Jumatatu, 20 Novemba 2017

MHE MWANJELWA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA IBIGI, APOKEA WANACHAMA WAPYA 21



Na Mwandishi wetu

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo amewasihi wananchi kwa kauli moja kuchagua kiongozi makini anayetokana na CCM.

Mhe Mwanjelwa alisema kuwa kumchagua diwani wa CCM ni dalili nzuri ya kumpongeza na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anazozifanya kwa muktadha wa kuwaletea maendeleo watanzania wote.

Mjumbe huyo wa NEC, aliyasema hayo Leo Novemba 20, 2017 katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Bujinga A na B kilichopo Kata ya Ibigi, Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya ambapo alimnadi mgombea Udiwani wa Kata hiyo Bi Suma Ikenda Fyandomo.

(Mnec), Mhe Mwanjelwa aliwakumbusha wananchi waliojitokeza katika mkutano huo kuwa Hawachagui ilani mpya Bali wanachagua Diwani kwa ajili ya kutekeleza ilani ya Ushindi ya CCM ya Mwaka 2015-2020 ambayo wananchi waliiamini na kuichagua Octoba 25, 2015.


Alisema kuwa nchini Tanzania hakuna chama chenye uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi Bali Chama Cha Mapinduzi pekee ndicho chenye uwezo na jukumu la kuwaletea maendeleo endelevu wananchi.


Katika Mkutano huo wanachama 21 walivutiwa na hotuba ya Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya CCM wakati akimnadi mgombea hivyo kufanya maamuzi ya kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM ambapo wameahidi kushirikiana na mgombea udiwani wa CCM ili kuhakikisha anashinda kwa kishindo.


Ushiriki wa kampeni hizo katika Kata ya Ibigi unajili wakati ambapo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa yupo ziarani Mkoani Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine Kesho Disemba 21, 2017 atashiriki ufunguzi wa Mkutano wa Makatibu Tawala na washauri wa kilimo wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini juu ya mfumo wa ununuzi wa mbolea (BPS).


Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa Jijini Mbeya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...