Hatimaye Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,Godfrey
Zambi,ametoa ruhusa ya kuuzwa mara moja shamba kubwa la kahawa la
Gararagua mali ya Chama Kikuu cha ushirika mkoani Kilimanjaro(KNCU).
Hatua hiyo imekuja siku chake baada ya ofisi ya Mrajis wa vyama
vya ushirika nchini kuzuia uuzwaji wa shamba hilo ikishinikiza kuondolewa kwa
Bodi ya wakurugenzi ya KNCU hatua ambayo iliibua malumbano makali baina
yake na bodi ya chama hicho.
Akizungumza wiki hii katika mkutano Mkuu maalumu,Zambi alisema
ofisi ya mrajis haina mamlaka kisheria ya kuiondoa bodi ya KNCU na kwamba
mwenye mamlaka hayo ni wanachama ambao oktoba 22 mwaka huu walipiga kura na
kuridhia bodi hiyo kuendelea kuwapo madarakani.
Waziri Zambi alisema kuwa,shamba hilo litauzwa kwa uwazi baada ya
kufanyika kwa tathimini ya thamani halisi ya shamba hilo na kwamba kitaundwa
chombo kitakachosimamia uuzwaji huo ili kukiwezesha kuondokana na mzigo wa
madeni unaokiandama likiwamo deni kubwa la benki ya CRDB .
Awali ofisi ya mrajis wa vyama vya ushirika nchini,licha ya
kuchelewa kutoa kibali cha kuuzwa kwa shamba hilo,ilitoa masharti ikitaka bodi
ya sasa ya KNCU iondoke madarakani na shamba hilo liuzwe chini ya bodi mpya
hatua ambayo ilisababisha malumbano makali.
Kutokana na masharti hayo, KNCU iliandika barua ya malalamiko kwa
waziri mwenye dhamana na ushirika wakidai kuwa masharti hayo yanaendelea kukiumiza
chama hicho kwa kuendelea kulipa mamilioni ya fedha kwa CRDB kama riba.
Katika taarifa yake kwa wajumbe wa mkutano huo mkuu
maalumu,mwenyekiti wa chama hicho,Maynard Swai alimweleza waziri Zambi
kuwa,hatua hiyo ya mrajis kuzuia uuzwaji wa shamba hilo ni kuleta machafuko kwa
chama hicho na kuua ushirika.
Chama hicho kinamiliki mashamba makubwa manne ambayo ni Gararagua,
Lerongo,Lyamungo na Molomo na kati ya hayo matatu yamekodishwa kwa wawekezaji
wazalendo huku moja likitarajiwa kutumika kwa shughuli za uzalishaji wa miche
bora ya kahawa na kuwa shamba darasa.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo,chama hicho kinakabiliwa na
changamoto kadhaa ikiwamo kuyumba kwa bei ya kahawa kwenye soko la dunia,mbinu
chafu za kibiashara kutoka kwa wapinzani wake.
Aliainisha changamoto nyingine kuwa ni kuwapo kwa ushawishi mbaya
wa kisiasa wenye nia ya kukivuruga chama hicho pamoja na mzigo mkubwa wa madeni
kuanzia msimu wa 2003/2004 hadi hivi sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni