Waziri
 wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akitoka nje ya nyumba ya 
kimasai alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha 
uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Waziri
 wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Wamasai 
waliokusanyika kwa ajili ya kusikia tamko la serikali juu ya uvumi wa 
kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Wamasai wakichukua kumbukumbu muhimu katika mkutano wao na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu. 
Waziri
 wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya 
pamoja na baadhi ya wanawake wa jamii ya kimasai mara baada ya kumaliza 
mkutano nao.
Makamu
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Raphael Rong’oi 
akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai kabla ya kumkaribisha Waziri
 wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu (aliyekaa kwenye pikipiki). 
Waziri
 wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu, amesema habari zinazodai 
kuwa Serikali inataka kuwaondoa wakazi wa zaidi ya 40,000 katika eneo la
 Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha  hazina ukweli wowote.
Novemba
 mwaka huu, gazeti The Guardian la nchini Uingereza, liliandika habari 
kuwa serikali ina mpango wa kuwafukuza Wamasai wanaoishi eneo hilo.
Gazeti hilo lilidai kuwa, lengo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu.
Akizungumza
 na wananchi wa jamii ya kimasai wilayani Ngorongoro mwishoni mwa wiki, 
Nyalandu alisema habari hizo hazina ukweli wowote isipokuwa zina lengo 
la kuchafua taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa.
Aliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi bila hofu, kwa sababu serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye makazi yao.
“Nami 
niwahakikishie wanajamii wa Loliondo, Ngorongoro na wanajamii wote wa 
kimasai ambao wametishiwa nyau, kuwa serikali ya Tanzania haina mpango 
wowote wa kumfuata na kumfukuza mtu yoyote,” alisema.
Credit.matukio-michuzi 
  
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni