Jumanne, 9 Desemba 2014

WAZIRI NYALANDU AKANUSHA UVUMI WA WAKAZI WA LOLIONDO KUTAKA KUONDOLEWA

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akitoka nje ya nyumba ya kimasai alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Wamasai waliokusanyika kwa ajili ya kusikia tamko la serikali juu ya uvumi wa kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Wamasai wakichukua kumbukumbu muhimu katika mkutano wao na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake wa jamii ya kimasai mara baada ya kumaliza mkutano nao.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Raphael Rong’oi akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu (aliyekaa kwenye pikipiki). 
 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu, amesema habari zinazodai kuwa Serikali inataka kuwaondoa wakazi wa zaidi ya 40,000 katika eneo la Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha  hazina ukweli wowote.

Novemba mwaka huu, gazeti The Guardian la nchini Uingereza, liliandika habari kuwa serikali ina mpango wa kuwafukuza Wamasai wanaoishi eneo hilo.

Gazeti hilo lilidai kuwa, lengo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu.

Akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai wilayani Ngorongoro mwishoni mwa wiki, Nyalandu alisema habari hizo hazina ukweli wowote isipokuwa zina lengo la kuchafua taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa.

Aliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi bila hofu, kwa sababu serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye makazi yao.

“Nami niwahakikishie wanajamii wa Loliondo, Ngorongoro na wanajamii wote wa kimasai ambao wametishiwa nyau, kuwa serikali ya Tanzania haina mpango wowote wa kumfuata na kumfukuza mtu yoyote,” alisema.
 
Credit.matukio-michuzi
 
 

Jumamosi, 6 Desemba 2014

WAZIRI ZAMBI, ATENGUA ZUIO LA MRAJIS UUZWAJI SHAMBA LA GARARAGUA


  Hatimaye Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,Godfrey Zambi,ametoa ruhusa ya kuuzwa mara moja  shamba kubwa la kahawa la Gararagua mali ya Chama Kikuu cha ushirika mkoani Kilimanjaro(KNCU). 


Hatua hiyo imekuja siku chake baada ya ofisi ya Mrajis wa vyama vya ushirika nchini kuzuia uuzwaji wa shamba hilo ikishinikiza kuondolewa kwa Bodi ya wakurugenzi ya KNCU  hatua ambayo iliibua malumbano makali baina yake na bodi ya chama hicho.

Akizungumza wiki hii katika mkutano Mkuu maalumu,Zambi alisema ofisi ya mrajis haina mamlaka kisheria ya kuiondoa bodi ya KNCU na kwamba mwenye mamlaka hayo ni wanachama ambao oktoba 22 mwaka huu walipiga kura na kuridhia bodi hiyo kuendelea kuwapo madarakani.

Waziri Zambi alisema kuwa,shamba hilo litauzwa kwa uwazi baada ya kufanyika kwa tathimini ya thamani halisi ya shamba hilo na kwamba kitaundwa chombo kitakachosimamia uuzwaji huo ili kukiwezesha kuondokana na mzigo wa madeni unaokiandama likiwamo deni kubwa la benki ya CRDB .

Awali ofisi ya  mrajis wa vyama vya ushirika nchini,licha ya kuchelewa kutoa kibali cha kuuzwa kwa shamba hilo,ilitoa masharti ikitaka bodi ya sasa ya KNCU iondoke madarakani na shamba hilo liuzwe chini ya bodi mpya hatua ambayo ilisababisha malumbano makali.

Kutokana na masharti hayo, KNCU iliandika barua ya malalamiko kwa waziri mwenye dhamana na ushirika  wakidai kuwa masharti hayo yanaendelea kukiumiza chama hicho kwa kuendelea kulipa mamilioni ya fedha kwa CRDB kama riba.

Katika taarifa yake kwa wajumbe wa mkutano huo mkuu maalumu,mwenyekiti wa chama hicho,Maynard Swai alimweleza waziri Zambi kuwa,hatua hiyo ya mrajis kuzuia uuzwaji wa shamba hilo ni kuleta machafuko kwa chama hicho na kuua ushirika.

Chama hicho kinamiliki mashamba makubwa manne ambayo ni Gararagua, Lerongo,Lyamungo na Molomo na kati ya hayo matatu yamekodishwa kwa wawekezaji wazalendo huku moja likitarajiwa kutumika kwa shughuli za uzalishaji wa miche bora ya kahawa na  kuwa shamba darasa.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo,chama hicho kinakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo kuyumba kwa bei ya kahawa kwenye soko la dunia,mbinu chafu za kibiashara kutoka kwa wapinzani wake.

Aliainisha changamoto nyingine kuwa ni kuwapo kwa ushawishi mbaya wa kisiasa wenye nia ya kukivuruga chama hicho pamoja na mzigo mkubwa wa madeni kuanzia msimu wa 2003/2004 hadi hivi sasa.
 
 

Jumatatu, 1 Desemba 2014

MAHAFARI YA 12 YA TIA MBEYA YAFANA, WAHITIMU NA WAHADHIRI WAPEWA SOMO.


Brass band ikiongoza maandamano






Vikundi mbalimbali vya ngoma vilitumbuiza katika Mahafali hiyo





WAHADHIRI wa Vyuo mbali mbali nchini wametakiwa kutoa elimu kwa wanafunzi kulingana na soko la ajira ikiwa ni pamoja na fani inayoendana na cheti alichopata ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Profesa Norman Sigalla, alipokuwa amemwakilisha Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, katika mahafali ya 12 ya Taasisi ya Uhasibu (TIA)Kampasi ya Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya taasisi hiyo mjini hapa.
Profesa Sigalla alisema hivi sasa kuna ushindani wa vyuo na ukosefu wa ajira nchini hivyo I vema wahadhiri wakatoa wanafunzi wenye sifa kulingana na vyeti wanavyopata ili kukidhi soko la ajira ikiwa ni pamoja na kujiajiri wenyewe na sio kusubiri kuajiriwa.
“ kutokana na ongezeko la vyuo na ushindani uliopo ni vema wahadhili wakatoa wahitimu wenye sifa za kipekee kuendana na aina ya cheti alichopata na kukabiliana na soko la ajira” alisema Profesa Sigalla.
Aliongeza kuwa wajibu wa vyuo ni kuandaa watalaam mbali mbali ili waweze kutumikia taifa na kukidhi haja ya nchi katika kujiletea maendeleo kwa wahitimu kufuata walitofundishwa madarasani na kutumia taaluma yao kupambana na changamoto zilizopo uraiani.
Alisema ni vema wahitimu kutokana na elimu waliyoipata wakaangalia fursa zilizopo nchini wakazitumia vizuri badala ya kusubiri kuajiriwa na serikali kutokana na mfumo uliopo wa kutoa ajira kwa kila mtu kuwa mgumu baada ya wahitimu kuongezeka kila kukicha.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji mkuu wa Tasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) Dk. Joseph Kihanda,alisema katika mwaka wa masomo 2013/2014 jumla ya wanafunzi 1960 wakiwemo wanawake 947 na wanaume 1013 wamehitimu katika fani za cheti cha awali, Stashahada na stashahada ya uzamili katika kampasi ya Mbeya.
Alisema Chuo hicho kinakabiliwa na Changamoto za kudumu na mpya ambazo ni uhaba wa majengo kama vile kumbi za mhadhara, maktaba za kisasa na vitabu, ofisi za wafanyakazi na nyumba za wafanyakazi na wahadhiri pamoja na upungufu wa thamani.
Aliongeza kuwa changamoto mpya zinazokikabili chuo hicho ni pamoja na uwiano wa wahadhirina wanafunzi kutokuwa mzuri kutokana na ongezeko kubwa la udahili kutokana na ajira ya wahadhiri kusimamiwa na Serikali kuu hivyo kushindwa kupata wahadhiri wanaoweza kuendana na idadi wa wanafunzi  ambapo hivi sasa chuo kina wahadhiri 19.
Dk Kihanda aliongeza kuwa Changamoto  nyingine ni upatikanaji wa maji katika Kampasi ya Mbeya kuwa ni wa kusuasua hivyo kuhatarisha afya za wanafunzi kunakoweza kusababishwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi inayofikia 3007.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi,Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Wizara ya Fedha,Profesa Isaya Jairo, alisema kazi ya bodi ya ushauri ni kutoa ushauri ili kuendeleza jitihada za serikali katika kutekeleza malengo makuu ya taasisi.
Aliyataja malengo ya taasisi kuwa ni kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri kwenye fani za uhasibu, ununuzi na ugavi, uongozi wa biashara, usimamizi wa rasilimali watu, masoko na uhusianowa jamii pamoja nauhasibu wa fedha za umma na katika Nyanja nyingine za biashara.
                                               Na Mbeya yetu

BANDARI YA KASANGA KUANZA KUBORESHWA

Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja katika jiwe la msingi la uzinduzi wa maghala ya kuhifadhia mizigo katika Bandari ya Kasanga. Maghala hayo yalifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilali tarehe 22 Februari 2012.
Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kushoto) akimfafanualia jambo Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kulia) wakati akimkabidhi taarifa ya maendeleo ya bandari hiyo. 
 
Na Saidi Mkabakuli, Sumbawanga
Serikali imeazimia kuanza kuiboresha bandari ya kimkakati ya Kasanga inayohudumia nchi za Burundi, Rwanda na Kongo iliyopo katika Ziwa Tanganyika, mkoani Rukwa.
Ahadi hiyo imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Bandari ya Kasanga.
Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania imepanga kuboresha bandari zote ili kuwa malango kuu la biashara kwa soko la ndani na kwa nchi jirani ili kuongeza uwezo wa kuhudumia shehena kwa ufanisi.
“Tumedhamiria kuendelea kuboresha miundombinu ya bandari hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa ikiwemo Bandari ya Kasanga ili kuweza kukidhi mahitaji ya utoaji wa huduma katika eneo hili,” alisema.
Bibi Mwanri aliongeza kuwa serikali pia imejipanga kuendelea kuboresha miundombinu na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kuhudumia shehena katika bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Kasanga na Kigoma na kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa bandari mpya za Mwambani (Tanga), Mbegani (Bagamoyo) na Bandari Kavu ya Kisarawe.
Akizungumza na ugeni huo, Msimamizi Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa alisema kuwa Bandari hiyo ina fursa nyingi katika kuhudumia shehena na abiria wanaopitia bandarini hapo.
“Bandari yetu ina fursa kubwa za kibiashara kwani tuna wateja wengi kutoka ndani na nje ya nchi wanaotumia bandari yetu kupitishia bidhaa zao, pamoja na abiria wanaosafiri kwenda nje na ndani ya Tanzania,” alisema.
Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo kwa mwaka ujao wa fedha Serikali imedhamiria kuboresha mazingira yatakayowezesha sekta binafsi kuwekeza katika kujenga miuondombinu na kuboresha usafirishaji wa mizigo katika bandari zote nchini.
Pia, Mpango huo unaweka bayana kuendeleza na ukarabati na ununuzi wa vyombo vya usafiri na usafirishaji katika maziwa.

Jumatano, 26 Novemba 2014

MAMLAKA YA BANDARI KUJENGA MELI ZIWA NYASA


Na Saidi Mkabakuli, Kyela

Kufuatia adha ya usafiri wa majini inayowakabili wakazi waishio katika fukwe za Ziwa Nyasa, Mamlaka ya Bandari Tanzania kupitia kituo chake cha Kyela ipo mbioni kujenga meli ya abiria na mizigo ili kuwahudumia wakazi hao.


Hayo yaliwekwa bayana na Mkuu wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema wakati timu wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Tume ya Mipango ilipotembelea na kukagua bandari za Itungi na Kiwira zilizopo wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.


Bw. Ntetema alisema kuwa Mamlaka imeshakamilisha mchakato wa manunuzi na tayari imempata mkandarasi M/S Songoro Marine Transport Ltd kwa ajili ya ujenzi wa meli yenye uwezo wa kubeba jumla ya tani 200 za mizigo na abiria 200.


“Mamlaka ipo kwenye hatua za mwisho za kuandaa mkataba unaotarajiwa kutiwa saini mwezi ujao  na kazi itaanza mwanzoni mwa mwaka ujao,” alisema.


Bw. Ntetema aliongeza kuwa mpaka sasa Bandari ya Kyela imeshaanza maandalizi ya kuvuta umeme uliofadhiliwa na Wakala wa Umeme Vijijini pamoja na kuaanza kwa kujenga matishari mawili ili yaweze kurahisisha utoaji wa huduma mara meli hiyo itakapoanza kazi mwishoni mwa mwaka ujao.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri aliupongeza uongozi wa Mamlaka kwa hatua yake hiyo kwani itaongeza tija ya shughuli za kiuchumi katika kanda hiyo ya Ziwa Nyasa.


“Ninaupongeza uongozi wa Mamlaka ya Bandari kwa kuanza mchakato huu utakaofungulia fursa za kiuchumi na maendeleo kwenye ukanda huu, hivyo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza vikwazo mbalimbali vinavorudisha kasi ya kusaka kupunguza umaskini nchini,” alisema. 


Bibi Mwanri aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutatoa fursa za kuhudumia shehena na abiria kutoka mikoa ya Mbeya, Njombe, na Ruvuma. Pamoja na kuhudumia nchi za jirani ikiwemo Malawi, Msumbiji na Zambia.


Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/2012 – 2015/2016) bandari ni mojawapo ya vipaumbele vitano vya kimkakati vyenye lengo la kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi wa uchumi kwa watu walio wengi.  

Vipaumbele vingine ni Kilimo ambapo lengo kuu likiwa ni kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo ili kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ya kuuza nje ya nchi; Maendeleo ya viwanda: 

Msisitizo umewekwa katika kuvutia, kuanzishwa na kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini (kama vile viwanda vya nguo, mbolea, saruji, makaa ya mawe, chuma na bidhaa za chuma) na pia sekta ya madini kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali. 


Pamoja na kipaumbele cha Maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi: Mpango unahimiza kuwekeza katika elimu (hasa katika elimu ya juu na vyuo vya ufundi) na huduma za afya (kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma) katika kujenga nguvu kazi itakayotuletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii; na Utalii, Biashara, na huduma za Fedha ambapo jitihada zimewekwa kwenye uendelezaji uwezo wa kuuza katika masoko ya ndani na nje, kuongeza   idadi ya watalii na matumizi yao wawapo nchini, na kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha.

Jumatatu, 24 Novemba 2014

NI CCM NA CHADEMA SERIKALI ZA MITAA MBALIZI




VYAMA viwili pekee, ndivyo vimethibitisha na kurejesha fomu za kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbalizi, Mbeya Vijijini,mkoani hapa, ili kuunda mji mdogo wa Mbalizi.


 
Msimamizi wa uchaguzi wa eneo hilo, ambaye ni afisa mtendaji wa Kijiji cha Mbalizi, Malongo Sumuni, alivitaja vyama hivyo kuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha demokrasia na Maendeleo(Chadema).

Aliwataja wagombea wa nafasi hiyo kuwa ni Asifiwe Godwin  Mwakalonge(CCM), na Elia Wilson  Mkono(Chadema), ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho na ni diwani wa kata ya Utengule Usongwe kupitia Chadema.

“Mbali na kurejesha fomu na kuteuliwa kuwania nafasi hiyo, hawaruhusiwi kufanya kampeni mpaka zitakaporuhusiwa tarehe 30/11/2014 na mwisho itakuwa Desemba 13, mwaka huu” alisema msimamizi huyo.

Alipoulizwa idadi ya wakazi wa eneo hilo, alisema kuwa takwimu alizonazo zinaonesha wakazi 13,690, takwimu ambazo amesema siyo halisi.”Tuna vitongozji vitano ambavyo ni Mlimareli yenye kaya 2900 wakazi 3700, Chapa Kazi kaya 1800 wakazi 3200, DDC kaya 1534 wakazi 2320, Pipeline kaya 1250 wakazi 1650 na Mtakuja kaya 1650 chenye wakazi 3200” alisema Sumuni.

Uchunguzi umebaini kuwa, ofisi yake ilipelekewa idadi ndogo ya wakazi kwa kile wenyeviti wa vitongozi walichokuwa wakihofia katika ukusanyaji wa michango, kuwa endapo wakazi wachache wangechagia, wangesumbuliwa wao kufuatilia.

Mji huo wa Mbalizi, ndiyo kitovu cha siasa za Jimbo la Mbeya Vijijini, ambapo vyama vine vya siasa vimekuwa vikichuana vikiwemo Chama cha wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi, CCM na Chadema.

Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wameendelea kujiandikisha kwa ajili ya upigaji kura wa viongozi wa serikali za mitaa ifikapo Desemba 14, mwaka huu, huku kila kituo kikiwa na mawakala wa vyama vya siasa, hususani CCM na Chadema.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...