Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya wakimsikilkiza Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akitoa maelekezo ya serikali kuhusu zao la Pareo akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mhe Oran Njeza akizungumza katika mkutano huo kufikisha kilio cha wananchi mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwwa kuhusu zao la Pareto na matatizo la wafanyabiashara kujaza Lumbesa kwenye uuzaji wa mazao mbalimbali likiwemo zao la viazi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijijini Jojo Kata ya Santilya, Jana Novemba 29, 2017.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya wakimsikilkiza Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akitoa maelekezo ya serikali kuhusu zao la Pareo akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
Na Mathias Canal, Mbeya
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Jana Novemba 29, 2017 amemuagiza Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kumsimamisha kazi Afisa Kilimo Wilaya ya Mbeya anayesimamia zao la Pareto Ndg Emmanuel Halinga ili kupisha uchunguzi.
Mhe Naibu Waziri ametoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania mara baada ya Mhe Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Oran Njeza na Wananchi wote waliokuwepo kwenye mkutano huo wa hadhara kumrushia shutuma nzito na kumkataa mtaalamu huyo wa kilimo mbele ya Naibu Waziri.
Alisema kuwa pamoja na zao hilo la Pareto kuwa la kwanza kwa uzalishaji katika nchi za Afrika huku likiwa zao la pili kwa uzalishaji Duniani lakini bado halijamkomboa Mkulima nchini jambo ambalo linaonyesha namna ambavyo baadhi ya wataalamu Wa Kilimo wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Alisema kuwa wataalamu wa kilimo walipaswa kusimamia kwa kiasi kikubwa zao hilo kwani Pato lake ni wastani wa tani 2000 kwa mwaka sawa na Bilioni 12 mpaka 14 ambapo katika kipindi hili bei ya kuanzia Mkulima analipwa shilingi 2300 kwa kilo lakini inapanda mpaka shilingi 3300 kulingana na ubora wa zao hilo ambalo mkulima amelima.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inaamini katika kazi ambazo matokeo yake yanapaswa kuonekana hivyo Mkulima kushindwa kunufaika na mazao ya Kilimo ni uzembe wa baadhi ya wataalamu Wa Kilimo unaosababishwa na kufanya kazi kwa mazoea.
Aidha, Mhe Mwanjelwa ametoa siku saba kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Pareto nchini Ndg Lucas Ayo kutoa sababu za kwanini mnunuzi ni mmoja wa zao hilo jambo ambalo linaonyesha kuwa na harufu ya rushwa au kupelekea kudumaza solo la zao hilo kwa kuwa na mnunuzi mmoja asiyekuwa na ushindani.
Ili kuongeza ufanisi wa zao hilo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ameelekeza wakulima Kuanzisha vikundi vya vyama vya ushirika vya msingi ambavyo vitakuwa na usajili serikalini kwani vitasaidia kuwa na mjadala wa jinsi ya kuwa na ubora wa zao la pareto jambo litakalopekea kuanzisha viwanda vidogo ambavyo ni ishara ya kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuwa na Tanzania ya Viwanda.
"Mkishaanzisha tu vikundi vya vyama vya ushirika mtoe taarifa mapema iwezekanavyo na serikali kupitia mrajisi itatoa Elimu ya ushirika" Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Ameagiza zao la Pareto kuwa huru ili mkulima awe huru kuuza kwa mnunuzi anayemtaka kwani kwa sasa kuna mnunuzi mmoja tu ambaye anajipangia mwenyewe namna ya kununua zao hilo kwa gharama atakazo pasina kupingwa.
Pia alielekeza wakulima Kuingia kwenye Kilimo cha mkataba kati yao na Chama cha msingi (AMCOS) jambo litakalorahisisha kupata mikopo ya Kilimo kupitia Benki ya Kilimo nchini (TADB).
Kuhusu Lumbesa, aliwataka wafanyabiashara wa wanaojaza Lumbesa badala ya kujazwa kilo 100 kwa gunia lakini linajazwa mpaka kilo 120 kuacha haraka tabia hiyo kwani wanakwenda kinyume na sheria hivyo kwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua Kali za kisheria.
Mary Mwanjelwa wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza kati ya mikutano saba (7) katika Kanda saba (7) za kilimo nchini inayotegemewa kufanyika ambao ni muhimu kwa makatibu tawala na washauri wa kilimo wa mikoa ya nyanda za juu kusini wa kuelimishana kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi ambao umefunguliwa rasmi.
Mhe Naibu Waziri wa Kilimo aliwasihi Makatibu Tawala hao wa Mikoa na wataalamu wa kilimo kuhakikisha kwamba wanasimamia bei elekezi ya mbolea, Wanatoa Elimu kwa Wakulima ili wanunue mbolea bora na pia kuimarisha vikundi vya wakulima ili waweze kutumia nguvu ya umoja katika kuboresha kilimo kwa ajili ya utoshelevu wa mahitaji ya kaya zao na kuuza ziada hapa nchini na nchi za nje.
Alisema kuwa wafanyabiashara licha ya kufahamu kuwa wanatakiwa kugawana faida na wauzaji wa rejareja lakini bado wanakiuka taratibu za kisheria hivyo aliwaagiza kuacha tabia hiyo ili mawakala wauze kwa rejareja na kwa bei elekezi bila kuathiri biashara zao.
Alisema Katika Sekta ya Kilimo mbolea ni moja ya pembejeo zinazohitaji ushirikiano mkubwa kutokana na ukweli kwamba inahitajika kwa wingi na ina gharama kubwa, inahitaji utaalamu katika matumizi yake na kwamba ni bidhaa inayoharibika kwa haraka endapo viwango vya utunzaji wake havizingatiwi.
Mhe Mwanjelwa aliwaagiza wakaguzi wote wa mbolea nchini kufuatilia na kuhakikisha kwamba kila mfanyabiashara wa mbolea ana leseni ya kufanya biashara ya mbolea ambayo itatolewa bure na TFRA na pia wahakikishe kwamba wote wamepata mafunzo haraka iwezekanavyo.
“Mbolea ni moja ya vichocheo vikubwa sana katika suala hili na hivyo, mwisho wa mkutano huu tunategemea kupata taarifa ya mikakati ya namna Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zitakavyosimamia ubora na bei elekezi ya mbolea ili Mkulima aweze kuipata na kuitumia kwa lengo linalokusudiwa” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Naibu Waziri huyo alisema kuwa Wizara ya kilimo ilitunga Kanuni ya Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (Fertilizer Bulk Procurement Regulations) na kuzitangaza kwenye Gazeti la Serikali kupitia tangazo G.N. 49/2017. Pamoja na kuunda kanuni hizo, Wizara ya kilimo ilirekebisha Kanuni ya Mbolea ya mwaka 2011 kwa Kanuni zilizotangazwa katika Gazeti la Serikali kwa tangazo G.N. Na. 50/2017 ili kuipa nguvu TFRA kukokotoa, kutangaza na kusimamia bei elekezi ya mbolea.
Aliwaagiza pia wafanyabiashara wanaotunza mbolea bila kuzingatia viwango vilivyowekwa na TFRA kuacha haraka tabia hiyo kwani kwani wanasababisha mbolea kumfikia mkulima ikiwa imepungua ubora au kuharibika kabisa na hivyo kumfanya mkulima asipate tija inayotokana na matumizi ya mbolea.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amewataka wataalamu hao Kutenda haki katika uwajibikaji wao, Kufanya kazi kwa weledi, uaminifu, uwajibikaji uliotukuka, na nidhamu ya hali ya juu.
Aliongeza kuwa kwa yeyote atakaye kwenda kinyume na matakwa ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli itamchukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria.