WAHADHIRI
wa Vyuo mbali mbali nchini wametakiwa kutoa elimu kwa wanafunzi kulingana na
soko la ajira ikiwa ni pamoja na fani inayoendana na cheti alichopata ili
kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
Hayo
yalibainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Profesa Norman Sigalla, alipokuwa
amemwakilisha Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, katika mahafali ya 12 ya
Taasisi ya Uhasibu (TIA)Kampasi ya Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya taasisi
hiyo mjini hapa.
Profesa
Sigalla alisema hivi sasa kuna ushindani wa vyuo na ukosefu wa ajira nchini
hivyo I vema wahadhiri wakatoa wanafunzi wenye sifa kulingana na vyeti
wanavyopata ili kukidhi soko la ajira ikiwa ni pamoja na kujiajiri wenyewe na
sio kusubiri kuajiriwa.
“
kutokana na ongezeko la vyuo na ushindani uliopo ni vema wahadhili wakatoa
wahitimu wenye sifa za kipekee kuendana na aina ya cheti alichopata na
kukabiliana na soko la ajira” alisema Profesa Sigalla.
Aliongeza
kuwa wajibu wa vyuo ni kuandaa watalaam mbali mbali ili waweze kutumikia taifa
na kukidhi haja ya nchi katika kujiletea maendeleo kwa wahitimu kufuata
walitofundishwa madarasani na kutumia taaluma yao kupambana na changamoto
zilizopo uraiani.
Alisema
ni vema wahitimu kutokana na elimu waliyoipata wakaangalia fursa zilizopo
nchini wakazitumia vizuri badala ya kusubiri kuajiriwa na serikali kutokana na
mfumo uliopo wa kutoa ajira kwa kila mtu kuwa mgumu baada ya wahitimu
kuongezeka kila kukicha.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji mkuu wa Tasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) Dk. Joseph
Kihanda,alisema katika mwaka wa masomo 2013/2014 jumla ya wanafunzi 1960
wakiwemo wanawake 947 na wanaume 1013 wamehitimu katika fani za cheti cha
awali, Stashahada na stashahada ya uzamili katika kampasi ya Mbeya.
Alisema
Chuo hicho kinakabiliwa na Changamoto za kudumu na mpya ambazo ni uhaba wa
majengo kama vile kumbi za mhadhara, maktaba za kisasa na vitabu, ofisi za
wafanyakazi na nyumba za wafanyakazi na wahadhiri pamoja na upungufu wa
thamani.
Aliongeza
kuwa changamoto mpya zinazokikabili chuo hicho ni pamoja na uwiano wa
wahadhirina wanafunzi kutokuwa mzuri kutokana na ongezeko kubwa la udahili
kutokana na ajira ya wahadhiri kusimamiwa na Serikali kuu hivyo kushindwa
kupata wahadhiri wanaoweza kuendana na idadi wa wanafunzi ambapo hivi
sasa chuo kina wahadhiri 19.
Dk
Kihanda aliongeza kuwa Changamoto nyingine ni upatikanaji wa maji katika
Kampasi ya Mbeya kuwa ni wa kusuasua hivyo kuhatarisha afya za wanafunzi kunakoweza
kusababishwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi
inayofikia 3007.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi,Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Wizara ya
Fedha,Profesa Isaya Jairo, alisema kazi ya bodi ya ushauri ni kutoa ushauri ili
kuendeleza jitihada za serikali katika kutekeleza malengo makuu ya taasisi.
Aliyataja
malengo ya taasisi kuwa ni kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri
kwenye fani za uhasibu, ununuzi na ugavi, uongozi wa biashara, usimamizi wa
rasilimali watu, masoko na uhusianowa jamii pamoja nauhasibu wa fedha za umma
na katika Nyanja nyingine za biashara.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni