VIJANA
wajasiliamali mkoani Mbeya, wametakiwa kuunda vikundi vinavyoanzia watu watano
kisha kupelekwa taarifa ofisi ya Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dr, Mary
Mwanjelwa ambaye atawapatia fedha za kusajili vikundi hivyo.
Ahadi hiyo
imetangazwa na Mbunge huyo alipokuwa akiwahutubia vijana wa Boda boda njia
panda Itende kata ya Kalobe na vijana wa eneo la Sido Jijini Mbeya.
Dr.
Mwanjelwa, alisema kuwa atagharamia fedha za usajili kwa vikundi vyote vya
ujasiliamali hasa kwa vijana na wanawake ambao wataunda vikundi hivyo.
‘’ Kwa sasa
benki ya wanawake inakuja Mbeya na tayari kibali kutoka benki kuu kimepatikana,
watakaounda vikundi ndiyo watakaoanza kupata mikopo ya riba nafuu’’ alisema Dr.
Mwanjelwa.
Alisema kuwa
licha ya kuitwa benki ya wanawake, lakini itatoa mikopo kwa watu wote bila
kujali jinsi ya mtu.
Akisoma
risala ya vijana waendesha bodaboda wa Njia panda Itende, Mwenyekiti wa vijana
hao, Lwitiko Kibona, alisema kuwa vijana wa shina hilo wapo 33 na tayari wana
kiasi cha Shilingi 99,000/=.
‘’Tunachangishana
1,000/= kwa kila mmoja kila mwezi na lengo likiwa kila mmoja awe anamiliki
pikipiki yak wake tofauti na sasa ambapo wanaendesha pikipiki za matajiri na
kupeleka malengo’’ alisema Kibona.
Naye Docas
Nzunda na Tito Ndunguru, kutoka katika kikundi cha vijana kata ya Kalobe,
walisema kuwa wameanzisha kikundi kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.
Dr.
Mwanjelwa, aliviwezesha kiasi cha Shilingi 40,000/= kila kikundi kwa ajili ya
usajili na kuahidi kuwapatia vijana wa Bodaboda pikipiki moja kama mtaji wa
kitega uchumi chao.
Wakati huo
huo, aliweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kukoboa Mpunga cha kikundi cha
Mbeya Aman Group cha Sido Mwanjelwa Jijini hapa na kuwachangia kiasi cha
Shilingi 500,000/= kwa ajili ya kuongezea katika ununuzi wa mitambo ya kiwanda
hicho kidogo.
Pia Mbunge
huyo, alitoa kiasi cha Shilingi 100,000 kwa Muungano wa jamii Tanzania(MUJATA)
baada ya kualikwa na kupewa Baraka na machifu wa mkoa wa Mbeya.
Mkuu wa mila
wa kanda ya Nyanda za juu kusini, Rocket Mwashinga, alisema kuwa, wanasiasa
wanaoanzisha vurugu watafanya kazi mchana lakini usiku watalala ndipo wao kama
wazee watafanya kazi zao.
Katibu wa
wajasiliamali wa kikundi cha Aman Group, Mustapha Ntupwa, alisema mbali na
kikundi hicho kuwa ni cha uchumi, pia lengo lake ni kupiga vita matumizi ya
dawa za kulevya na kutunza mazingira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni