Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,
Dr. Mary Mwanjelwa, akikaribishwa leo na wanawake katika ukumbi wa OTTU
Mbeya, kwa ajili ya ufunguzi wa semina ya ambapo mgeni rasmi alikuwa ni
Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla.
Wanawake hoyeee. Kulia ni mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla.
Baadhi ya washiriki ukumbini.
Mwandaaji wa semina hiyo ya stadi za uongozi. Dr. Mary Mwanjelwa, akisema neno..
Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, akifungua semina ya wanawake, kuhusu stadi za uongozi Jijini Mbeya, katika ukumbi wa OTTU, ambapo wanawake kutoka wilaya tisa za mkoa wa Mbeya, walihudhuria.
Mmoja wa watoa mada katika semina hiyo, Tumaini Mwakatika, akisema neno mbele ya kamera ya TBC1.
Kulia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akipongezwa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, kwa kuandaa semina ya stadi za uongozi kwa wanawake wa wilaya tisa za mkoa wa Mbeya.

MKUU wa
wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, amewaasa wanawake
nchini, kuacha kudharauliana ili waweze kufikia nafasi ya hamsini kwa hamsini
katika uongozi.
Ameyasema
hayo jana, alipofungua semina ya wanawake kutoka wilaya zote za mkoa wa Mbeya,
iliyoandaliwa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, MNEC, Dr, Mary Mwanjelwa,
kuhusu stadi za uongozi na mbinu za kufanikiwa kisiasa ndani ya vyama vingi.
Prof.
Sigalla, alisema kuwa, wanawake wengi wanashindwa kuchaguliwa kwenye nafasi
mbalimbali kutokana na kutopendana na kutosimamisha mwanamke shupavu.
“Mkimsimamisha
mwanamke kama Dr. Mwanjelwa, hata mimi nitamchagua siyo kwasababu ni mwanamke,
bali kwasababu anao uwezo wa kuongoza na mwonekano’’ alisema Prof. Sigalla.
Mwandaaji wa
mafunzo hayo, Dr. Mary Mwanjelwa, alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa
wanawake, maana ukimwezesha mwanamke umewezesha jamii nzima.
“Mwanzo semina
kama hii niliwaandalia madiwani wanawake wote wa mkoa wa Mbeya kisha na
madiwani wanaume na sasa viongozi hawa ngazi ya matawi na kata ambao naamini
watapeleka elimu watakayoipata kwa jamii’’ alisema Dr. Mwanjelwa.
Mmoja wa
wawezeshaji wa semina hiyo ambayo inahusu mada ya stadi za uongozi na mbinu za
kufanikiwa kisiasa ndani ya demokrasia ya vyama vingi, Tumaini Mwakatika,
alisema kuwa semina hiyo ya siku tatu, itawawezesha wanawake hao kutambua mambo
ya msingi katika uongozi.
“Watapata
kujua changamoto za uongozi, nadharia ya uongozi na tabia za viongozi, mambo ya
msingi katika uongozi na misingi ya utawala wa kidemokrasia na matarajio ya
wananchi”alisema Tumaini Mwakatika.
Baadhi ya
washiriki akiwemo Everada Mwangwala na Agatha Ngole, walisema kuwa, matarajio
yao katika semina hiyo ni kupata ujasiri wa kujiamini kwa manufaa ya wananchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni