Jumatano, 7 Mei 2014

MZEE MIAKA 70, AFARIKI BAADA YA KUMWAGIWA MAJI YA MOTO

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi.

MZEE WA MIAKA 70 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FOLO MWALUSEPO MKAZI WA KIJIJI CHA IGUNDU WILAYA YA CHUNYA ALIKUTWA AMEUAWA   KWA KUMWAGIWA MAJI YA MOTO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA NYUMBANI KWAKE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 06.05.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA ISOKO, KIJIJI CHA IGUNDU, KATA NA TARAFA YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILI KINACHUNGUZWA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

KUMEKUCHA MICHEZO YA UMISETA MBEYA

 Mwalimu wa mchezo wa Netiboli kutoka Sekondaraia ya Sangu, Zahara Shabani, akipanga kikosi cha timu yake kabla ya  kuvaa na  timu ya Sekondari ya wasichana ya Lolezi.

Mchezo huo uliofanyika katika viwanja Cathoric Youth Center jiji Mbeya.
Wanafunzi kutoka Sekondari ya wasaichana ya Loloza ya jiji Mbeya, wakifuatilia kwa makini mchezo wa Netiboli baina ya timu ya shule yao, ilikuwa ikimenyana na timu ya wasichana ya Sangu.

Katika mchezo wa fainali za Umiseta  kundi ‘C’ kutoka sekondari za jiji la Mbeya na Sangu walifanikiwa kuwa mabingwa katika kundi hilo baada ya kuifunga Loleza kwa jumla ya magoli 16 –14, mchezo huo ulipigwa juzi katika viwanja vya Cathoric Youth Center.

 (Picha na Kenneth Ngelesi)

Jumanne, 6 Mei 2014

WATEMBEA KILOMITA 30 KUSAKA MASOMO YA SEKONDARI

DIWANI WA KATA YA MASOKO WILAYA YA MBEYA, EDWARD MWAMPAMBA.
WAKATI Serikali ikijivunia mafanikio ya kujenga sekondari kila kata nchi nzima, wanafunzi wa kata ya Masoko wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa, wanalazimika kutembea kilomita 30 kutoka kwenye kata yao kwenda kusoma masomo ya sekondari.

Uchunguzi uliofanywa, umebani uwepo wa wanafunzi 205 ambao wanatoka katika kata hiyo na kwenda kusoma katika shule ya Sekondari ya Shisyete.

Baadhi ya wanafunzi waliohojiwa kuhusu umbali huo, walisema kuwa ni hatari kwa wanafunzi wa kike hasa kipindi cha masika ambacho kuna maeneo kunakuwa na vichaka vya nyasi nyingi.

Katika kata hiyo ya Masoko, majengo ya Sekondari yapo na yamekamilika.

Diwani wa kata hiyo, Edward Mwampamba(Chadema), alipohojiwa kuhusu hali ya wanafunzi kwenda umbali mrefu kusaka elimu ya sekodari, alikiri kuwepo kwa hali hiyo na kueleza baadhi ya changamoto zinazosababisha shule ya Sekondari ya kata yake kutofunguliwa.

“Majengo yote yamekamilika na wakaguzi walikuja kukagua, lakini kikwazo walisema lazima tukamilishe jengo la utawala kuwa na Siringboad, milango, samani, nyumba ya mwalimu na choo’’ alisema Mwampamba.

Hata hivyo ameiomba serikali kufanya jitihada za makusudi kuifungua shule hiyo ifikapo Januari mwakani, ili kuepusha adha waipatayo wanafunzi wanaotoka katika kata hiyo, ambao alisema mbali na kutembea umbali mrefu, ndiyo wanafunzi wanaoongoza kwa ufaulu katika shule ya Sekondari ya Shisyete.

RAIS KIKWETE AUNDA TUME KUCHUNGUZA OPERESHENI TOKOMEZA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameunda Tume ya Uchunguzi (Commission Inquiry) Kuhusu Vitendo vilivyotokana na Uendeshaji wa Operesheni Tokomeza. 
 
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam jioni ya Ijumaa, Mei 2, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Rais ameunda Tume hiyo kwa mujibu wa kifungu cha tatu cha Sheria ya Uchunguzi Sura ya 32.
 
 
Kutokana na hatua yake ya kuunda Tume hiyo, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji na Balozi Mstaafu Hamisi Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
 
 
Aidha, Rais Kikwete amewateua Mheshimiwa Jaji Mstaafu Stephen Ernest Mtashiwa Ihema na Mheshimiwa Jaji Mstaafu Vincent Kitubio Damian Lyimo kuwa Makamishna. 
 
 
Rais pia amemteua Ndugu Frederick Manyanda, Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa Katibu wa Tume hiyo.

Taarifa ya Balozi Sefue inasema kuwa uteuzi huu ulianza jana, Alhamisi, Mei Mosi 2014.
 
 
Taarifa ya Balozi Sefue iliyataja majukumu ya Tume hiyo yatakuwa yafuatayo:
Kuchunguza na kubaini Operesheni Tokomeza ilivyoendeshwa.


Kuchunguza na kubaini iwapo Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu za Rejea zilifuatwa na watu waliotekeleza Operesheni Tokomeza.


Kuchunguza na kubaini iwapo yupo mtu yeyote aliyekiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea wakati wa Operesheni Tokomeza.


Kuchunguza na kubaini kama wapo watu wowote waliokiuka Sheria yoyote wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na kupima kama hatua zilizochukuliwa dhidi yao au mali zao zilikuwa stahiki.


Kupendekeza hatua zozote zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea za Operesheni Tokomeza.
 
 
Kupendekeza mambo ya kuzingatiwa wakati wa kuandaa na kutekeleza operesheni nyingine siku zijazo ili kuepuka kasoro.


Uteuzi huo wa Tume hiyo unatekeleza ahadi ya Rais Kikwete ambayo aliitoa wakati anahutubia Bunge Novemba 18, mwaka jana, 2013 mjini Dodoma.


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

MILA NA DESTURI, KIKWAZO WANAUME KUSHIRIKI AFYA YA UZAZI



MILA na desturi ni kikwazo moja wapo kinachokwamisha malengo ya milenia ya kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kufikia asilimia 75 kati ya vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2015.

Kwa mujibu wa utafiti wa masuala ya afya ya uzazi ya Tanzania ya serikali mwaka 2010(TDHS), unaeleza kuwa kila siku wajawazito 23 wanapoteza maisha kwa matatizo mbalimbali ya uzazi wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua.

Baadhi ya wanaume wana mawazo ya kimazoea kuwa kuongozena na wake zao Kliniki ni kama wamelishwa dawa za kupumbazwa(Limbwata).

Wanaume wengi wanasema kuwa kuongozana na wake zao kwenda Kiliniki si utamaduni wao.

Katika utafiti niliofanya kwa miezi sita katika mikoa kadhaa hapa nchini chini, imebainika kuwa bado hali hiyo ipo ingawa baadhi ya wanaume wameanza kuelimika na kushiriki pamoja na wenza wao kwenda sehemu za kutolea huduma za afya za kitaalam.

Katika wilaya ya Ileje mkoani Mbeya kijana Henry Kayuni anasema kuwa kutokana na mila za kabila la Wandali wanaume walikuwa hawaendi na wake zao Kliniki lakini kwa sasa akiwemo yeye anaongozana na mkewe ikiwa ni pamoja na kumpeleka mtoto Kliniki.

‘’Nilifanya hivyo tangu wakati wa mimba kwa ajili ya kujua afya zetu kwa pamoja hasa ugonjwa wa Ukimwi.’’ Anasema Kayuni.

Kijana Samson James mkazi wa Kijiji cha Kambubu wilaya ya Bunda mkoani Mara, anasema

Mila na desturi, kikwazo cha wanaume kushiriki afya ya uzazi Tanzania

April 25th, 2013 | by Gordon Kalulunga
MILA na desturi ni kikwazo moja wapo kinachokwamisha malengo ya milenia ya kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kufikia asilimia 75 kati ya vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2015.

Kwa mujibu wa utafiti wa masuala ya afya ya uzazi ya Tanzania ya serikali mwaka 2010(TDHS), unaeleza kuwa kila siku wajawazito 23 wanapoteza maisha kwa matatizo mbalimbali ya uzazi wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua.
Baadhi ya wanaume wana mawazo ya kimazoea kuwa kuongozena na wake zao Kliniki ni kama wamelishwa dawa za kupumbazwa(Limbwata).
Wanaume wengi wanasema kuwa kuongozana na wake zao kwenda Kiliniki si utamaduni wao.
Katika utafiti niliofanya kwa miezi sita katika mikoa kadhaa hapa nchini chini, imebainika kuwa bado hali hiyo ipo ingawa baadhi ya wanaume wameanza kuelimika na kushiriki pamoja na wenza wao kwenda sehemu za kutolea huduma za afya za kitaalam.
Katika wilaya ya Ileje mkoani Mbeya kijana Henry Kayuni anasema kuwa kutokana na mila za kabila la Wandali wanaume walikuwa hawaendi na wake zao Kliniki lakini kwa sasa akiwemo yeye anaongozana na mkewe ikiwa ni pamoja na kumpeleka mtoto Kliniki.
‘’Nilifanya hivyo tangu wakati wa mimba kwa ajili ya kujua afya zetu kwa pamoja hasa ugonjwa wa Ukimwi.’’ Anasema Kayuni.
Kijana Samson James mkazi wa Kijiji cha Kambubu wilaya ya Bunda mkoani Mara, anasema kuwa yeye ni mmoja kati ya vijana wanaojisikia vizuri kuongozana na mkewe kwenda Kliniki.
Anasema mbali na mwitikio huo, lakini kikwazo ni huduma duni wanazozipata hasa katika kituo cha afya cha Ikizu maarufu kwa jina la Nyamuswa.
‘’Tunaongozana na wenza wetu lakini tatizo ni huduma bora ambapo hata katika magonjwa ya kawaida tunapata vipimo tu, lakini dawa huwa tunanunua maduka ya dawa na endapo katika maduka ya dawa kungekuwa na vipimo tusingethubutu kwenda huko’’ anasema Samsoni.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Kambubu Warioba Kiharata anasema kuongozana na mkewe kwenda hospitali siyo shida bali tatizo ni kupata huduma bora za afya hasa kwa wajawazito na watoto chini ya miaka mitano ambapo kwa masikini ni tatizo!.
‘’Wananchi wengi hasa vijana wanahamasika kwenda na wake zao Hospitali hasa wakati wa kujifungua na malezi ya watoto, shida ni majibu yasiyoridhisha kutoka kwa wataalam wa afya, ukiwaambia kuwa wakusaidie mkeo anaumwa wanakuuliza kuwa sasa wao wafanyeje!’’ anasema Kiharata.
Anasema kutokana na hali hiyo, wananchi wa kijiji chao wamehamasishana kujenga zahanati ya kijiji na tayari wamekusanya mchanga na mawe.
‘’Kwa sasa katika kijiji chetu tunasubiri kibali cha kujenga zahanati ambapo wanaotukwamisha ni serikali hawataki kutupa ramani’’ anasema Mwenyekiti huyo.
Mjamzito Agnes Baraka anakiri kuwa wanashirikiana na mumewe katika kulea mimba na kushiriki kumpeleka hospitalini lakini anasema kuwa endapo mimba hiyo haitakuwa na matatizo atajifungulia nyumbani au kwa mkunga wa jadi kutokana na hospitali kutokuwa na huduma bora.
Naye Anna Japhet(35) anasema kuwa wakunga wa jadi wanatoa huduma bure na wale wanaotoza fedha ni Sh. 3,000 tofauti na hospitalini ambako mjamzito analazimika kununua karatasi, gharama za kitanda, na mafuta ya taa 1,000 jambo ambalo kutokana na uchumi wake anaona anamtesa mumewe.
Msaidizi wa mganga wa zahanati ya Bunda mkoani humo, Victoria Awino anasema kuwa katika zahanati hiyo ili kuhamasisha wanaume kushiriki katika afya ya uzazi wanawapa kipaumbele zaidi wajawazito wanaoenda na wenza wao.
‘’Mjamzito anayekuja na mumewe ndiye tunaanza kumuhudumia kisha tunaendelea na wengine ambao hawaji na waume zao’’ anasema Victoria.
Anasema kuwa baada ya kufanya hivyo, wanawake wengi wamekuwa wakijitokeza na waume zao kwenda kupata huduma za Kliniki kabla, wakati na baada ya kujifungua.
Anasema kwa sasa zahanati hiyo inahudumia wagonjwa kati ya 30 mpaka 40 kwa siku.
Mjamzito Nyangeta Makori mkazi wa kijiji cha Nyambono wilaya ya Musoma vijijini, kutokana na usafiri unaofaa kwa mjamzito kutokuwepo, alilazimika kukodi pikipiki na mumewe na kupita katika barabara mbovu kwa saa nne, huku akisikilizia uchungu kutoka Msoma vijijini mpaka Kituo cha afya cha Manyamanyama wilaya ya Bunda.
Alitoka saa 8;30 nyumbani kwake na kufika saa 11:30 jioni kisha kupokelewa katika kituo cha afya cha Manyamanyama, baada ya muda wa saa moja alijifungua mapacha, Doto akiwa na kilo 3.1 na Kulwa naye ana kilo 3.5.
Nyangeta anasema huo ni uzao wake wa tano ana watoto sita wote wakiume, watoto wa nne amejifungulia nyumbani akisaidiwa na wifi yake kwa kumshika sehemu ya mgongo wakati wa kujifungua na yeye kusukuma na kujifungua mtoto.
Kitu kinachosababisha Nyangeta kuzalia nyumbani watoto wanne ni kijiji anachokaa hakuna zahanati na hospitali iko mbali.
Wifi yake Nyangeta ambaye tunaweza kumwita shujaa, amemuokoa Nyangeta asipoteze maisha kwa kumshawishi kwenda katika kituo cha afya kujifungua pamoja na kumsindikiza kutoka musoma vijijini mpaka Bunda, lakini pia ndiye mwanamke aliyemsaidia kujifungua nyumbani watoto wanne.
Huyo ni mmoja wa wajawazito Tanzania wanaokumbana na shida wakati wa kutafuta huduma za kujifungua ikiwa pamoja na umbali, usafiri usio wa uhakika, umasikini na barabara mbovu.
Endapo mumewe hasingeweza kumkodia pikipiki hueda angefariki maana awali anasema alipohudhuria Kliniki aliambiwa mimba yake inamatatizo na alikuwa akiugua tofauti na mimba zilizopita.
Katika wilaya za Butiama na Musoma Mjini mkoa wa Mara, wajawazito wanapokwenda kliniki wanachangia huduma za upimaji kama kupima wingi wa damu wanalipia shilingi 1,000, kadi la kliniki wananunua shilingi 1,000.
Tatizo la kuchangia huduma kwa wajawazito kinyume na sera ya afya ya mwaka 2007 inayosema kuwa wajawazito watapata huduma bure, pia lipo katika wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi, idadi ni kubwa ya wajawazito lakini wanakosa huduma bora ya kujifungua.
Pia katika wilaya ya Songea mkoa wa Ruvuma hali sio nzuri katika upatikanaji wa huduma za kliniki, katika zahanati ya Ifinga kwenye kijiji cha Ifinga wajawazito wanachangia huduma mbalimbali za kliniki, kupima ujauzito wanalipia shilingi 2,000, kupima wingi wa damu wnalipa shilingi 1500.
Kama mjamzito damu yake ni pungufu hupewa dawa za kuongeza damu kwa malipo ya shilingi 1,000.
Kwa upande wake ofisa mradi mwandamizi mawasiliano mradi wa CHAMPION Muganyizi Mutta, alipokuwa akitoa mada kwa baadhi ya waandishi wa habari mkoani Mbeya zinazolenga kushirikisha wanaume katika mapambano dhidi ya maambukizi ya (VVU), anasema kuwa ni vema wanaume wakajua haki za kushiriki Kliniki na wenza wao.
Mutta anasema mradi huo ni mradi wa kwanza Tanzania unaolenga kushirikisha wanaume katika mapambano chanya dhidi ya maambukizi ya VVU.
Anasema kinachokwamisha baadhi ya wanaume kushiriki katika huduma za afya na kwenda hospitalini na wake au wenza wao ni pamoja na mila na desturi zinazoeleza kuwa jukumu la kutunza mimba na kulea mtoto ni la mwanamke.
"Mbali na hilo pia kuna mitazamo ya kimazoea Stereotype ambapo mwanaume kwenda na mkewe kliniki jamii inamshangaa, hivyo umefika wakati jamii ibadilike na kuona suala la mimba kabla na baada ya kujifungua ni jukumu la wote yaani mwanamke na mwanaume'' anasema Mutta.
Mradi huo unasimamiwa na shirika la EngenderHealth na shirika mwenza linalojulikana kwa jina la FHI360 na kufadhiliwa na USAID ambapo wanaifikia jamii hasa wanaume kwa njia mbalibali ikiwemo mwanaume mmojammoja, mikusanyiko (jamii) na maeneo ya kazi.
Kupitia makala hii, ili jamii iweze kuepukana na ongezeko la VVU inapaswa elimu iwafikie kikamilifu wanaume wenye umri wa kuingia kwenye ndoa na walioko kwenye ndoa.
Lengo likiwa ni kujua umhumi wa kabla ya kupanga kuzaa watoto, wanandoa waweze kufika katika vituo vya afya na hospitali kupima afya zao ili hata kama watakuwa wameambukizwa au mmoja wao waweze kupata mbinu ya kutomwambukiza mtoto anayetarajiwa kuzaliwa.
Vipimo vinavyopimwa kwa mjamzito siku za kwanza ni pamoja na VVU, kipimo cha wingi wa damu (HB test), maambukizi ya kaswende na gonorea (VDRL test) na mfumo wa mkojo.
Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa simu 0754 440749 na Barua pepe;kalulunga2006@yahoo.com
- See more at: http://www.jamiiforums.com/blog/mila-na-desturi-kikwazo-cha-wanaume-kushiriki-afya-ya-uzazi-tanzania/#sthash.41BwWG2D.dpuf

Jumapili, 4 Mei 2014

WANAFUNZI MZUMBE WAFA MAJI WAKIOGELEA

WANAFUNZI wawili waliokuwa wakisoma katika Chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya, wamekufa maji wakati wanaogelea na mitumbwi katika bwawa la samaki lililopo katika hifadhi (zoo)ya wanyama Ifisi inayomilikiwa na kanisa la Uinjilisti Tanzania, Mbeya Vijijini.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Jackob Mwakasole, alisema tukio hilo lilitokea Mei 2, mwaka huu katika eneo hilo na kuleta simanzi kubwa.
 
Alisema madimbwi hayo ni maalum kwa ajili ya kuhifadhi samaki na maji ya mvua kwa ajili ya wanyama wanaotunzwa katika eneo hilo, lakini ajabu wanafunzi hao waliingia na kuanza kuogelea.
 
“Tumepata simanzi kubwa, kwasababu bwawa walilojitosa kuogelea ni kwa ajili ya kufugia samaki na maji ya wanyama. Ni maji ambayo kwa akili ya kawaida mtu mzima hawezi kuingia kuogelea, tulifanya jitihada za kuopoa miili kwa kuanza kupunguza maji kwa mashine tukishirikiana na Mkurugenzi wetu Mch.Marcus Lehner, vijana wanaojua kuogelea na kuzamia, askari polisi na wasamaria wema wengine ’’ alisema Mwakasole.
 
Alipoulizwa kuwa ilikuwaje marehemu waliruhusiwa kuingia katika bwawa hilo, alisema katika eneo hilo kuna mitumbwi midogo kwa ajili ya kuvulia samaki na kupiga picha, lakini walimshawishi mtumishi mmoja wa hifadhi hiyo kuwa wao walikuwa na utaalam, jambo ambalo kumbe halikuwa sahihi.
 
“Walikuwa na mabinti kadhaa, tulikuta eneo la tukio mabaki ya vinywaji kama Juice na karatasi za pombe kali na baadhi ya wanafunzi waliokuwa nao pia tuliwakuta eneo hilo’’ alisema Mwakasole.
 
Kwa upande wa Jeshi la polisi mkoani Mbeya, Kamanda wa polisi Ahmed Msangi, aliwataja marehemu kuwa ni Michael Tarimo(20), Albert Shenkalwa(23) na kwamba wanafunzi hao walikuwa mwaka wa kwanza katika chuo hicho wakisomea uongozi wa biashara ngazi ya Stashahada.
 
“Walikuwa 12, walikwenda picknic kwa ajili ya kuangalia wanyama, baadaye kwenda kwenye bwawa linalotunza samaki na kuingia kwenye maji kwa zamu na mitumbwi, Mtumbwi waliokuwa wakiutumia ukapinduka na wao kushindwa kuogelea’’ alisema Kamanda Msangi.
 
Mwandishi wa habari hizi alifika eneo la chuo hicho na kuwakuta wanafunzi wakiwa na huzuni huku wakiwa wamavaa mavazi ya staha kuliko siku zingine zote.
 

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...