1. UTANGULIZI
ASILIMIA ya
Wanaume katika uongozi ni kubwa kuliko ya Wanawake. Hii ni katika Nyanja zote.
Na sio kwa Tanzania tu, tatizo hili ni a kidunia.
Kutokana na
data za Bunge la Kidunia, Wanawake wameendelea kuwa ni ‘’minolity’’ katika Mabunge,
wakiwa ni asilimia 12.7 dunia nzima(1999). Hii ni pamoja na kwamba Wanawake ndio
wapiga kura walio wengi.
Asilimia kubwa
Bungeni kwenye nchi za Nordic ilikuwa asilimia 38.9, na asilimia ndogo ilikuwa
3.4 katika nchi za Uarabuni. Nchi za Nordic walifanikiw kutokana na kuwathamini
wanawake kiusawa katika elimu na umuhimu wao wa kupiga kura.
2. WANAWAKE.
Uwezo wa
kuongoza hauangalii jinsia. Mtu yeyote anaweza kuongoza. karama na uwezo wa
mtu.
Tanzania Wanawake hawajashirikishwa kwa asilimia ya kutosha. Mfano; Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wamekuwa ni wanaume tangu enzi na enzi hizo, na dalili ya kubadilisha hili ni finyu.
Itabidi tuliangalie kwenye katiba mpya kama Wanawake kwa maana ya kwamba tunaendelea na mchakato wa katiba mpya.
Tanzania Wanawake hawajashirikishwa kwa asilimia ya kutosha. Mfano; Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wamekuwa ni wanaume tangu enzi na enzi hizo, na dalili ya kubadilisha hili ni finyu.
Itabidi tuliangalie kwenye katiba mpya kama Wanawake kwa maana ya kwamba tunaendelea na mchakato wa katiba mpya.
Wanawake wanaonekana
kuwa sehemu yao ni kazi za nyumbani tu, kuzaa watoto, kulea familia na wanaume,
hivyo hawana sauti.
3. MWANAMKE KATIKA MAAMUZI KIDUNIA
Kidunia,
maamuzi mengi yamekuwa yakifanyika kuhakikisha wanawake wanapata haki sawa na
wanaume katika maamuzi ya uongozi na utawala (Platform for Action 1995 (SADC)
ambayo inataka serikali iji-commit katika suala zima la usawa wa kijinsia
katika ngazi zote-sheria, uwakilishi wa wananchi, Executive, taasisi binafsi,
Asasi mbalimbali n.k Viongezeke.
Tanzania,
kabla ya uhuru mwaka 1961 ilikuwa inatawaliwa kichifu ingawa tulitofautiana
kijamii. Machifu hawa walikuwa ni wanaume.
Tanzania Wanawake
ni asilimia 52 zaidi ya wanaume. Hii ina maana kwamba mchango wao katika jamii,
uchumi pia ni mkubwa kulinganisha na wanaume.
Ingawa serikali
na vyama vya siasa wanazungumzia umuhimu wa kuwashirikisha wanawake katika
maamuzi, bado asilimia ni ndogo; haijafanya juhudi za utekelezaji wa kutosha.
Tanzania,
statistics za vyama vingi(Multi parties) ilianza mwaka 1995. Kwa sasa Tanzania
Mawaziri wanawake ni 9 kati ya mawaziri wanaume 30.
Wabunge wanawake sasa ni 100 kati ya wabunge 350 na hii ni kwasababu ya viti maalum.
Wabunge wanawake sasa ni 100 kati ya wabunge 350 na hii ni kwasababu ya viti maalum.
Katiba ibara
ya 46 (1)(a)(g)-Haki za wanawake; Kuheshimiwa, kuthaminiwa, kutambuliwa.
4. SABABU ZINAZOSABABISHA MWANAMKE
KUTOPEWA NAFASI ZA KIMAAMUZI.
· Mila na desturi, katika nchi nyingi
Wanawake wanachukuliwa kama daraja la pili.
· Structure ya kisiasa ilivyokaa na
utawala wake(tunahitaji hii tuibadilishe na iingie kwenye katiba mpya) i.e viti
maalum 50/50 majimboni.
· Wanawake kutojiamini.
· Social Attitude i.e Wanawake
kutopendana, i.e wivu roho ya kwa nini?
5. MAONI NA
MWELEKEO UJAO-TUFANYEJE?
· Wanawake LAZIMA wawe ‘empowered’ wawe
‘sensitized’ wapewe mafunzo na wawekwe vizuri katika uongozi/ujuzi ili waweze
kushiriki vema kama walivyo Wanaume.
Wanawake ambao wako kwenye uongozi
waungane kuwapa moyo wengine na kuwasaidia, wasiwe wabinafsi ili nao wagombee
nafasi mbalimbali katika level zote na kuwa kitu kimoja na sauti moja kama
Wanawake. Wasijione wao zaidi kwa vile wamepata.
· Wanawake wanaharakati wasaidie
kupinga vikali mila potofu zozote za kumdidimiza mwanamke.
· ‘Empowerment’ ya Mwanamke ianze ndani
ya famiia, watoto wa kike na wa Kiume tangia umri mdogo wanavyolelewa. Hii itasaidia
maana mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
· Serikali pia iandae program maalum ya
–empower Wanawake (capacity bulding).
· Kuwepo na tume/chombo cha
kushughulikia haki na masuala ya Wanawake tu.
· Wanawake wasibaguliwe.
AHSANTENI
!!!!!!
ZAIDI SOMA
MTANDAO WA MBUNGE HUYO www.marymwanjelwa.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni