WAREMBO 15 wanatarajia kuchuana vikali katika wilaya ya Mbeya Vijijini, katika ukumbi wa Royal Tughimbe uliopo eneo la Mbalizi wilaya hapa.
Mwandaaji wa shindano hilo, Sarah Kalinga(Mama Neema Decoration
enterprses), alisema warembo tayari wameingia kambini na wapenzi wa mashindano
hayo watarajie kuona utofauti na mashindano yaliyopita.
Alizitaja
changamoto zinazomkabili mpaka sasa kuwa ni ucheleweshaji wa zawadi kwa baadhi
ya wadhamini walizoahidi katika shindano hilo na kwamba ni mdhamini mmoja tu
ambaye tayari mpaka jana alikuwa amewasilisha zawadi.
“Tunamshukuru
mdhamini wetu Acces Computer kwa kuwa mdhamini wa kwanza kutuletea zawadi‘’alisema
Sarah.
Aliyekuwa Miss
Mbeya Vijijini mwaka 2010, Magreth Lucas, alipotafutwa na gazeti hili kwa njia
ya simu kutoka mkoani Shinyanga anakoishi na mumewe, alisema kuna faida nyingi
ya kushiriki katika mashindano hayo.
Alizitaja
baadhi ya faida ambazo wanazipata warembo kuwa ni pamoja na washindi kusoma
bure na kupata mafunzo ya kujitambua wawapo kambini ili wasirubuniwe kirahisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni