Ukarabati wa mabweni unaedelea......
SIKU chache
baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania(CCM), Abdallah Majura
Bulembo, kuamuru shule zote zinazomilikiwa na jumuiya hiyo kote nchini kukata
bima ya moto, shule ya Sekondari Ivumwe imetangaza rasmi kuwa mwishoni mwa
mwezi huu inakata bima hiyo.
Mkuu wa
shule hiyo, Emerry Muhondwa, ameyasema hayo leo baada ya kupokea misaada ya
mabati bando tatu na mifuko ya saruji 20, kutoka kwa kamati ya Utekelezaji ya
Jumuiya hiyo mkoa wa Mbeya, baada ya kuunguliwa na mabweni ya wavulana.
Mbali na
kushukuru, alisema baada ya mabweni ya shule hiyo kuteketea kwa moto na wao
kugharamia pesa nyingi kwa ajili ya ukarabati na kuwanunulia wanafunzi baadhi
ya vitu, wameona umuhimu wa bima hiyo.
Mwenyekiti
wa Jumuiya hiyo mkoani hapa, Fatuma Kasenga, alisema janga la moto huo
lililotokea April 23, mwaka huu, limeleta simanzi na hasara katika shule hiyo,
lakini jambo la kumshukuru Mungu, moto haukuleta madhara ya kibinadamu.
“Msaada huu
unagharimu kiasi cha Milioni Moja, tutahakikisha katika shule zetu zote
kunakuwa na bima ya moto maana tungekuwa na bima tusingepata kazi kubwa ya
ukarabati na hata samani zilizokuwemo ndani ya mabweni hayo’’alisema Fatuma
Kasenga.
Mabweni saba ya wavulana wa shule hiyo
yaliteketea na moto, pia Vitanda 93,
Magodoro 186, mashuka 372, Mablanketi 186, mabegi 186, matranker 186 pamoja na
vitabu na madaftari, vyote vikiwa na jumla ya Milioni 30 viliteketea.
Uongozi wa
shule umesema, umefanikiwa kuwanunulia wanafunzi mablanketi na vitanda 72, huku
wanafunzi wakiwa bado wanahitaji msaada wa kiutu zikiwemo nguo za shule na
kushindia, madaftari na vitabu.
Jumuiya hiyo
ya wazazi wa CCM, kwa mkoa wa Mbeya ina jumla ya shule 18 ambazo zote hazina bima
ya moto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni