Jumatano, 11 Juni 2014

WAKULIMA WADOGO WAASWA KEPUKA MATUMIZI YA KEMIKALI ZENYE ATHARI KWA MAZINGIRA NA AFYA.

Picha na 1Mshindi wa tuzo mbalimbali na mwanaharakati wa mazingira duniani Dkt.Vandana Shiva kutoka nchini India akisisitiza jambo kuhusu umuhimu wa wakulima wadogo ambao wanazalisha 70% ya chakula kinachotumiwa duniani kote walivyo na wajibu wa kuiepusha jamii na matumizi ya vyakula vinavyozalishwa na kuhifadhiwa na kemikali za viwandani zenye madhara kwa afya.Picha no 2Mkurugenzi wa Taasisi ya Kilimo Hai Tanzania Bw. Jordan Augustino (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa Tanzania katika mkutano wa kimataifa wa mwaka wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kilimo utakaofanyika June 12 katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es salaam ambapo washiriki wa mkutano huo watabadilishana uzoefu kuhusu mchango wa wakulima wadogo katika sekta ya kilimo.Picha no 3Mratibu wa Muungano huru wa watetezi wa Kilimo Hai na Chakula Salama Barani Afrika (AFSA) kutoka Ethiopia Dkt. Million Belay akiongea na waandishi wa habari kuhusu  umuhimu wa kilimo kinachoendana na mazingira halisi barani Afrika leo jijini Dar es salaamPicha no 4Mshindi wa tuzo mbalimbali na mwanaharakati wa mazingira duniani Dkt.Vandana Shiva kutoka nchini India akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kitabu kinachoelezea shughuli mbalimbali za binadamu zinavyoathiri uharibifu wa mazingira ya asili duniani. Kulia ni Muhamasishaji na mtetezi wa uhifadhi wa Mazingira kutoka Greenpeace Bw. Glen Tyler.Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
……………………………………………….
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Dar es salaam.
Wito umetolewa kwa wakulima wadogo kote nchini kuzingatia kilimo salama kinachohimiza matumizi ya mbolea za asili ili kupata mazao bora na salama kwa afya ya jamii na kuepuka kutumia kemikali zenye athari kwa uhifadhi wa mazingira.
Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es salaam mshindi wa tuzo mbalimbali na mwanaharakati wa mazingira duniani Dkt.Vandana Shiva kutoka nchini India amesema kuwa wakulima wadogo ambao wanazalisha 70% ya chakula kinachotumiwa duniani wanao wajibu wa kuiepusha jamii na matumizi ya vyakula vinavyozalishwa na kuhifadhiwa na kemikali za viwandani zenye madhara kwa afya.
Dkt. Vandana ambaye yuko nchini Tanzania kuungana na wadau wengine wa kutetea kilimo salama na rafiki wa mazingira wanaohudhuria  mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kilimo ameeleza kuwa yeye pamoja na wadau wengine wanaendelea kuhamasisha wakulima duniani kote kupitia programu zinazohimiza kilimo kinachoshabihiana na mazingira ya asili na uhifadhi wa mazingira kwa chakula salama barani Afrika.
Amesema kuwa yeye pamoja na wadau wengine wa Muungano huru wa watetezi wa Kilimo Hai na Chakula Salama Barani Afrika (AFSA) wanaamini kuwa chakula bora na salama ni kile kinachozalishwa kutokana na ardhi na si vinginevyo na kuongeza kuwa kilimo kinachohimiza matumizi ya mbegu na mbolea za viwandani licha ya kuwa na gharama kubwa za uzalishaji kina athari na madhara kwa afya na viumbe wengine wakiwemo nyuki na vipepeo.
“Ninao ushahidi wa kutosha unaoonesha madhara makubwa yanayotokana na matumizi ya madawa makali na kemikali za viwandani kwa afya ya binadamu na viumbe wengine wa asili ambayo kama tusipochukua tahadhari mapema dunia itakua si mahali salama pa kuishi” amesema.
Kwa upande wake Mratibu wa Muungano huru wa watetezi wa Kilimo Hai na Chakula Salama Barani Afrika (AFSA) kutoka Ethiopia Dkt. Million Belay amesisitiza kuwa kilimo kinachoendana na mazingira halisi ndicho kitakacholifanya bara la Afrika kujitosheleza kwa chakula.
 Amesema wao kama muungano na watetezi wa kilimo kinachozingatia uhifadhi wa mazingira wanaendelea kufanya tafiti mbalimbali na tayari baadhi ya nchi za Afrika zikiwemo Ghana,Ethiopia,Tanzania na Msumbiji zimechaguliwa katika mpango huo wenye lengo la kuwafanya wananchi wake kujitosheleza kwa chakula .
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Kilimo Hai Tanzania Bw. Jordan Augustino ameeleza kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano huo wa kimataifa utakaofanyika June 12 katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es salaam ambapo washiriki wa mkutano huo watabadilishana uzoefu kuhusu mchango wa wakulima wadogo katika sekta ya kilimo.

CHANZO FULL SHANGWE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...