halisi barani Afrika leo jijini Dar es salaamPicha no 4Mshindi wa tuzo mbalimbali na mwanaharakati wa mazingira duniani Dkt.Vandana Shiva kutoka nchini India akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kitabu kinachoelezea shughuli mbalimbali za binadamu zinavyoathiri uharibifu wa mazingira ya asili duniani. Kulia ni Muhamasishaji na mtetezi wa uhifadhi wa Mazingira kutoka Greenpeace Bw. Glen Tyler.Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
……………………………………………….
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Dar es salaam.
Wito umetolewa kwa wakulima wadogo kote nchini kuzingatia kilimo salama kinachohimiza matumizi ya mbolea za asili ili kupata mazao bora na salama kwa afya ya jamii na kuepuka kutumia kemikali zenye athari kwa uhifadhi wa mazingira.
Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es salaam mshindi wa tuzo mbalimbali na mwanaharakati wa mazingira duniani Dkt.Vandana Shiva kutoka nchini India amesema kuwa wakulima wadogo ambao wanazalisha 70% ya chakula kinachotumiwa duniani wanao wajibu wa kuiepusha jamii na matumizi ya vyakula vinavyozalishwa na kuhifadhiwa na kemikali za viwandani zenye madhara kwa afya.
Dkt. Vandana ambaye yuko nchini Tanzania kuungana na wadau wengine wa kutetea kilimo salama na rafiki wa mazingira wanaohudhuria  mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kilimo ameeleza kuwa yeye pamoja na wadau wengine wanaendelea kuhamasisha wakulima duniani kote kupitia programu zinazohimiza kilimo kinachoshabihiana na mazingira ya asili na uhifadhi wa mazingira kwa chakula salama barani Afrika.
Amesema kuwa yeye pamoja na wadau wengine wa Muungano huru wa watetezi wa Kilimo Hai na Chakula Salama Barani Afrika (AFSA) wanaamini kuwa chakula bora na salama ni kile kinachozalishwa kutokana na ardhi na si vinginevyo na kuongeza kuwa kilimo kinachohimiza matumizi ya mbegu na mbolea za viwandani licha ya kuwa na gharama kubwa za uzalishaji kina athari na madhara kwa afya na viumbe wengine wakiwemo nyuki na vipepeo.
“Ninao ushahidi wa kutosha unaoonesha madhara makubwa yanayotokana na matumizi ya madawa makali na kemikali za viwandani kwa afya ya binadamu na viumbe wengine wa asili ambayo kama tusipochukua tahadhari mapema dunia itakua si mahali salama pa kuishi” amesema.
Kwa upande wake Mratibu wa Muungano huru wa watetezi wa Kilimo Hai na Chakula Salama Barani Afrika (AFSA) kutoka Ethiopia Dkt. Million Belay amesisitiza kuwa kilimo kinachoendana na mazingira halisi ndicho kitakacholifanya bara la Afrika kujitosheleza kwa chakula.
 Amesema wao kama muungano na watetezi wa kilimo kinachozingatia uhifadhi wa mazingira wanaendelea kufanya tafiti mbalimbali na tayari baadhi ya nchi za Afrika zikiwemo Ghana,Ethiopia,Tanzania na Msumbiji zimechaguliwa katika mpango huo wenye lengo la kuwafanya wananchi wake kujitosheleza kwa chakula .
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Kilimo Hai Tanzania Bw. Jordan Augustino ameeleza kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano huo wa kimataifa utakaofanyika June 12 katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es salaam ambapo washiriki wa mkutano huo watabadilishana uzoefu kuhusu mchango wa wakulima wadogo katika sekta ya kilimo.

CHANZO FULL SHANGWE

Jumapili, 8 Juni 2014

MBUNGE DR.MWANJELWA, ANAVYOWAJALI WAHITAJI MBEYA

Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akimkabidhi mashuka Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Magreth Malenga na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Clemens Kasongo, kabla ya kwenda kuwakabidhi wananchi walioathirika na mafuriko mwaka huu 2014.
 
MBALI na Mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya, Dr, Harrison Mwakyembe, kutoa misaada kwa waathirika wa mafuriko Jimboni humo,  Mbunge wa viti maalum (CCM), Mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, naye amejitokeza na kutoa misaada ya kiutu kwa wananchi wa wilaya hiyo.
 
 
Mbunge huyo wa viti maalum, alifika wilayani Kyela Mei 22, mwaka huu.
 
Akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara wa Kijiji cha Nyerere, Dr. Mary Mwanjelwa, anasema mbali na kwamba mafuriko hayo yameathiri kaya nyingi, lakini ana uhakika kuwa wanawake na watoto ndiyo walioathirika zaidi.
 
“Maandiko yanasema lieni na wanaolia, najua wakati mafuriko yanatokea wengine yamewakuta wakiwa wajawazito, ninyi siyo wakiwa, tupo pamoja, nilipopata taarifa hii sikuweza kukaa na amani pale Bungeni, nimeacha posho na kuja kuwapa pole ndugu zangu’’ anasema Dr.Mwanjelwa huku akipiga magoti.
 
 
Diwani wa kata ya Bujonde, Paul Mwambafula, anamshukuru Mbunge huyo kwa kusema Kata yake ndiyo kata iliyoathirika zaidi katika wilaya hiyo ambapo kaya 2,400 zilikumbwa na mafuriko hayo, lakini kaya 1800, ziliathirika zaidi.
 
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania(UWT), Pricila Mbwaga na Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya, Mariam Yusuph, waliwaambia wananchi wa Kijiji cha Nyerere na Mpunguti kuwa, tatizo hilo siyo la kwao peke yao, maana dunia imelisikia.
 
Mkuu wa wilaya ya Kyela, Magreth Malenga na Afisa tarafa ya Unyakyusa, Kheri William, wanamshukuru Mbunge, Dr. Mwanjelwa kuwa mstari wa mbele kujitoa kusaidia wenye uhitaji na kwamba kamati ya maafa ya wilaya hiyo, itamalizia kusaidia kaya zilizoathirika katika Kijiji cha Nyerere.
 
Dr. Mwanjelwa alitoa mashuka 150 katika Vijiji vya Nyerere na Mpunguti na kutoa wito kwa taasisi na watu binafsi kujitokeza kuwasaidia wananchi wa wilaya hiyo walioathirika na mafuriko hayo.
 
Baadhi ya mashuka yalitolewa na benki ya NMB baada ya Mbunge huyo kuiomba taasisi hiyo ya kifedha, ambayo mbali na mashuka, ilimkabidhi madawati 83 kwa ajili ya shule za Msingi.
 
“Benki ya NMB inatoa huduma zake katika jamii ya watu mbalimbali. Wanafunzi, watoto, watu wazima, wazee, mashirika na makampuni na wateja mbalimbali. Sis kwetu hawa wote ni wadau ambao ndio wanafanya NMB iendelee kuwepo’’ alisema Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za juu kusini, Lucresia Makiriye.
 
Akishukuru kwa niaba ya wananchi wenzake wa Kijiji cha Mpunguti, Mzee Water Butungulu, alienda mbali na kumweleza Dr. Mwanjelwa kuwa endapo atawania nafasi ya Ubunge mwakani, atashinda kutokana  na juhudi zake za kuhudumia jamii.
 
Mbali na msaada huo kwa waathirika wa mafuriko, Mbunge huyo anasema ‘’Kuanzia mwaka 2010, kwa kukumbuka baadhi ya niliyoyafanya ni pamoja na kujumuika na kuwasaidia yatima,  kusaidia vikundi vya akina mama na kufadhili semina za madiwani wa vyama vyote juu ya utendaji bora’’ anasema Dr. Mwanjelwa.
 
Anaeleza kuwa ni mambo mengi ya jamii aliyoshiriki na mengine ameyasahau lakini anakumbuka pia aligawa magodoro 250 katika hospital za serikali katika wadi za wazazi wilaya ya Ileje, Mbozi, Chimala(Mbarali), Ruanda na hospitali ya Rufaa ya Mbeya kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya.
 
Sanjali na vitu hivyo, anasema kuwa alitoa pia viti vya walemavu wa viungo katika Jiji la Mbeya mbele ya Askofu kiongozi wa kanisa la Moravian Tanzania Alinikisa Cheyo siku alipokuwa akimshukuru Mungu kwa kumponya na mauti katika ajali mbaya aliyoipata mwaka jana 2012.
 
Katika masuala ya uongozi, anasema aliendesha semina kwa madiwani wa vyama vyote vya siasa na atazidi kufanya hivyo kwa kufadhili mafunzo/semina za mara kwa mara kwa Madiwani wote wa Mkoa wa Mbeya, juu ya Uongozi na uwajibikaji.
 
‘’Mbali na mafunzo ya madiwani hao, nimewahi kuendesha mafunzo/semina kwa watendaji wote wa ngazi ya kata juu ya Uongozi na uwajibikaji na nitazidi kufanya hivyo’’ anasema.
 
Kabla ya kujikita katika masuala ya siasa alikuwa Mkurugenzi wa shirika la PSI Tanzania ambako historia haimuhukumu hata baada ya kutoka huko kwa kile kinachojieleza kuwa alitoka na utumishi uliotukuka.
 

Jumanne, 3 Juni 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 03.06.2014.



KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA NDONYA SUGU (23) MKAZI WA KIJIJI CHA MAFYEKO ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA ZAHANATI YA CHA BITIMANYANGA BAADA YA KUPIGWA FIMBO KICHWANI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.06.2014 MAJIRA YA SAA 02:30 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA ITAGA, KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA MAFYEKO, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MAREHEMU ALIPIGWA FIMBO KICHWANI TAREHE 01.06.2014 MAJIRA YA SAA 16:30 JIONI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SHAGEMBE KUNAWIJI (54) MKAZI WA KIJIJI CHA BITIMANYANGA WAKATI WANACHEZA NGOMA ZA KABILA LA KISUKUMA MAARUFU KWA JINA LA CHAGULAGA KIJIJINI HAPO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.


KATIKA TUKIO LA PILI:

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.163 ATQ AINA YA TOYOTA HAICE LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA GODFREY AWDHI NGOLE (32) MKAZI WA IGURUSI KUACHA NJIA NA KISHA KUPINDUKA KATIKA ENEO LA MAMBI WILAYA YA MBARALI.

ABIRIA MMOJA KATI YA WAWILI ALITAMBULIKA KWA JINA LA ELIZABETH MKARAWE (30) MKAZI WA IGURUSI NA 2. MSICHANA MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI WALIFARIKI DUNIA. AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 02.06.2014 MAJIRA YA SAA 11:50 ASUBUHI KATIKA ENEO LA MAMBI, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/NJOMBE.

AIDHA KATIKA TUKIO HILO WATU SABA WALIJERUHIWA KATI YAO WANAUME WATATU NA WANAWAKE WAWILI AKIWEMO DEREVA WA GARI HILO.CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MIILI YA MAREHEMU NA MAJERUHI WAPO HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.

KATIKA TUKIO LA TATU

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA NAKONDE NCHINI ZAMBIA LINAMSHIKILIA JAMBAZI MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JIMMY NYILENDA RAIA WA ZAMBIA BAADA YA  KUJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI KATIKA JARIBIO LA UNYANG’ANYI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.06.2014 MAJIRA YA SAA 17:45 JIONI KATIKA ENEO LA MPAKANI KATI YA TANZANIA NA ZAMBIA [TUNDUMA/NAKONDE]. INADAIWA KUWA WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WALIFYATUA RISASI OVYO KWA LENGO LA KUWAPORA PESA WABADILISHAJI FEDHA WA ENEO HILO NA POLISI WA TUNDUMA [TANZANIA] NA NAKONDE [ZAMBIA] WALIKABILIANA NA MAJAMBAZI HAO. KATIKA MAJIBIZANO HAYO, MAJAMBAZI WATATU WALIUAWA WAWILI  WAKIFAHAMIKA KUWA NI SIKAPWITE BONIPHACE  MFANYAKAZI WA COUNCIL NAKONDE RAIA WA ZAMBIA NA CHAPWA KIPAKWA RAIA NA MKAZI WA ZAMBIA  NA MWINGINE HAKUWEZA KUFAHAMIKA.

AIDHA MAJAMBAZI WENGINE WALIWEZA KUKIMBIA NA JAMBAZI MMOJA JIMMY NYILENDA RAIA WA ZAMBIA AMEKAMATWA AKIWA  MAHUTUTI BAADA YA  KUJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI.

KATIKA TUKIO HILO SILAHA MBILI AINA YA AK-47 ZENYE NAMBA 625562 NA 1963EC58 ZILIKAMATWA. HATA HIVYO KATIKA MAJIBIZANO HAYO RAIA WAWILI WA NAKONDE –ZAMBIA WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA.HAKUNA MADHARA KWA ASKARI NA SILAHA ZIPO POLISI NAKONDE ZAMBIA. JUHUDI ZA KUWATAFUTA MAJAMBAZI WALIOKIMBIA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA HAO WA TUKIO LA UJAMBAZI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUWA MAKINI KWA KUCHUKUA TAHADHARI KATIKA KAZI ZAO.

KATIKA MSAKO:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WANYAMAPORI TANAPA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMOS NAIMWA (30) MKAZI WA KIJIJI CHA UTURO AKIWA NA SILAHA/BUNDUKI MOJA AINA YA GOBOLE NA GOROLI 12 BILA KIBALI.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 31.05.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA KATIKA KIJIJI NA KATA YA   ULANGA, TARAFA YA   RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAFUATE TARTIBU ZA UMILIKAJI SILAHA KIHALALI  ILI KUEPUKA MATATIZO.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Jumatatu, 2 Juni 2014

MWIGULU NCHEMBA APINGA BUNGE LA KATIBA KUONGEZEWA SIKU 60

MWIGULU NCHEMBA
UWEZEKANO wa bunge maalumu la Katiba kukaa kwa siku zingine 60 umeingia doa baada ya Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kusema kwamba hakubaliani na mapendekezo hayo.

Aliyasema hayo juzi wakati aakihutubia mamia ya wakazi wa manispaa ya Iringa na vitongoji vyake katika mkutano uliopewa jina la Ondoa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.

Alisema atapinga kwa nguvu zake zote bunge hilo kukutana kwa siku nyingine 60 kwasababu ikifanyika hivyo itakuwa ni sawa na kutumia vibaya fedha za walipa kodi.

Pamoja na kupinga bunge hilo kukutana kwa siku nyingine 60 alisema atamshauri Spika wake amuandikie Rais barua ya kulivunja endapo watashindwa kuzitumia wiki mbili za mwanzo kujadili mambo ya msingi katik rasimu hiyo.

Alisema nchi imepoteza fedha nyingi katika awamu ya kwanza ya mjadala wa rasimu ya katiba hiyo kwani kwa zaidi ya siku 40 walikuwa wakilumbana kuhusu kanuni na muundo wa serikali.

Alisema kuliko kuendelea kupoteza fedha kwa kuwalipa wabunge wanaolumbana kwa mambo yanayojadilika ni bora fedha hizo zikapelekwa katika sekta zingine za maendeleo.

Kuhusu uchumi
Katika kuboresha uchumi wa nchi Mwigulu alisema; “Tunapeleka sheria ya kufuta misamaha ya kodi; tunataka wakubwa na wadogo kwa pamoja walipe kodi; habari ya likizo ya kodi haitakuwepo tena.” 

Pamoja na sheria hiyo kuahidi kupelekwa katika bunge hili bajeti, Mwigulu alisema serikali itapeleka sheria nyingine ya kubana matumizi.

Alisema kwa kupitia sheria hizo mapato ya serikali yataongezeka na kusaidia kuimarisha uchumi wa nchi.

“Mapato hayo yatatuweka katika mazingira ya kuboresha maslai ya watumishi wa umma wakiwemo walimu na polisi,” alisema huku akisisitiza kwamba hilo linawezekana kama mapato ya serikali yataimarika.

“Inawezekanaje mzazi mkulima asomeshe mtoto hadi kidato cha sita kwa mapato yanayotokana uuzaji wa vitumbua halafu serikali ikashindwa kumpatia mkopo kwa ajili ya elimu yake ya juu,” alisema.

Chanzo;bongo leaks

Jumamosi, 31 Mei 2014

FAIDA ZA WAJAWAZITO KUJIFUNGULIA VITUO VYA AFYA HIZI HAPA

IKIWA mkoa wa Mbeya una asilimia 57 ya wajawazito wanaojifungulia hospitali na vituo vya afya, wito umetolewa kwao kujitokeza kwa wingi kuhudhuria Kliniki ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Mhadhiri, kaimu mkuu wa taasisi ya tiba ya St. Aggrey Jijini Mbeya, Dr. Karim Segumba.
Dr. Karim alisema kuwa faida wanazozipata wajawazito wanapohudhuria Kliniki ni pamoja na mjamzito kuchunguzwa afya yake kwa undani, ikiwemo umri wa mimba, kimo cha mimba, historia ya uzazi wa awali, uwingi wa damu, mkojo kwa protini na kutoa wasiwasi wa kifafa cha mimba.

‘’Mwanamke anachunguzwa shinikizo la damu, mlalo wa mtoto, mapigo ya moyo ya mtoto, ikibidi ultrasound kuangalia kama mtoto yupo hai, au ni mlemavu, ukubwa wa mtoto, kondo la nyuma la mama, kukomaa kwa mtoto, nyonga za mama kama zinaruhusu kujifungua kwa njia ya kawaida au upasuaji na anaelezwa tarehe ya makisio ya kujifungua’’ alisema Dr. Karim.

Mbali na uchunguzi huo, alisema kuwa mjamzito anayehudhuria kliniki anapimwa pia VVU na anapoonekana kuwa ana maambukizi anapewa mbinu za kumkinga mtoto aliye tumboni.

Alipoulizwa madhara yanayoweza kuwapata wajawazito ambao hawaendi kliniki na hawajifungulii hospitali na vituo vya afya, alisema ni pamoja na mjamzito kutoelewa maendeleo ya mimba yake na hatari ambazo zingeweza kugundulika na kutatuliwa na wataalam ili kuzuia kifo chake na mtoto.

‘’Hivyo ili kupunguza vifo vya mama na mtoto ni muhimu wajawazito wakahudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya tiba na kizuri zaidi huduma zote hizo kwa mama mjamzito na mtoto chini ya miaka mitano hutolewa bure kote nchini’’ alisema mhadhili huyo.

Mratibu wa huduma ya mama na mtoto katika hospitali ya mkoa wa Mbeya Prisca Butuyuyu, alisema kwa sasa mkoa wa Mbeya, wajawazito wengi wanahudhuria kliniki lakini wengi wao wanajifunguli nyumbani.

Aliitaja wilaya ya Ileje kuwa ndiyo wilaya inayoongoza kwa wajawazito kujifungulia nyumbani, ambapo Jiji la Mbeya linaongoza kwa wajawazito wengi kujifungulia katika vituo vya tiba.

‘’Zaidi ya asilimia 40 wajawazito wanajifungulia nyumbani lakini baadhi wanajifungulia kwa wakunga wa jadi na njiani ingawa hatuna takwimu sahihi zaidi’’ alisema Butuyuyu.

Alisema Jiji la Mbeya wajawazito wanajifungulia hospitali hasa hospitali ya wazazi Meta kwa asilimia 109, Kyela 67, Chunya 58, Rungwe 55, Mbozi 45, Mbeya Vijijini asilimia 38 na wilaya ya Ileje asilimia 33.

FAIDA ZA WAJAWAZITO KUJIFUNGULIA VITUO VYA AFYA HIZI HAPA

IKIWA mkoa wa Mbeya una asilimia 57 ya wajawazito wanaojifungulia hospitali na vituo vya afya, wito umetolewa kwao kujitokeza kwa wingi kuhudhuria Kliniki ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Mhadhiri, kaimu mkuu wa taasisi ya tiba ya St. Aggrey Jijini Mbeya, Dr. Karim Segumba.
Dr. Karim alisema kuwa faida wanazozipata wajawazito wanapohudhuria Kliniki ni pamoja na mjamzito kuchunguzwa afya yake kwa undani, ikiwemo umri wa mimba, kimo cha mimba, historia ya uzazi wa awali, uwingi wa damu, mkojo kwa protini na kutoa wasiwasi wa kifafa cha mimba.

‘’Mwanamke anachunguzwa shinikizo la damu, mlalo wa mtoto, mapigo ya moyo ya mtoto, ikibidi ultrasound kuangalia kama mtoto yupo hai, au ni mlemavu, ukubwa wa mtoto, kondo la nyuma la mama, kukomaa kwa mtoto, nyonga za mama kama zinaruhusu kujifungua kwa njia ya kawaida au upasuaji na anaelezwa tarehe ya makisio ya kujifungua’’ alisema Dr. Karim.

Mbali na uchunguzi huo, alisema kuwa mjamzito anayehudhuria kliniki anapimwa pia VVU na anapoonekana kuwa ana maambukizi anapewa mbinu za kumkinga mtoto aliye tumboni.

Alipoulizwa madhara yanayoweza kuwapata wajawazito ambao hawaendi kliniki na hawajifungulii hospitali na vituo vya afya, alisema ni pamoja na mjamzito kutoelewa maendeleo ya mimba yake na hatari ambazo zingeweza kugundulika na kutatuliwa na wataalam ili kuzuia kifo chake na mtoto.

‘’Hivyo ili kupunguza vifo vya mama na mtoto ni muhimu wajawazito wakahudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya tiba na kizuri zaidi huduma zote hizo kwa mama mjamzito na mtoto chini ya miaka mitano hutolewa bure kote nchini’’ alisema mhadhili huyo.

Mratibu wa huduma ya mama na mtoto katika hospitali ya mkoa wa Mbeya Prisca Butuyuyu, alisema kwa sasa mkoa wa Mbeya, wajawazito wengi wanahudhuria kliniki lakini wengi wao wanajifunguli nyumbani.

Aliitaja wilaya ya Ileje kuwa ndiyo wilaya inayoongoza kwa wajawazito kujifungulia nyumbani, ambapo Jiji la Mbeya linaongoza kwa wajawazito wengi kujifungulia katika vituo vya tiba.

‘’Zaidi ya asilimia 40 wajawazito wanajifungulia nyumbani lakini baadhi wanajifungulia kwa wakunga wa jadi na njiani ingawa hatuna takwimu sahihi zaidi’’ alisema Butuyuyu.

Alisema Jiji la Mbeya wajawazito wanajifungulia hospitali hasa hospitali ya wazazi Meta kwa asilimia 109, Kyela 67, Chunya 58, Rungwe 55, Mbozi 45, Mbeya Vijijini asilimia 38 na wilaya ya Ileje asilimia 33.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...