MWIGULU NCHEMBA |
UWEZEKANO
wa bunge maalumu la Katiba kukaa kwa siku zingine 60 umeingia doa baada ya
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kusema kwamba hakubaliani na mapendekezo
hayo.
Aliyasema
hayo juzi wakati aakihutubia mamia ya wakazi wa manispaa ya Iringa na vitongoji
vyake katika mkutano uliopewa jina la Ondoa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.
Alisema
atapinga kwa nguvu zake zote bunge hilo kukutana kwa siku nyingine 60 kwasababu
ikifanyika hivyo itakuwa ni sawa na kutumia vibaya fedha za walipa kodi.
Pamoja
na kupinga bunge hilo kukutana kwa siku nyingine 60 alisema atamshauri Spika
wake amuandikie Rais barua ya kulivunja endapo watashindwa kuzitumia wiki mbili
za mwanzo kujadili mambo ya msingi katik rasimu hiyo.
Alisema
nchi imepoteza fedha nyingi katika awamu ya kwanza ya mjadala wa rasimu ya
katiba hiyo kwani kwa zaidi ya siku 40 walikuwa wakilumbana kuhusu kanuni na muundo
wa serikali.
Alisema
kuliko kuendelea kupoteza fedha kwa kuwalipa wabunge wanaolumbana kwa mambo
yanayojadilika ni bora fedha hizo zikapelekwa katika sekta zingine za
maendeleo.
Kuhusu uchumi
Katika
kuboresha uchumi wa nchi Mwigulu alisema; “Tunapeleka sheria ya kufuta misamaha
ya kodi; tunataka wakubwa na wadogo kwa pamoja walipe kodi; habari ya likizo ya
kodi haitakuwepo tena.”
Pamoja
na sheria hiyo kuahidi kupelekwa katika bunge hili bajeti, Mwigulu alisema
serikali itapeleka sheria nyingine ya kubana matumizi.
Alisema
kwa kupitia sheria hizo mapato ya serikali yataongezeka na kusaidia kuimarisha
uchumi wa nchi.
“Mapato
hayo yatatuweka katika mazingira ya kuboresha maslai ya watumishi wa umma
wakiwemo walimu na polisi,” alisema huku akisisitiza kwamba hilo linawezekana
kama mapato ya serikali yataimarika.
“Inawezekanaje mzazi mkulima asomeshe mtoto hadi kidato cha sita kwa mapato yanayotokana uuzaji wa vitumbua halafu serikali ikashindwa kumpatia mkopo kwa ajili ya elimu yake ya juu,” alisema.
Chanzo;bongo leaks
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni