WANAFUNZI
wawili waliokuwa wakisoma katika Chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya, wamekufa
maji wakati wanaogelea na mitumbwi katika bwawa la samaki lililopo katika
hifadhi (zoo)ya wanyama Ifisi inayomilikiwa na kanisa la Uinjilisti Tanzania,
Mbeya Vijijini.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana ofisini kwake, Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Jackob Mwakasole,
alisema tukio hilo lilitokea Mei 2, mwaka huu katika eneo hilo na kuleta
simanzi kubwa.
Alisema madimbwi
hayo ni maalum kwa ajili ya kuhifadhi samaki na maji ya mvua kwa ajili ya
wanyama wanaotunzwa katika eneo hilo, lakini ajabu wanafunzi hao waliingia na
kuanza kuogelea.
“Tumepata
simanzi kubwa, kwasababu bwawa walilojitosa kuogelea ni kwa ajili ya kufugia
samaki na maji ya wanyama. Ni maji ambayo kwa akili ya kawaida mtu mzima hawezi
kuingia kuogelea, tulifanya jitihada za kuopoa miili kwa kuanza kupunguza maji
kwa mashine tukishirikiana na Mkurugenzi wetu Mch.Marcus Lehner, vijana
wanaojua kuogelea na kuzamia, askari polisi na wasamaria wema wengine ’’
alisema Mwakasole.
Alipoulizwa kuwa
ilikuwaje marehemu waliruhusiwa kuingia katika bwawa hilo, alisema katika eneo
hilo kuna mitumbwi midogo kwa ajili ya kuvulia samaki na kupiga picha, lakini
walimshawishi mtumishi mmoja wa hifadhi hiyo kuwa wao walikuwa na utaalam,
jambo ambalo kumbe halikuwa sahihi.
“Walikuwa na
mabinti kadhaa, tulikuta eneo la tukio mabaki ya vinywaji kama Juice na karatasi
za pombe kali na baadhi ya wanafunzi waliokuwa nao pia tuliwakuta eneo hilo’’
alisema Mwakasole.
Kwa upande
wa Jeshi la polisi mkoani Mbeya, Kamanda wa polisi Ahmed Msangi, aliwataja
marehemu kuwa ni Michael Tarimo(20), Albert Shenkalwa(23) na kwamba wanafunzi
hao walikuwa mwaka wa kwanza katika chuo hicho wakisomea uongozi wa biashara
ngazi ya Stashahada.
“Walikuwa
12, walikwenda picknic kwa ajili ya kuangalia wanyama, baadaye kwenda kwenye
bwawa linalotunza samaki na kuingia kwenye maji kwa zamu na mitumbwi, Mtumbwi
waliokuwa wakiutumia ukapinduka na wao kushindwa kuogelea’’ alisema Kamanda
Msangi.
Mwandishi wa
habari hizi alifika eneo la chuo hicho na kuwakuta wanafunzi wakiwa na huzuni
huku wakiwa wamavaa mavazi ya staha kuliko siku zingine zote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni