Jumatano, 30 Julai 2014
Jumanne, 29 Julai 2014
NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
NAFASI ZA
MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
UTANGULIZI
Moja ya mikakati ya
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha
kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti ni
wale wenye ufaulu mzuri katika mtihani ya kidato cha NNE. Ili kufanikisha azma
hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa
Daraja la Tatu kwa ajili ya Cheti na wenye ufaulu wa alama 26 au 27 (mwaka 2004
hadi 2012) na alama 33 au 34 (mwaka 2013) watadahiliwa katika programu ya
mafunzo kabilishi ya mwaka mmoja.
Aidha, kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo
ya Sayansi, Hisabati, English na
Kiswahili. Watakaojiunga na mafunzo ya ualimu na kufaulu mafunzo yao watapatiwa
ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za Serikali.
VIGEZO
Vigezo vifuatavyo
vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/15.
1:
|
MAFUNZO
YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA
CHETI DARAJA ‘A’: MUDA MIAKA 2
|
(i)
Cheti Ualimu wa kawaida katika vyuo vya Ilonga, Kabanga, , Kitangali, Mandaka ,
Murutunguru , Ndala , na Tarime
(ii)
Cheti
Ualimu Elimu ya Awali katika vyuo vya
Kabanga,
Kinampanda, Mhonda, Mtwara (U), Singachini, Tandala, Tarime
(iii) Cheti Ualimu Elimu kwa michezo katika
vyuo vya Ilonga, Tarime, Ndala na Mtwara
(U)
Mwombaji
awe:
Mhitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 mwenye
ufaulu wa kiwango kisichopungua Daraja
la III katika Mtihani
uliofanyika katika kikao kimoja.
|
|
2:
|
MAFUNZO
KABILISHI NGAZI YA CHETI (BRIDGING COURSE) KWA AJILI YA KUJIUNGA NA MAFUNZO
YA UALIMU NGAZI YA CHETI:- MUDA MWAKA 1
|
Mafunzo katika vyuo vya
ualimu Bustani,
Kinampanda, Mhonda, Mpuguso, Mtwara (U), Nachingwea, Singachini, Tandala,
Katoke na Sumbawanga
Mwombaji awe:
(i)
Amehitimu wa Kidato cha IV
kati ya mwaka 2004 hadi 2012 na
awe amefaulu kwa kiwango
kisichopungua Daraja la IV kwa alama 26 au 27 (kwa mtihani wa mwaka
2004 hadi 2012) na alama 33 au 34 (mtihani wa mwaka 2013) kwa
mitihani iliyofanyika katika kikao kimoja; na
(ii)
Mwenye ufaulu wa angalau kiwango cha D katika masomo ya Sayansi, Hisabati, English na
Kiswahili katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi:
Watakaofaulu mtihani wa mafunzo kabilishi wataendelea na mwaka wa pili wa
mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti Daraja A
|
|
3:
|
ELIMU MAALUM: MIAKA 2
katika chuo cha Patandi:-
|
Mwombaji awe:
(i)
Mwalimu wa
Daraja ‘A’ mwenye uzoefu wa
kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
(ii) Mwenye ufaulu angalau
somo moja la Sayansi katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi:Walimu wanaofundisha Elimu
Maalum hata kama hawana mafunzo maalumu ni sifa ya nyongeza (uthibitisho
uambatishwe).
|
MAELEZO MUHIMU
(i)
Vigezo vilivyoelekezwa kwa
waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti ni kwa ajili ya waombaji wa
mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu
vya Serikali na visivyo vya Serikali;
(ii)
Muombaji wa chuo cha ualimu
cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa
kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
(iii)
Wahitimu Kidato cha IV mwaka
2013 waliojaza nafasi ya mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti Daraja ‘A’ kwenye ‘Selforms’ wakati wanamaliza Elimu ya
Sekondari wanatakiwa kuomba upya
mafunzo hayo;
(iv)
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu
walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release)
kutoka kwa waajiri wao;
(v)
Majibu kwa watakaochaguliwa
kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti
za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE
(www.nacte.go.tz)
(vi)
Waombaji watakaochaguliwa
watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu
watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
(vii)
Tangazo hili lipo pia katika
tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM
TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye
ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu.
Namna ya kutuma maombi:
a) Waombaji watume maombi yao kwa njia ya MTANDAO
(online application) kupitia tovuti zifuatazo: www.moe.go.tz AU www.nacte.go.tz
Maombi kwa njia ya mtandao yataambatana na ada ya shilingi 10,000 itakayolipwa
kwa kutumia MPESA. Maelekezo ya kina kuhusu namna ya kutuma maombi kwa
njia ya mtandao yanapatikana katika tuvuti ya wizara www.moe.go.tz na Baraza la Taifa
la Elimu ya Ufundi www.nacte.go.tz
Malipo ya
maombi yanaweza kufanyika kupitia MPESA kama ifuatavyo:
1.
Piga
*150*00#
2.
Chagua
4. (Lipa kwa MPESA);
3.
Chagua
1. (Weka LIPA Namba);
4.
Weka
LIPA Namba (ingiza namba 607070);
5.
Ingiza
kiasi (ingiza kiasi cha 10,000.00);
6.
Weka
Enter Reference No. ( ingiza 1234);
7.
Weka
namba ya SIRI (ingiza namba yako ya siri); na
8.
Ingiza
1 kuthibibitisha malipo.
AU
b) Barua kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA
MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione:
Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)
Jumapili, 20 Julai 2014
UMEME KUTUA VIJIJINI, MKOANI RUVUMA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akielekea eneo la jukwaa mara baada ya kuwasili katika
eneo palipofanyika uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme vijijini unaosimamiwa
na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) wilaya ya Nyasa mwishoni mwa wiki, kushoto kwake
ni Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
Meneja
wa Shirika la umeme nchini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Bi Salome Nkondola akiwasilisha taarifa fupi
ya utekelezaji wa miradi ya umeme kwa mkoa wa Ruvuma mbele ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete.
Rais
Jakaya M. Kikwete akichukua mkasi kwa ajili ya kukata utepe tayari kuelekea
katika eneo la uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa umeme wilayani Nyasa mkoa wa
Ruvuma, kulia kwake ni Waziri mwenye dhamana na nishati Prof. Sospeter Muhongo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wa serikali wakiwepo Waziri
wa Ardhi na maendeleo ya Makazi, Waziri wa Nishati na
Madini, Waziri wa Ujenzi wakiwa wameshika utepe tayari kwa Rais kuukata na
kuelekea kubonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi huo wa umeme.
Rais akifunua kitambaa mahali palipowekwa kitufe
kwa ajili ya uzinduzi rasmi
Rais akifunua kitambaa mahali palipowekwa kitufe
kwa ajili ya uzinduzi rasmi
Rais
akibonyeza kitufe
Rais akifurahia uzinduzi mara baada ya zoezi
hilo kukamilika
Burudani wakati wa sherehe hizo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
amezindua mradi wa kusambaza umeme vijijini unaosimamiwa na Wakala wa
Umeme Vijijini (REA) utakaowanufaisha wakazi wa Mkoa wa Ruvuma
utakaochangia kuongeza kasi ya maendeleo vijijini.
Rais
Jakaya Kikwete yuko katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya
maendeleo katika mkoa huo lengo likiwa ni kutimiza azma ya serikali ya
kuwa kila mwananchi anapata huduma ya nishati ya umeme.
Kwa
upande wake Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo
amewahakikishia wakazi hao kwamba hadi ifikapo mwezi Novemba mwaka huu
vijiji vyote vilivyoko katika mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya
II watakuwa tayari wanatumia nishati hiyo kwa wale watakao wamemudu
gharama ya Shilingi Elfu Ishirini na Saba ya kuunganishiwa nishati
hiyo.
Imeelezwa
kwamba mradi wa usambazaji wa umeme vijijini katika mkoa wa Ruvuma
utagharimu kiasi cha Tsh. 26.53 bilioni zitakazohusisha ujenzi wa njia
za umeme zenye msongo wa kilovolti 33 zenye jumla ya urefu wa km 538,
ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovolti 11 yenye urefu wa km 23,
ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa km 272,
ufungaji wa transfoma 129 za ukubwa mbalimbali pamoja na kuunganisha
wateja 7,488.
Mradi
huu utatekelezwa na kampuni ya Lanka Transfomers Limited, (LTL) ya
nchini SRILANKA kwa mkoa wa Ruvuma. Mradi huo unatarajiwa kukamilika
ifikapo Juni 2015 na kunufaisha wakazi wa wilaya za Songea, Tunduru,
Mbinga na Nyasa.
Pamoja
na uwepo wa mradi huo pia kuna mradi wa kuongeza nguvu ya umeme kwenye
wilaya za Mbinga na Tunduru unaotekelezwa na kampuni ya Taikai Co.Ltd
ambapo tayari amekamilisha survey ya vituo vyote na ameshawasilisha
transifoma ya kituo cha Tunduru.
Prof. MUHONGO amesema mradi wa kuongeza nguvu ya umeme utagharimu kiasi
cha pesa za kitanzania Shilingi bilioni 2.27 zitakazohusisha ujenzi wa
vituo viwili vya kuongeza nguvu ya umeme kutoka kilovoti 11 hadi kufikia
kilovoti 33 kwa ajili ya kufikisha umeme katika vijiji vilivyoko
mbali.
Vituo
hivyo vitakuwa na transifoma zenye uwezo wa kilowati 3,000 (3.0MW) kila
kimoja.
Kwa upande wake Mbunge wa MBAMBABAY Captain JOHN KOMBA ameishukuru
serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi
ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara hasa
madaraja, kuwawekea umeme, na kupandishwa hadhi kituo cha afya na kuwa
hospitali ya wilaya.
Miradi
ya REA awamu ya II imeanza kutekelezwa rasmi Novemba 2013 na inatakiwa
kukamilika ifikapo Juni2015 kwa nchi nzima hivyo kuchangia katika
kuongeza kiasi cha wananchi waliofikiwa na huduma ya umeme kufikia
asilimia 30.
CREDIT;Michuzi blog
NDOO ZA MSUMBIJI MARUFUKU KUNUNULIA MPUNGA KYELA
NDOO zinazotoka nchini Msumbiji, zimepigwa marufuku kununulia mpunga katika kata ya Ipande,wilayani Kyela mkoani Mbeya, kutokana na ndoo hizo kuwa na ujazo mkubwa.
Marufuku hiyo imepgwa na Halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Ipande, na kwamba atakayekutwa akinunulia ndoo hizo au kuwapeleka watu kununua mpunga kwa kutumia ndoo hizo, atatozwa faini ya Tsh.20,000/=
Diwani wa kata hiyo, Steven Mwangalaba, amethibitisha na kwamba, wao hawakatazi mtu kununua mpunga wala kuuza, bali wanazikataa ndoo hizo kwasababu zinawanyonya wakulima.
Marufuku hiyo imepgwa na Halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Ipande, na kwamba atakayekutwa akinunulia ndoo hizo au kuwapeleka watu kununua mpunga kwa kutumia ndoo hizo, atatozwa faini ya Tsh.20,000/=
Diwani wa kata hiyo, Steven Mwangalaba, amethibitisha na kwamba, wao hawakatazi mtu kununua mpunga wala kuuza, bali wanazikataa ndoo hizo kwasababu zinawanyonya wakulima.
Jumatano, 16 Julai 2014
Jumanne, 15 Julai 2014
MBUNGE VITI MAALUM MKOA WA MBEYA, DR.MARY MWANJELWA, ATIMIZA AHADI YA VIJANA WALIOMUOMBA JEZI NA MIPIRA ISYESYE MBEYA MJINI
MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akifurahia jambo na kocha mkuu wa timu ya Isyesye FC, Steve Kasalila (KULIA) na Katibu wa wanawake wa CCM kata ya Isyesye, Zainab Kessy(KULIA).
MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akifunga gori la penalti, na kumwacha mlinda mlango wa timu ya Isyesye.MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akimkabidhi kocha mkuu wa timu ya Isyesye Jijini Mbeya,Steve Kasalila, jozi ya jezi na mipira mitano leo.
MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akihutubia wananchi na wachezaji wa timu ya Isyesye na Veta leo jioni, katika uwanja wa Isyesye, Vingunguti Relini Jijini Mbeya, wakati wa kukabidhi jozi moja ya jezi na mipira mitano kwa timu ya Isyesye Jijini Mbeya.
MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akihutubia wananchi na wachezaji wa timu ya Isyesye na Veta leo jioni, katika uwanja wa Isyesye, Vingunguti Relini Jijini Mbeya, wakati wa kukabidhi jozi moja ya jezi na mipira mitano kwa timu ya Isyesye Jijini Mbeya.
Mweyekiti wa UVCCM Mbeya Mjini, Maranyingi Matukuta, akifungua jezi, wakati wa MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akihutubia wananchi na wachezaji wa timu ya Isyesye na Veta leo jioni, katika uwanja wa Isyesye, Vingunguti Relini Jijini Mbeya, kisha kukabidhi jozi moja ya jezi na mipira mitano kwa timu ya Isyesye Jijini Mbeya.
Akipokea bahasha kutoka kwa machifu wa eneo la Isyesye, Jijini Mbeya leo.
MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akisalimiana na wachezaji wa timu ya VETA NA ISYESYE Jijini Mbeya, eneo la uwanja wa vingunguti Relini Jijini Mbeya, wakati wa kukabidhi jozi moja ya jezi na mipira mitano kwa timu ya Isyesye Jijini Mbeya.
MBUNGE viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr, Mary Mwanjelwa, akipiga penlti kwa ustadi mkubwa, baada ya kuhutubia wananchi na wachezaji wa timu ya Isyesye na Veta leo jioni, katika uwanja wa Isyesye, Vingunguti Relini Jijini Mbeya, na kukabidhi jozi moja ya jezi na mipira mitano kwa timu ya Isyesye Jijini Mbeya.
MORAVIAN JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI, WACHUNGAJI WATAKA KUFUNGA OFISI, SERIKALI YANUSURU.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla akiongea na baadhi ya wachungaji na waumini wa kanisa la Moravian kuwaomba wafunguo ofisi hizo ili mazungumzo yafanyike |
Mmoja wa wachungaji hao, Edward Chilale akiongea na Baadhi ya waandishi wa habari |
Moja ya waumini wa kanisa hilo akifungua mnyororo uliofungwa ofisini kwa Askofu |
PROF;MWANDOSYA AKUTANA NA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA LEO MBEYA
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya University of Science and Technology-MUST) (Chancellor),Profesa Mark Mwandosya (kulia) akiwa kwenye mkutano na uongozi wa Chuo hicho ofisini kwake Ikulu,Dar es Salaam.Ujumbe huo,ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo umempa taarifa Mkuu wa Chuo kuhusu maendeleo ya Chuo, changamoto zinzokikabili,na mipango ya kukiimarisha Chuo kifedha,kitaaluma,na miundombinu yake.
credit;michuzi blog
Jumatatu, 14 Julai 2014
PROF. SIGALLA; DR. MWANJELWA ANAO UWEZO WA KIUONGOZI
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,
Dr. Mary Mwanjelwa, akikaribishwa leo na wanawake katika ukumbi wa OTTU
Mbeya, kwa ajili ya ufunguzi wa semina ya ambapo mgeni rasmi alikuwa ni
Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla.
Wanawake hoyeee. Kulia ni mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla.
Baadhi ya washiriki ukumbini.
Mwandaaji wa semina hiyo ya stadi za uongozi. Dr. Mary Mwanjelwa, akisema neno..
Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, akifungua semina ya wanawake, kuhusu stadi za uongozi Jijini Mbeya, katika ukumbi wa OTTU, ambapo wanawake kutoka wilaya tisa za mkoa wa Mbeya, walihudhuria.
Mmoja wa watoa mada katika semina hiyo, Tumaini Mwakatika, akisema neno mbele ya kamera ya TBC1.
Kulia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akipongezwa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, kwa kuandaa semina ya stadi za uongozi kwa wanawake wa wilaya tisa za mkoa wa Mbeya.
Wanawake hoyeee. Kulia ni mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla.
Baadhi ya washiriki ukumbini.
Mwandaaji wa semina hiyo ya stadi za uongozi. Dr. Mary Mwanjelwa, akisema neno..
Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, akifungua semina ya wanawake, kuhusu stadi za uongozi Jijini Mbeya, katika ukumbi wa OTTU, ambapo wanawake kutoka wilaya tisa za mkoa wa Mbeya, walihudhuria.
Mmoja wa watoa mada katika semina hiyo, Tumaini Mwakatika, akisema neno mbele ya kamera ya TBC1.
Kulia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akipongezwa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, kwa kuandaa semina ya stadi za uongozi kwa wanawake wa wilaya tisa za mkoa wa Mbeya.
MKUU wa
wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, amewaasa wanawake
nchini, kuacha kudharauliana ili waweze kufikia nafasi ya hamsini kwa hamsini
katika uongozi.
Ameyasema
hayo jana, alipofungua semina ya wanawake kutoka wilaya zote za mkoa wa Mbeya,
iliyoandaliwa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, MNEC, Dr, Mary Mwanjelwa,
kuhusu stadi za uongozi na mbinu za kufanikiwa kisiasa ndani ya vyama vingi.
Prof.
Sigalla, alisema kuwa, wanawake wengi wanashindwa kuchaguliwa kwenye nafasi
mbalimbali kutokana na kutopendana na kutosimamisha mwanamke shupavu.
“Mkimsimamisha
mwanamke kama Dr. Mwanjelwa, hata mimi nitamchagua siyo kwasababu ni mwanamke,
bali kwasababu anao uwezo wa kuongoza na mwonekano’’ alisema Prof. Sigalla.
Mwandaaji wa
mafunzo hayo, Dr. Mary Mwanjelwa, alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa
wanawake, maana ukimwezesha mwanamke umewezesha jamii nzima.
“Mwanzo semina
kama hii niliwaandalia madiwani wanawake wote wa mkoa wa Mbeya kisha na
madiwani wanaume na sasa viongozi hawa ngazi ya matawi na kata ambao naamini
watapeleka elimu watakayoipata kwa jamii’’ alisema Dr. Mwanjelwa.
Mmoja wa
wawezeshaji wa semina hiyo ambayo inahusu mada ya stadi za uongozi na mbinu za
kufanikiwa kisiasa ndani ya demokrasia ya vyama vingi, Tumaini Mwakatika,
alisema kuwa semina hiyo ya siku tatu, itawawezesha wanawake hao kutambua mambo
ya msingi katika uongozi.
“Watapata
kujua changamoto za uongozi, nadharia ya uongozi na tabia za viongozi, mambo ya
msingi katika uongozi na misingi ya utawala wa kidemokrasia na matarajio ya
wananchi”alisema Tumaini Mwakatika.
Baadhi ya
washiriki akiwemo Everada Mwangwala na Agatha Ngole, walisema kuwa, matarajio
yao katika semina hiyo ni kupata ujasiri wa kujiamini kwa manufaa ya wananchi.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...