Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akisikiliza kwa makini taarifa kuhusu utekelezwaji wa maagizo ya waziri Mkuu mara baada ya kutembeleaa kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza kwa makini taarifa kuhusu utekelezwaji wa maagizo ya waziri Mkuu mara baada ya kutembeleaa kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
Muonekano wa vitendea kazi vya kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd).
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
Muonekano wa baadhi ya vitendea kazi vya Kiwanda cha mbolea cha Minjingu kilichopo eneo na Kata ya Minjingu Mkoani Manyara.
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ametembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) kilichopo katika eneo na Kata ya Minjingu Mkoani Manyara ambapo pamoja na mambo mengine amejionea hali ya uzalishaji wa mbolea asilia ya kupandia aina ya Minjingu.
Mhe Mwanjelwa alitembelea kiwandani hapo ambapo miongoni mwa matakwa yake ilikuwa ni pamoja na kufatilia maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu alitembelea eneo la machimbo ya mbolea ya Minjingu na kupokea taarifa ya uendeshaji wa Kiwanda cha Mbolea cha Minjingu.
Mhe Mwanjelwa alishuhudia uzalishaji ukiwa umeongezeka kufikia Tani 150,000 kwa mwaka ambapo uongozi wa kiwanda hicho umetii agizo la Waziri Mkuu la kuwasihi kuboresha teknolojia ili kuzalisha Tani zaidi ya 150,000 ambazo zitaongeza kiwango cha upatikanaji wa mbolea hapa nchini kwwani bado upo chini kuliko mahitaji
Katika hatua nyingine Uongozi wa kiwanda hicho ulitii agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye aliwagiza kuandika barua kwa Mhe Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pomnbe Magufuli kuomba radhi kwani mifuko waliyokuwa wanatumia kuuzia Mbolea hiyo ya Minjingu ilikuwa na nembo ya nchi ya Kenya licha ya kuwa inazalishwa hapa nchini.
Hata hivyo Mhe Mwanjelwa alijionea mifuko hiyo ikiwa imebadilishwa na kuwa na muonekano wa anuani ya Tanzania kama uzalishwaji wake ulivyo.
Sambamba na hayo pia Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ameutaka uongozi wa kiwanda hicho cha mbolea Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) kutoa elimu kwa umma juu ya ubora na umuhimu wa mbolea hiyo ya kupandia.
Mbolea hiyo inatokana na miamba inayochimbwa katika eneo la Minjingu Mkoani Manyara ambayo husagwa na kufungashwa kwenye kiwanda kilichojengwa katika eneo hilo. Mbolea ya Minjingu imeboreshwa kwa kuongezwa virutubisho vya Nitrogen, Salfa, Magnesi, Zinki na Boron (N, S, Mg, Zn, na B).
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky) ameiomba serikali kupitia wizara ya kilimo kuwaruhusu maafisa ugani kote nchini kupatiwa mafunzo maalumu yatakayowaimarisha ili waweze kuwa sehemu ya kuitangaza mbolea bora ya Minjingu ambayo inazalishwa nchini.
Alisema kuwa serikali inapaswa kutazama upya utozaji wa VAT kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali hapa nchini kwani tozo ya VAT ya asilimia 18 wanayotozwa ni kubwa huku waagizaji wa mbolea nje ya nchi wao wanaingiza pasipo tozo kama hiyo.
Aidha, alisema kuwa tayari makala za vipindi vya Redio, Televisheni na Magazeti mbalimbali zimeanza kuandaliwa kwa ajili ya kuelimisha wakulima juu ya umuhimu wa mbolea hiyo ya Minjingu ambayo ni bora kuliko mbolea nyingine yoyote nchini na nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imejidhatiti katika viwanda hivyo inathamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni