Jumanne, 29 Julai 2014

NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu: 022-2110146/2110150/2, 211679, Faksi: 022-2113271, Tovuti: www.moe.go.tz
NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
UTANGULIZI
Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti ni wale wenye ufaulu mzuri katika mtihani ya kidato cha NNE. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la Tatu kwa ajili ya Cheti na wenye ufaulu wa alama 26 au 27 (mwaka 2004 hadi 2012) na alama 33 au 34 (mwaka 2013) watadahiliwa katika programu ya mafunzo kabilishi ya mwaka mmoja.
Aidha, kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili. Watakaojiunga na mafunzo ya ualimu na kufaulu mafunzo yao watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za Serikali.
VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/15.
1:
MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’: MUDA MIAKA 2
(i)    Cheti Ualimu wa kawaida katika vyuo vya Ilonga, Kabanga, , Kitangali, Mandaka , Murutunguru , Ndala , na Tarime
(ii)  Cheti Ualimu Elimu ya Awali katika vyuo vya Kabanga, Kinampanda, Mhonda, Mtwara (U), Singachini, Tandala, Tarime
(iii) Cheti Ualimu Elimu kwa michezo katika vyuo vya Ilonga, Tarime, Ndala na Mtwara (U)
Mwombaji awe:
Mhitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 mwenye ufaulu wa kiwango kisichopungua Daraja la III katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.
2:
MAFUNZO KABILISHI NGAZI YA CHETI (BRIDGING COURSE) KWA AJILI YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI:- MUDA MWAKA 1
Mafunzo katika vyuo vya ualimu Bustani, Kinampanda, Mhonda, Mpuguso, Mtwara (U), Nachingwea, Singachini, Tandala, Katoke na Sumbawanga
Mwombaji awe:
(i)             Amehitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 hadi 2012 na awe amefaulu kwa kiwango kisichopungua Daraja la IV kwa alama 26 au 27 (kwa mtihani wa mwaka 2004 hadi 2012) na alama 33 au 34 (mtihani wa mwaka 2013) kwa mitihani iliyofanyika katika kikao kimoja; na
(ii)           Mwenye ufaulu wa angalau kiwango cha D katika masomo ya Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi: Watakaofaulu mtihani wa mafunzo kabilishi wataendelea na mwaka wa pili wa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti Daraja A
3:
ELIMU MAALUM: MIAKA 2 katika chuo cha Patandi:-
Mwombaji awe:
(i)        Mwalimu wa Daraja ‘A’ mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
(ii)      Mwenye ufaulu angalau somo moja la Sayansi katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi:Walimu wanaofundisha Elimu Maalum hata kama hawana mafunzo maalumu ni sifa ya nyongeza (uthibitisho uambatishwe).
MAELEZO MUHIMU
(i)            Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
(ii)          Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
(iii)         Wahitimu Kidato cha IV mwaka 2013 waliojaza nafasi ya mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti Daraja ‘A’ kwenye ‘Selforms’ wakati wanamaliza Elimu ya Sekondari wanatakiwa kuomba upya mafunzo hayo;
(iv)          Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
(v)           Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz)
(vi)         Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
(vii)        Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu.
Namna ya kutuma maombi:
a)    Waombaji watume maombi yao kwa njia ya MTANDAO (online application) kupitia tovuti zifuatazo: www.moe.go.tz  AU  www.nacte.go.tz

Maombi kwa njia ya mtandao yataambatana na ada ya shilingi 10,000 itakayolipwa kwa kutumia MPESA. Maelekezo ya kina kuhusu namna ya kutuma maombi kwa njia ya mtandao yanapatikana katika tuvuti ya wizara www.moe.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi www.nacte.go.tz
Malipo ya maombi yanaweza kufanyika kupitia MPESA kama ifuatavyo:
1.       Piga *150*00#
2.      Chagua 4. (Lipa kwa MPESA);
3.      Chagua 1. (Weka LIPA Namba);
4.      Weka LIPA Namba (ingiza namba 607070);
5.      Ingiza kiasi (ingiza kiasi cha 10,000.00);
6.      Weka Enter Reference No. ( ingiza 1234);
7.      Weka namba ya SIRI (ingiza namba yako ya siri); na
8.      Ingiza 1 kuthibibitisha malipo.
AU
b)    Barua kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...