DIWANI WA KATA YA MASOKO WILAYA YA MBEYA, EDWARD MWAMPAMBA.
WAKATI
Serikali ikijivunia mafanikio ya kujenga sekondari kila kata nchi nzima,
wanafunzi wa kata ya Masoko wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa, wanalazimika
kutembea kilomita 30 kutoka kwenye kata yao kwenda kusoma masomo ya sekondari.
Uchunguzi
uliofanywa, umebani uwepo wa wanafunzi 205 ambao wanatoka
katika kata hiyo na kwenda kusoma katika shule ya Sekondari ya Shisyete.
Baadhi ya
wanafunzi waliohojiwa kuhusu umbali huo, walisema kuwa ni hatari kwa wanafunzi
wa kike hasa kipindi cha masika ambacho kuna maeneo kunakuwa na vichaka vya nyasi
nyingi.
Katika kata
hiyo ya Masoko, majengo ya Sekondari yapo na yamekamilika.
Diwani wa
kata hiyo, Edward Mwampamba(Chadema), alipohojiwa kuhusu hali ya wanafunzi kwenda umbali
mrefu kusaka elimu ya sekodari, alikiri kuwepo kwa hali hiyo na kueleza baadhi
ya changamoto zinazosababisha shule ya Sekondari ya kata yake kutofunguliwa.
“Majengo
yote yamekamilika na wakaguzi walikuja kukagua, lakini kikwazo walisema lazima
tukamilishe jengo la utawala kuwa na Siringboad, milango, samani, nyumba ya
mwalimu na choo’’ alisema Mwampamba.
Hata hivyo ameiomba
serikali kufanya jitihada za makusudi kuifungua shule hiyo ifikapo Januari
mwakani, ili kuepusha adha waipatayo wanafunzi wanaotoka katika kata hiyo,
ambao alisema mbali na kutembea umbali mrefu, ndiyo wanafunzi wanaoongoza kwa
ufaulu katika shule ya Sekondari ya Shisyete.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni