*Asema
anakerwa na matumizi ya fedha kutafuta uongozi
*************************************************************************
NAIBU waziri
wa Wizara ya Mawasiliano sayansi na teknolojia, January Makamba, ambaye pia ni Munge wa Jimbo la Bumbuli, ametumia
dakika 17 kueleza kwanini anaweza kuwania nafasi ya Urais mwaka 2015 kupitia
Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Alitumia
muda huo baada ya mmoja wa waadhiri wa vyuo na vyuo vikuu mkoani Mbeya kutaka
kujua uhalisia wa uvumi kuwa yeye ni miongozi mwa vijana wa CCM ambao wanatajwa
kuwa watawania nafasi hiyo.
Makamba
alisema kuwa, makundi ya watu wa rika mbalimbali wameendelea kumshawishi
kuwania nafasi hiyo mwaka 2015 na kumtaka atafakari na kuchukua hatua.
Alisema kuwania
nafasi hiyo ni jambo kubwa sana hasa wakati huu ambao yeye anakerwa na matumizi
ya fedha yenye lengo la kupata uongozi.
‘’Nakerwa
sana na matumizi ya fedha kutafuta uongozi jambo ambalo linawanyima fursa watu
wenye vipawa vya uongozi kutuongoza, mimi sina hela, lakini kadri siku
zinavyozidi kwenda watu wanazidi kunifuata’’alisema Makamba.
Alisema
kabla hajachukua hatua ya kutamka kuwa atagombea, anaendelea kutafakari kama
kazi yenyewe ataiweza au la kwasababu kazi ya kuwa Rais si kazi yeye na familia
yake bali ni ya kuwatumikia watanzania.
‘’Natafakari
kuwa je! Ninaweza kuungwa mkono na watu wote Tanzania? Isije ikawa ni kikundi
cha ndugu au marafiki pekee ndiyo wanakuunga mkono, Urais siyo wa Bumbuli tu’’
alisema Makamba.
Aliongeza
kuwa tafakuri yake ni kwamba akijiridhisha kuwa atapata wapi fedha za kuendeshea
nchi katika utawala bora, elimu na mambo mengine, atatamka rasmi kuwa anagombea
nafasi hiyo kubwa na ya heshima.
‘’Ni rahisi
kusema kuwa unataka kugombea, lakini ni lazima ujiulize maswali kadhaa yakiwemo
kuwa je unaweza kuwaridhisha watanzania kimwili, kiakiri, kifikra na kuwa na
fikra za kubadili nchi kuwa kwanini tumeshindwa mahala fulani na tunawezaje
kuziba mapengo hayo. Hivyo mimi bado natafakari’’ alisema Naibu Waziri huyo.
Katika
kongamano hilo lililolenga kuwakaribisha wanafunzi ambao ni wanaCCM wa mwaka wa
kwanza katika vyuo hivyo, Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary
Mwanjelwa alitoa mada ya asilimia hamsini kwa hamsini ya uogozi kwa wanawake.
Alisema ili
kufikia kiwango hicho cha Hamsini kwa hamsini, ni lazima wanawake waache
kuchukiana na jamii iwape nafasi wanawake katika nafasi za kiungozi.
‘’Wanawake
ndiyo wapiga kura wakubwa na Tanzania takwimu zinaonesha kuwa wanawake ni
asilimia 52, lakini wanawake tuna tatizo la kutoungana mkono na kuchukiana’’
alisema Dr. Mwanjelwa.
Mkuu wa
wilaya ya Mbeya, Dr. Norman Sigalla, alitoa mada ya ukosefu wa ajira kwa wasomi
ambapo alisema kuwa wasomi wengi hawafanikiwi kwasababu wanachagua kazi za
kufanya.
‘’Hakuna
serikali yeyote duniani ambayo inaajiri wasomi wake wote, na ukiangalia
wafanyabiashara wakubwa zaidi ya asilimia 86 hawana elimu ya kidato cha sita
ama shahada’’ alisema Dr. Sigalla.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni