KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA NDONYA SUGU (23)
MKAZI WA KIJIJI CHA MAFYEKO ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU
KATIKA ZAHANATI YA CHA BITIMANYANGA BAADA YA KUPIGWA FIMBO KICHWANI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.06.2014
MAJIRA YA SAA 02:30 USIKU KATIKA
KITONGOJI CHA ITAGA, KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA MAFYEKO, TARAFA YA
KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MAREHEMU ALIPIGWA FIMBO KICHWANI
TAREHE 01.06.2014 MAJIRA YA SAA 16:30 JIONI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA SHAGEMBE KUNAWIJI (54) MKAZI WA KIJIJI CHA BITIMANYANGA WAKATI
WANACHEZA NGOMA ZA KABILA LA KISUKUMA MAARUFU KWA JINA LA CHAGULAGA KIJIJINI
HAPO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
WATU WAWILI
WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.163 ATQ AINA YA TOYOTA HAICE LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA GODFREY AWDHI NGOLE (32) MKAZI WA IGURUSI KUACHA NJIA NA
KISHA KUPINDUKA KATIKA ENEO LA MAMBI WILAYA YA MBARALI.
ABIRIA MMOJA
KATI YA WAWILI ALITAMBULIKA KWA JINA LA ELIZABETH
MKARAWE (30) MKAZI WA IGURUSI NA
2. MSICHANA MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA
JINA WALA MAKAZI WALIFARIKI DUNIA. AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 02.06.2014 MAJIRA YA SAA 11:50 ASUBUHI KATIKA ENEO LA MAMBI,
KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA
BARABARA YA MBEYA/NJOMBE.
AIDHA KATIKA
TUKIO HILO WATU SABA WALIJERUHIWA KATI YAO WANAUME WATATU NA WANAWAKE WAWILI
AKIWEMO DEREVA WA GARI HILO.CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MIILI YA MAREHEMU
NA MAJERUHI WAPO HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA
ASKARI WA NAKONDE NCHINI ZAMBIA LINAMSHIKILIA JAMBAZI MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA JIMMY NYILENDA RAIA WA
ZAMBIA BAADA YA KUJERUHIWA KWA KUPIGWA
RISASI KATIKA JARIBIO LA UNYANG’ANYI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.06.2014 MAJIRA YA SAA 17:45
JIONI KATIKA ENEO LA MPAKANI KATI YA TANZANIA NA ZAMBIA [TUNDUMA/NAKONDE].
INADAIWA KUWA WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WALIFYATUA RISASI OVYO KWA
LENGO LA KUWAPORA PESA WABADILISHAJI FEDHA WA ENEO HILO NA POLISI WA TUNDUMA
[TANZANIA] NA NAKONDE [ZAMBIA] WALIKABILIANA NA MAJAMBAZI HAO. KATIKA
MAJIBIZANO HAYO, MAJAMBAZI WATATU WALIUAWA WAWILI WAKIFAHAMIKA KUWA NI SIKAPWITE BONIPHACE
MFANYAKAZI WA COUNCIL NAKONDE RAIA WA ZAMBIA NA CHAPWA KIPAKWA RAIA NA MKAZI WA ZAMBIA NA MWINGINE HAKUWEZA KUFAHAMIKA.
AIDHA MAJAMBAZI WENGINE WALIWEZA KUKIMBIA NA JAMBAZI
MMOJA JIMMY NYILENDA RAIA WA ZAMBIA
AMEKAMATWA AKIWA MAHUTUTI BAADA YA KUJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI.
KATIKA TUKIO HILO SILAHA MBILI AINA YA AK-47 ZENYE NAMBA 625562 NA 1963EC58
ZILIKAMATWA. HATA HIVYO KATIKA MAJIBIZANO HAYO RAIA WAWILI WA NAKONDE –ZAMBIA
WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA.HAKUNA MADHARA KWA ASKARI NA
SILAHA ZIPO POLISI NAKONDE ZAMBIA. JUHUDI ZA KUWATAFUTA MAJAMBAZI WALIOKIMBIA
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA HAO WA TUKIO
LA UJAMBAZI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUWA MAKINI KWA
KUCHUKUA TAHADHARI KATIKA KAZI ZAO.
KATIKA
MSAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA
ASKARI WANYAMAPORI TANAPA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMOS NAIMWA (30) MKAZI WA KIJIJI CHA
UTURO AKIWA NA SILAHA/BUNDUKI MOJA AINA YA GOBOLE NA GOROLI 12 BILA KIBALI.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 31.05.2014 MAJIRA YA SAA 12:00
MCHANA KATIKA KIJIJI NA KATA YA
ULANGA, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA
YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU, TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE
WAFUATE TARTIBU ZA UMILIKAJI SILAHA KIHALALI
ILI KUEPUKA MATATIZO.
Imesainiwa
na:
[AHMED Z.
MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni